Ikulu sio wodi ya wagonjwa, Lusinde amnanga Dk. Slaa

Ikulu sio wodi ya wagonjwa, Lusinde amnanga Dk. Slaa

wewe FOXY wa LUMUMBA usiwe zombi kiasi hicho loh!! utadhani ulikaa nae au alikupangia chumba na wewe kujifanya unamjua saaaaanaaa...
nikuswalike hili ukamuulize jeee kale kabinti alikowahi kukapangia geto pale mtaa wa shimo la udongo aka KURASINI na halafu akakatunuku katoto kamoja je alihudhuria mazishi yakeee??
ukinipa jibu ntajua uko karibu nae vinginevyo funga hilo kalio lako usijihusishe usio yajua

Porojo za mitaani hizo, danganyaneni hukohuko.
 
Unaweza kukuta huyu anayetukana ni Diwani wa Chadema.

hahahaa kijana wa LUMUMBA upoooo ulifichwa:mimba:wapi weyee!!! hahaaa

anakusalimia FOXY wako:msela::msela:
 
mkuu hivi mzee slaa anaumwa ugonjwa gani?

uliskia lini anaenda ujerumani kutibiwa?? au usa japo kutibiwa TEZI DUME?

MUULIZE MKUU WA KAYA au EDO ndio wana uhusiano mkubwa na hizo sehemu
 

" NI kweli serikali ya CCM imechoka kwasababu imefanyakazi kubwa sana ya kujenga barabara,mahospitali,madaraja,kuleta maendeleo kwa taifa.

Hata gari likitembea umbali mrefu linachoka linaitaji kufanyiwa sevisi halafu linaendelea na safari.

Kwani hata gari la Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe na Tundu Lissu magari yakitembea umbali mrefu yakichoka hawayatupi wanachokifanya ni kuyafanyia sevisi kisha magari hayo yanaendelea na safari.

Ndio maana nakiri CCM imechoka kwasababu imefanyakazi nzito ya kuleta maendeleo katika nchi ni lazima ichoke ipumzike halafu ndio maana kwenye kampeni za Oktoba mwaka 2015 ,CCM itaomba tena ridhaa ya wananchi ili irudi kuendelea kufanyakazi kubwa zaidi.

UKAWA hawajachoka kwasababu haijafanyakazi ngumu ,UKAWA imekuwa ikifanyakazi nyepesi sana na kazi hiyo ina herufi sita tu ambayo ni kusimama na kusema neno hili(HAPANA). Sasa mtu ambaye ana kazi moja tu ya kusema neno HAPANA kama UKAWA na Chadema ni wazi hawawezi kuchoka maana hawajafanya kazi nzito.Kusema HAPANA kwa kila kitu siyo kazi nzito ndiyo maana UKAWA hawajachoka.

UKAWA wamekuwa wakisema CCM imechoka kwasababu imekaa muda mrefu madarakani, mimi na waambia hivi Chadema wakati mwingine wanajitukana wenyewe kwasababu Mzee Mtei , Dk.Wilbroad Slaa ni wazee lakini ndiyo wanaiongoza Chadema na UKAWA ndio wanamtegemea Slaa awe mgombea urais wakati Slaa ni mgombea urais mzee kuliko wagombea wote na amechoka.

Jamani Ikulu sio wodi ya wagonjwa,Ikulu watu wanatakiwa kwenda kufanyakazi sio kulazwa.

Nasema sumu haionjwi , Ukawa ni sumu na watanzania sio wajinga hawapo tayari kuona sumu kwa kuiweka UKAWA madarakani kwanza UKAWA una sera gani na ni chama kilichosajiliwa wapi na nani?

Maana hili Chama kichaguliwe lazima kiuze sera zake kwa wananchi,wananchi waulizeni Ilani na sera za UKAWA ni zipi maana hakuna chama kilichosajiliwa kinaitwa UKAWA?

CCM ukawa wasitutishe ,hawana wameishakwisha mapema na ninawaakikishia UKAWA mtashindwa vibaya katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

Eti Mbunge wa Iringa Mjini (Peter Msigwa), anasema CCM ya CCM ni hatari kwa usalama wa Taifa kwasababu Hazina hailipi madeni ya makandarasi na serikali ina madeni makubwa sana .

Kwanza amenishangaza sana huyu Msigwa,anajifanya kushangaa madeni inayodaiwa serikali lakini anashindwa kujishangaa kwanza yeye binafsi maana na yeye ana madeni alikopa hapa bungeni.

Mbona hashangai madeni tunayodaiwa sisi wabunge humu ndani maana kuna wabunge humu ndani tulikopa mikopo zaidi ya Sh.Milioni 200"
 
Uyu Lusinde ni debe tupu nakumbuka wakati wa Escraw alijaribu kuwatetea wezi wa Escraw na kumpakazia Zitto lakin alionekana kama punguani tu Watu wamejiuzulu wengine wameuzulishwa na rais, Its shame kwa Lusinde!
 
Sijaona hoja ya maana aliyochangia kwa faida ya wananchi wake wa mtera zaidi ya vijembe.
 
Kamanda jifunze kusoma vitu usivyovipenda huyu Lusinde mlikuwa naye bega kwa bega alivyokuwa anamponda Zitto kwenye issue ya Escrow kuliko leo tena amekuchefua vumilia.

Ukawa wanaposema CCM imechoka wanakuja na data kutoka ndani ya report za CCM lakin akipanda ccm anakuja na chuki kumchukia mtu kutokana na umri eti slaa kachoka kwa sabab ni mzee, this is what? Ivi huyu Lusinde hakumbukii uongoz wa Mandela S.Africa??
 
maneno KUNTU

Ukawa wanaposema CCM imechoka wanakuja na data kutoka ndani ya report za CCM lakin akipanda ccm anakuja na chuki kumchukia mtu kutokana na umri eti slaa kachoka kwa sabab ni mzee, this is what? Ivi huyu Lusinde hakumbukii uongoz wa Mandela S.Africa??
 
Back
Top Bottom