Nafasi yoyote ya chama cha kisiasa ni nafasi ya kisiasa by definition. Hata nafasi ya utendaji ndani ya chama ni nafasi ya utendaji katika muktadha wa kisiasa.
Maana yake, Katibu Mkuu wa Chama atakuwa mtendaji katika kueneza itikadi ya Chama, hivyo hiyo ni nafasi ya kisiasa.
Katibu Mkuu Kiongozi ni mtu anayeongoza watumishi wa umma ambao hawana open affiliation na chama chochote.Na yeye anaongoza kwa maadili ya utumishi wa umma yanayokataza ushabiki wa vyama.
Sasa Bashiru aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM aende kuongoza utumishi wa umma na kukataza ushabiki wa vyama?
Kumfanya Katibu Mkuu wa CCM kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ni kama kumfanya Kocha wa Yanga ajiuzulu ukocha wa Yanga, halafu aende kuwa refa katika mechi ya Simba na Yanga!
Kazi kubwa ya katibu mkuu( General Secretary) wa CCM, ni kuwa msimamizi mkuu wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kupitia nafasi yake kama mwenyekiti wa sekretarieti ya CCM
Kwa sasa chama cha mapinduzi ( CCM) ndio kinaongoza serikali, baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliopita
Baada ya watanzania wengi kuridhishwa na ilani ya uchaguzi ya CCM( 2020- 2025), watanzania waliamua kuipa kura CCM
Sasa baada ya uchaguzi, ilani ya CCM( chama kilichoshinda uchaguzi) ya miaka 5, upelekwa bungeni na kuwa mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka 5( mpango wa taifa wa maendeleo utengenezwa kutokana na ilani ya chama kilichoshinda uchaguzi mkuu)
Sasa katibu mkuu kiongozi( Chief Secretary) kwa nafasi yake kama mkuu wa utumishi wa umma kwa niabaya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, yeye ndie msimamizi mkuu wa watumishi wote wa umma, ambao utekekeza majukumu yao kulingana na mpango wa maendeleo wa taifa unavyoelekeza
Sasa kwa mheshimiwa Rais kumteua katibu mkuu wa chama tawala, ambaye ndie alikuwa msimamizi mkuu wa ilani ya chama tawala, ambayo kimsingi ndio mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka 5( 2020-2025), kwenda kuwa katibu mkuu kiongozi ( Chief Secretary) na kuwa mkuu wa watumishi wote wa umma, ambao watakuwa wanatekeleza mpango wa maendeleo wa taifa,
B³inafsi naona ni jambo sahihi kabisa kwa sababu Dr Bashiru Ally atakuwa anaujua upasavyo mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5, ambao umetokana na ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo yeye ndio alikuwa msimamizi mkuu wa ilani hiyo