IKULU, inakuwaje Rais anasimama upande wa kushoto halafu Dangote kulia? Hamna watu wa Protocol?

IKULU, inakuwaje Rais anasimama upande wa kushoto halafu Dangote kulia? Hamna watu wa Protocol?

Ni mimi tu ndo macho yangu yana makengeza???
Maana naona Samia yupo Kulia na Dangote yupo Kushoto.
Dangote amesimama upande wa kulia wa mama samia.

Wajuaji wanataka Dangote asimame upande wa kushoto wa Mama Samia. Umeelewa?

Kama bado hujaelewa njoo PM
 
Hii picha ni ile ile kama iliyopo hapo juu ila wahusika wamepishanishwa namana ya kusimama kwa kuchezea picha

Kuthibitisha angalia maeneo yafuatayo
1. Mwelekeo wa ngazi na zulia jekundu
2. Swichi nyekundu ya king'ora hapo kwenye langu la kuingilia mjengoni
3. Mkono wa Mh Rais SSH ambao haukukunjwa ngumi
4. Mguu ambao kiatu kimefunikwa na gauni
5. Mwinamo wa shingo wa Mh Rais SSH
6. Taswira ya Dangote alivyosimama, mwelekeo wa uso na miguu ilivyosimama
7. Swichi nyekendu iliyonyuma ya Dangote amepinduka nayo upande ule ule
8. Maandishi yaliyo chini ya nembo ya bibi na bwana yamepinduka kinyume nyume

Hitimisho picha imechezewa kuhalalisha changamoto ambayo mtoa mada amepewa na mdau wa JF, kwa hiyo picha ya kwanza kabisa na hii hapa ni moja .
 
Kwa kweli ni Jambo la Aibu kusahau mambo muhim hivi! ina maana Dangote kicheo ni mkubwa kuliko mama yetu?

Hizi aibu zisijirudie! hata mpiga picha hajui protokali?

daah noma kweliView attachment 1796531
Hivi hii ilikuwa selfie nini!?
images%20(15).jpg
 
Vitu vingine ni vidogo jamani, tujaribu zaidi kujadili mambo ya bread n butter... sasa mnashindwa kupigania na kupata ufumbuzi wa mambo muhimu kama bei ya mafuta ya kula au cement ishuke, nyie mnakazania vitu ' subjective'... kaazi kweli kweli....kazi iendelee.
Mambo mengine mkuu tumerithi Kwa wakoloni tu lakin kimsingi hayana maana yoyote wala athari zozote kiuchumi, kiutamaduni wala kisiasa.
 
Ukiachana na hayo yote, huyo jamaa hapo pembeni ndiye mtu mweusi mwenye hela kuliko wote duniani....sio mchezo.
 
Kwani kwa kusimama kwa namna hiyo huyo Dangote na Rais Samoa wanapata au wanapoteza nini kila mmoja?

Naelewa kuwa "protocol" ni utaratibu na unapokuwa haufuatwi, mambo yatakwenda shaghala baghala...

Hata hivyo siyo wakati wote na mahali popote na mazingira yoyote the so called "protocol" matters...!!

Kwa hapa, mimi sioni tatizo lolote kwa sbb mwisho kila mmoja wao anaendelea na shughuli zake
 
Jamani tufikiria mambo ya msingi sasa mbona picha pili iko sawa au wamerudia baada kutoa lalamiko ? Mataga buanaaa
 
Kuna maana ya kuwa na protocol, huyo mama yenu analojua ni lipi sasa kama ya maana hajui hata haya madogo pia yanamshinda?
Lipi asilolijua ambalo wewe unalijuwa zaidi mmepatikana mara hii rais kutoka zanzibar halafu ni mwanamke halafu zaidi si dikteta kama magufuli mpaka sasa hakuna moja aliloharibu ila nchi inaiweka sawa kakuta nchi imevurugika kabisa chini ya dikteta na genge lake la wizi na kuhadaa wananchi kwamba yeye ni rais wa wanyonge.
 
Back
Top Bottom