Ikulu: Rais Samia na viongozi mbalimbali wakati wa futari leo Machi 30, 2023

Ikulu: Rais Samia na viongozi mbalimbali wakati wa futari leo Machi 30, 2023

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris wakati akiwasili kwa ajili ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris wakati wa Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023. Wa kwanza kulia ni Mume wa Makamu huyo wa Rais Douglas Emhoff, Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.

3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris pamoja na Mume wa Makamu huyo wa Rais Douglas Emhoff mara baada ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

1680206327021.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete mara baada ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

1680206672785.png

4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa mara baada ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

1680206709829.png


1680206901429.png
 
NAISUBIRI TEUZI

Mimi mwanamapinduzi, hakika mmenilea.
Mmenifunza ujuzi, elimu kunipatia.
Sasa nawaomba kazi, Ili kujitegemea.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Kwa hapa ninaujuzi, kwa kazi nilosomea.
Na Nikajifunza kazi, tena kwa kujitolea.
Nawaomba viongozi, waweze nifikiria.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Kwa elimu bila kazi, hakika ninaumia.
Vigezo vipo nakizi, sina wa kunitetea.
Mwisho nipate uchizi, mawazo kunizidia.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Mimi sifanyi ajizi, nipo radhi kujitoa.
Sitakuwa mkupuzi, uzalendo utamea.
Kweli nitapiga kazi, hili mtashuhudia.
Naisubiri teuzi, nafasi kunipatia.

Nakuomba kiongozi, Suluhu mama Samia.
Mwanao naomba kazi, niweze kutumikia.
Wasifu ni toshelezi, tafadhali angalia.
Nasubiria teuzi, Suluhu mama Samia.

Ninasubiri teuzi, labda utanichagua.
Nami nitapata kazi, niweze piga hatua.
Niiondoe simanzi, huzuni kuiondoa.
Naisubiri teuzi, Suluhu Mama Samia.


Y H K
2023
 
NAISUBIRI TEUZI

Mimi mwanamapinduzi, hakika mmenilea.
Mmenifunza ujuzi, elimu kunipatia.
Sasa nawaomba kazi, Ili kujitegemea.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Kwa hapa ninaujuzi, kwa kazi nilosomea.
Na Nikajifunza kazi, tena kwa kujitolea.
Nawaomba viongozi, waweze nifikiria.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Kwa elimu bila kazi, hakika ninaumia.
Vigezo vipo nakizi, sina wa kunitetea.
Mwisho nipate uchizi, mawazo kunizidia.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Mimi sifanyi ajizi, nipo radhi kujitoa.
Sitakuwa mkupuzi, uzalendo utamea.
Kweli nitapiga kazi, hili mtashuhudia.
Naisubiri teuzi, nafasi kunipatia.

Nakuomba kiongozi, Suluhu mama Samia.
Mwanao naomba kazi, niweze kutumikia.
Wasifu ni toshelezi, tafadhali angalia.
Nasubiria teuzi, Suluhu mama Samia.

Ninasubiri teuzi, labda utanichagua.
Nami nitapata kazi, niweze piga hatua.
Niiondoe simanzi, huzuni kuiondoa.
Naisubiri teuzi, Suluhu Mama Samia.


Y H K
2023
Watu wana vipaji
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani , miongoni mwa watu wazito waliohudhuria jambo hilo alikuwepo Mwamba wa siasa za Tanzania na Africa Freeman Mbowe .

Taarifa zinadokeza kwamba Freeman Mbowe ama Ustaadh Aboubakar kama anavyojulikana huko Zanzibar amepata wasaa mzuri wa kuteta mambo muhimu kuhusu mustakabhari wa Nchi na Makamu huyo wa Rais wa Marekani .

Yajayo yanafurahisha .
 
Back
Top Bottom