Ikulu: Rais Magufuli awataka watendaji kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyao. Awaasa kuridhika na nafasi walizo nazo, siyo kukimbilia Ubunge

Kwa kifupi ni kasema hajali kura na hajali swala la wengi wape. Hii inaweza kusaidia kucounter watoa rushwa ndani ya chama.

Nje ya chama?
Magufuli CCM atawanyorosha
 
Ma RC na DC walijitutumua vifua wakiamini kuwa wanajitengenezea himaya zao.
 
Raisi kaongea kweli kwanini huridhiki na cheo chake, naomba tu awakate wote wenye tamaa.
 
Kwa kifupi ni kasema hajali kura na hajali swala la wengi wape. Hii inaweza kusaidia kucounter watoa rushwa ndani ya chama.

Nje ya chama?
Itasaidia Tena kupata watu Bora wasio jua rushwa kabisa.
 
Kwani stand ya Arusha inatakiwa ijengwe wapi? Huko karibu na bay-pass
Inatakiwa kujengwa eneo la Bondeni City njia ya kwenda Oljoro JKT. Mwanzo eneo lilikuwa Olasiti karibu na bypass sema lilihitaji fidia kubwa. , Ndipo CCM wakataka ijengwe Kule Sakina njia ya kwenda Nairobi..
 
Kitendo cha aliyekuwa RC wa Arusha Mrisho Gambo kutaka aonekane ni mtu mwema huku akiwasiliba viongozi wenzake waonekane wabaya kwa hakika siyo jambo jema.

Kiukweli dhambi ikikomaa matokeo yake ndio haya, Gambo alianza na mbunge Lema lakini hatimaye kaondoka na DC na Mkurugenzi wa jiji huku akiwaacha RPC na Kamanda wa TAKUKURU wakikalia kuti kavu.

" Uswahili swahili" siyo mzuri kwenye uongozi.

Maendeleo hayana vyama 10 Yatosha!
 


“Nimewatimua RC,DC na DED Arusha kwasababu katika kipindi cha miaka miwili walikua wanagombana tu, kila mmoja anajiona Boss, kila mmoja anamtengenezea mizengwe mwenzake, waliniudhi, wanafanya kazi ila nilichukia kuona hawashirikiani, sitaki yakajirudie”

"Nimeona viongozi hawa wapumzike kwanza kama kubishana wakabishanie huko huko uraiani ndani ya Serikali hapana liwe fundisho mvumiliane, kama kubishana na kugombana kagombane na mkeo na watoto wako ndani ya Serikali hapana tuzingatie sheria na maadili na viapo" Rais Dkt John Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…