Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

hongera sana Mh Mbowe huo ndio uungwana maana upo kwa ajili ya manufaa ya watu wengi
 
Vijana wa Mwendazake WAMEPOTEANA, hakika MHALIFU yule kifo chake kitaiponya Tanzania.
 
Hivi siku Wana CHADEMA wakija Gundua kua Mbowe ni Afisa kipenyo Wa inner ya inner cycle sijui itakuaje?!

Hata wakuu wa nchi taarifa hii huwa hawapewi, Ila Mama alikaza, alitaka kumpoteza, ikafikia hatua Sasa hakuna namna, ikabidi apewe taarifa ya kua huyu ni mwenzao katika ujenzi wa taifa. Asante Baba wa taifa kwa kuasis watch Dog.

Dk. Slaa, Hongera kwa kustaafu kazi maalum. Lakini Consultancy yako itaendelea. Legacy yako itadumu kwa kipindi kirefu.

Hawa makomandoo Wana bahati Sana, issue yao ilidhaniwa kua ile ya MKKIRU.

Na huenda wakakamatwa tena.

Oh!, kumbe asubuhi imefika!? Kumbe naota?! Duh!, afadhali. Mapigo ya moyo naona yapo 120b/m. Pressure imepanda.
Baba yenu mwendazake alikuwa MHALIFU sana, kama angeendelea kuishi hakika angetumaliza sote .
 
Tukubaliane kwamba bila katiba mpya hakuna uchaguzi na kama ccm watalazimisha basi waende kwenye huo "Uchaguzi" na vile vyama vyake tanzu tu.
 
Baba yenu mwendazake alikuwa MHALIFU sana, kama angeendelea kuishi hakika angetumaliza sote.
Hahahaha! Nje kabisa na kinacho zungumzwa.

Naona unahangaika na marehemu.

Si bure,utakua unahangaishwa na mizimu.
 
Cheza na kitu kingine, si Rais au Mkuu wa nchi, utajutia milele
 

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe Ikulu Mkoani Dar Es Salaam.

Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.

Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

====

Picha Mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022

Mikopo mikopo misaada misaada hakuna kingine
 
Hivi mmeshinda kesi au DPP kaamua kutoendelea na kesi- leteni majivuno tu maana sheria inamruhusu DPP kuanza kesi upya- miezi mingine 9
Ameamua kutoendelea na kesi baada ya kuona haina mashiko na haina tija kwa Taifa. Ushahidi wa mashahidi wa jamhuri umemfanya DPP akafikia hatua ya kutokua na nia ya kuendelea na hiyo kesi.

Kesi ilikua imeisha baada ya jamhuri kufunga ushahidi, lakini unajua nini kiliirefusha ifike ilipofika. Palitafutwa penye unafuu wa kumaliza kesi ili "kuhifadhi heshima"
 
Ameamua kutoendelea na kesi baada ya kuona haina mashiko na haina tija kwa Taifa. Ushahidi wa mashahidi wa jamhuri umemfanya DPP akafikia hatua ya kutokua na nia ya kuendelea na hiyo kesi.

Kesi ilikua imeisha baada ya jamhuri kufunga ushahidi, lakini unajua nini kiliirefusha ifike ilipofika. Palitafutwa penye unafuu wa kumaliza kesi ili "kuhifadhi heshima"
Jamhuri ilishafunga ushahidi wake na Mbowe kuonekana na kesi ya kijibu- umetoka lini mwezini?
 
Wanasiasa wa Tanzania wanapaswa kujigunza kwa Mbowe ni Jasiri, anajua siasa, mvumilivu licha ya yote ameenda kwa adui yake kuonana.
 
Kiongozi huwa hayumbishwi, anateleza bila kuanguka.
Kwa hiyo 'Mama Mizinguo' aliteleza bila kuanguka safari hii; je unajuaje kwamba hatateleza na kuanguka kabisa huko mbeleni? Maanake, mtu akiteleza hana uamzi wa ama aanguke au asianguke!
 
Hahahaha! Nje kabisa na kinacho zungumzwa.

Naona unahangaika na marehemu.

Si bure,utakua unahangaishwa na mizimu.
Mwendazake aliwaambikiza UHALIFU vijana wengi huko UVCCM kama sabaya, kwa tukio hili ni lazima KUPOTEANA kuwepo tu.
 
Kwa hiyo 'Mama Mizinguo' aliteleza bila kuanguka safari hii; je unajuaje kwamba hatateleza na kuanguka kabisa huko mbeleni? Maanake, mtu akiteleza hana uamzi wa ama aanguke au asianguke!
Binadamu ndivyotulivyo umbiwa, lakini tutafika.
 
Back
Top Bottom