Ikulu: Rais Samia na viongozi mbalimbali wakati wa futari leo Machi 30, 2023

Ikulu: Rais Samia na viongozi mbalimbali wakati wa futari leo Machi 30, 2023

Watu wamejifunza kutoka kwa mwendazake. Sasa hivi uwanja wa chato, watu wanaanikia mahindi.

Yale mambo yakufukuzishana kazi muda wwte hayapo.

Umechelewa kazini hauna kazi , unawekwa selo au unashushwa cheo.

Watu wasiojulikana hawapo sasa.

Matambo yote mwisho unafukiwa ardhini. Tuishi kwa amani na upendo.
 
Muanzisha thread na Mbowe...utasema Mr and Mrs.....

Eti mtu mzito kwenye futari dah...
 
Ni mpuuzi tuu atakayedhani Mbowe atasusia chakula cha pamoja na makamu wa rais wa Marekani
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani , miongoni mwa watu wazito waliohudhuria jambo hilo alikuwepo Mwamba wa siasa za Tanzania na Africa Freeman Mbowe .

Taarifa zinadokeza kwamba Freeman Mbowe amepata wasaa mzuri wa kuteta mambo muhimu na Makamu huyo wa Rais wa Marekani .

Yajayo yanafurahisha .
Shida nn
 
NAISUBIRI TEUZI

Mimi mwanamapinduzi, hakika mmenilea.
Mmenifunza ujuzi, elimu kunipatia.
Sasa nawaomba kazi, Ili kujitegemea.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Kwa hapa ninaujuzi, kwa kazi nilosomea.
Na Nikajifunza kazi, tena kwa kujitolea.
Nawaomba viongozi, waweze nifikiria.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Kwa elimu bila kazi, hakika ninaumia.
Vigezo vipo nakizi, sina wa kunitetea.
Mwisho nipate uchizi, mawazo kunizidia.
Naisubiri teuzi, niweze kujikomboa.

Mimi sifanyi ajizi, nipo radhi kujitoa.
Sitakuwa mkupuzi, uzalendo utamea.
Kweli nitapiga kazi, hili mtashuhudia.
Naisubiri teuzi, nafasi kunipatia.

Nakuomba kiongozi, Suluhu mama Samia.
Mwanao naomba kazi, niweze kutumikia.
Wasifu ni toshelezi, tafadhali angalia.
Nasubiria teuzi, Suluhu mama Samia.

Ninasubiri teuzi, labda utanichagua.
Nami nitapata kazi, niweze piga hatua.
Niiondoe simanzi, huzuni kuiondoa.
Naisubiri teuzi, Suluhu Mama Samia.


Y H K
2023

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom