IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Yule Bashiru niliyezoea kumuona wakati wa mijadala ya kwenye TV kwenye vipindi vya mzee Makwahia wa Kuhenga jina la kipindi "Je tutafika?"misimamo yake na huyu wa sasa ni watu wawili tofauti!!!
kweli hujafa hujaumbika
 
Bashiru alivyoteuliwa kuwa KM wa CCM kutoka kwenye Civil Servant mbona hukulalamika? Sasa ameeudishwa alikotoka nayo iwe nongwa?
 
Trump fan bana
 
Katibu Mkuu kiongozi ndio Serikali yenyewe,yani kumteua bashiru hapa kuna kitu Magu anataka kutuchezea keusi kekundu sio bure.
 
Bashiru alivyoteuliwa kuwa KM wa CCM kutoka kwenye Civil Servant mbona hukulalamika? Sasa ameeudishwa alikotoka nayo iwe nongwa?
Pitia historia ya wote waliowahi kushika hiyo nafasi hivi karibuni. Hakuna hata mmoja amewahi kuwa mwanasiasa, tena wote wameondoka kwenye utumishi hawajaingia kwenye siasa.

Hivi kweli unaweza fananisha utumishi wa umma wa Kijazi na Bashiru?

Ngoja tuone
 
Jf ya siku hizi ina vilaza sana. Balozi Kijazi alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Balozi Sefue alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Vipi kuhusu Balozi Mahiga alipokuwa waziri alikuwa balozi wa nchi gani pia?
Bosi, hao wote uliowataja hapo juu walishawahi kuwa mabalozi wetu nchi za nje. Ndo maana wakabaki na tittle hizo!
 
Hongera sana Classmate wangu PS 2000

He was very intelligent

Alituongoza kuanzia mwaka wa kwanza hadi watatu

Alikuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja kwa kuandika na kuzungumza
Hakuwa na muda wa mambo ya kipuuzi na kiujumla mwenendo wake ulikuwa mzuri sana

Ni mswalihina sana

Katibu Mkuu Utumishi Dkt Ndumbaro ni Mwalimu wake pale Mlimani

Anafaa sana kushika wadhifa huo
 

Kwenye mazingira kama haya, it’s natural to be unease, lakini naamini Bashiru ni mtu anayeelewa vizuri sana scope ya kazi anazopewa. Kama KM wa CCM amefanya precisely what katibu mkuu wa chama anapaswa na kutarajiwa kufanya!

Hakuna record inayoonesha kwamba Bashiru alikuwa anapigania CCM hata kabla hajawa KM wa CCM. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kuamini kwamba atapigania CCM hata asipokuwa na nafasi ya uongozi ndani ya chama.

Kwa ujumla, hakuna mtu ambaye ideologically haegemei chama fulani, hata kama sio mwanachama rasmi. Katika civil service wapo hata watumishi ambao ideologically wanaegemea vyama vingine mbali na CCM. Ndiyo maana wakati mwingine baadhi ya siri za Serikali zinakuwa leaked to the Opposition!
 
Reactions: Ame
Hakuna uhusiano wo wote baina ya utumishi serikalini na ilani ya chama cha siasa. Mtumishi wa serikali anafanya kazi kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa umma na anaweza kufanya kazi katika mazingira yo yote ya kisiasa bila kujali itikadi ya chama kilichopo madarakani.

Hivyo katibu mkuu kiongozi hapaswi kuwa mwanasiasa!
 
Bashiru alivyoteuliwa kuwa KM wa CCM kutoka kwenye Civil Servant mbona hukulalamika? Sasa ameeudishwa alikotoka nayo iwe nongwa?
Bashiru hajawahi kuwa civil servant bali public servant, muda wote alikuwa mwanaharakati akifundisha chuo kikuu. Labda kama huelewi, waalimu siyo civil servants bali ni watoa taaluma ambao wanaweza kuwa serikalini au kwenye siasa.
 
..kwa baadhi it is a big.

..na wengine wanaona it is not a big deal.

NB:

..hata Gavana wa BOT aliyeteuliwa na Jpm ni mwanasheria, wakati sheria inaelekeza Gavana wa BOT anapaswa kuwa mtaalamu wa uchumi ama fedha.

Jiwe hana hulka ya kuheshimu sheria ingawa yeye anasisitiza kuwa watu wafuate sheria!! He is an anarchist by nature!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…