Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atakutana na mjumbe maalum (Special envoy)wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta leo katika ikulu Dar Es Salaam.
Uhusiano Kati ya Kenya na Tanzania ni moja Kati ya masuala yanayotarajiwa kupewa kipaumbele ikizingatiwa kuwa urafiki wa nchi hizi mbili 'ulivurugika' Sana katika kipindi cha Hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Ikumbukwe siku zote Rais Kenyatta amesisitiza kuwa Tanzania ndiyo taifa muhimu zaidi kwake na halioni kama mshindani bali kama mshirika wa kimkakati(Strategic partner).
Rais Uhuru Kenyatta anaijua Tanzania,amekuwa akija Tanzania kabla ya kuwa Waziri,alikuwa akija kufanya starehe Dar!!,anao marafiki na Biashara hapa Tanzania.
Tanzania ni nchi muhimu,ni kwa vile viongozi wengi wa Tanzania hawana mitazamo ya kibiashara,wanakosa ubunifu.
Sidhani kama viongozi Tanzania wanajua; 1
1.umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi.
2.Hakuna kiongozi aliye na biadhara nje ya nchi.
3.Hakuna kiongozi anayeamini kuwa nchi zinazotuzungika ni "FURSA"
4.Hakuna kiongozi anayefikiria tukijenga na kuwa na bandari nyingi ni "Fursa".
5.Hakuna kiongozi anayeaamini KILWA inaweza kuwa na bandari na tukahufumia Zambia,Malawi na DRC(upande wa Lubumbashi).
6.Hakuna kiongozi anayeamini au kufikiria MTWARA inaweza kuwa na Bandari kubwa itakayo hudumia Msumbiji,Zambia,Malawi na DRC.
7.Sijui kama Viongozi wa juu wanafikiria kueweka vivutio ili wawekezaji waende mikoa inayopakana na nchi jirani:
8.Mtwara inaweza kuwa na viwanda vyenye bidhaa za kuuza Msimbiji,Malawi,Zambia na DRC.
9.Kigoma inaweza kuwa na Viwanda vya výenye bidhaa za kuhudumia Maziwa Makuu!!!
10.Rais kwenye ziara asiwasahau Waziri wa Uwekezaji,Biashara na Viwanda.!