Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,943
Lusekelo!! Sawa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Nina wazo Jamaa ni Mzuri,Ila Katiba Ni Msahafu,Kwani Akitokata Kwa Mujibu wa Katiba hata Kama Hajamaliza Miradi kwani Serikali si IPO?Ili tupae kiuchumi Anahitaji Aongoze Miaka 20 ili amalizie miradi yake yote, kama ninavompinga jpm na ninapompongeza tuungane mkono makamanda.
Gesi tuliambiwa na CCM itamaliza tatizo la umeme, kwa sasa sio gesi tena ni majiNchi inazalisha megawat 1500 na uhitaji ni megawat 2500 kwa makadilio na ST gorge inazalisha megawat 2000 jumla ikishaunganishwa na grid ya taifa nchi itazalisha megawat 3500 hivi sasa usichokijua ni kipi ?
Wabongo munavituko! GT thinker yeyote lazima asimkilize yeyote ata chizi kazi inaaki kwake kuchambua tu! Hivi unafikiri Zitto hajamsikiliza? unafikiri Lissu hajamsikiliza leo?Only fools can waste time listerning .......
Vipi tena kuna ubaya ? mbona unamshanga Lusekelo?Lusekelo!! Sawa.
Hii miradi bila kujipanga matokeo yake ndio haya sasa tunakamuliwa kodi kwenywe kila kitu.
Miradi hii mpaka ikamilike, wabongo mtakuwa hohehahe huku uchumi ukiwa taabani(mtakuwa kama waethiopia)
Msisahau zoezi la kujenga mji wa kiserikali Dodoma nalo linaendelea.
Serikali imejitwika mzigo isio na uwezo nao japo baadhi ya hiyo miradi michache ni muhimu ila utekelezaji wake na gharama zake ni lazima tutuumie tena sio kidogo na hata uchumi unaweza kuyumb maana baadhi ya miradi inapeleka fedha nyingi nje ya nchi..
Hauwezi kujenga nchi kwa kuongeza expenditure,kukopa kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo mapato ya nchi yanaporomoka/biashara nyingi zinafungwa.
Chagueni miradi michache na muitekeleze kwa awamu kulingana na uchumi wetu na kwa kuzingatia pato halisi la Taifa letu.
Kamati ya Bunge ya Bajeti yahofia makusanyo yote ya serikali kutumika kuhudumia deni la Taifa, yataka kuwe na ukomo wa kukopa - JamiiForums
Serikali hii ina majukumu mengi zaidi ya
kujenga miundombinu na hazina yetu ni hiyo hiyo moja na ili tusonge mbele, ni lazima tutoe kipaumbele na kwa sekta nyingine maana zinategemeana.
Ni swala la muda tu itawabidi mbuni kodi za ajabu ajabu ili kujaribu kujikwamua.
Kwa sasa wengine hatutaeleweka kama ilivyo kawaida ila muda ndio kila kitu.
Vipi tena kuna ubaya ? mbona unamshanga Lusekelo?
Munakumbuka mulituambia Ndege zile injini zake kimeo zimeshika moto ndiyo maana zinaishia kumwagiwa maji?Ninauhakika hiyo sijui stilaz goji itaishia kuwa kimeo kama boing
Mimi kinachonisumbu ni uwongo, hili bwawa ni kubwa kuliko lile la ethiopia, ambalo limeamza kujengwa 2014 na mpaka leo ni 60% done na litachukua miaka minane kulijaza, leo naambiwa bwawa kubwa zaidi litajengwa kwa miezi 36 na kujaa miezi sita huu uwongo utaisha lini?View attachment 965593View attachment 965589
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake, Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, wanashiriki utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Rufiji (Stieglers Gorge).
Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na Makamu wa a Rais, Mama Samia; Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai; Mawaziri; Jaji Mkuu na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Ulinzi ha Usalama, pamoja na Viongozi wa Dini.
Kulingana na vyanzo, Mradi huo utagharimu US $ 3.6 Billion (zaidi ya Tsh. Trilioni 8).
Waziri wa Nishati - Medard Kalemani:
Waziri amesema kuwa, urafiti uliofanyika tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere miaka ya 1970s, ulipanga kuutekeleza Mradi wa Stieglers Gorge katika Awamu tatu:
Hata hivyo, kutokana na gharama kubwa za Mradi kwa wakati huo, pamoja na na mahitaji kidogo ya umeme nchini kwa wakati huo yaliyokuwa MW 100 pekee, yalipelekea kuahirishwa utekelezaji wa Mradi huo.
- Awamu ya I - MW 400;
- Awamu ya II - MW 800 na
- Awamu ya II - MW 900
Kwa sasa mahitaji yamekuwa na kubwa nchini, hivyo Mradi urajengwa wote kwa pamoja kuzalisha MW 2,100 na ujenzi wake utakuwa katika stages nne:
Eneo la Mradi ni km za mraba 914 sawa na 1% ya km za mraba 50,000 za Selous Game areserve. Eneo la Mtambo ni km za mraba 36 sawa na asilimia 0.007 ya Mbuga ya Selous.
- Kujenga ukuta.
- Kujenga tuta lenye uwezo wa kutunza mita za ujazo bilioni 35.2
- Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wenye mashine (turbines) 9.
- Kujenga sub-stations za kufua umeme wa KV 400.
Hili ni Bwawa kubwa la 60 duniani na la nne barani Afrika, likizidiwa tu na na mabwawa yaliyoko Ethiopia (2) na moja la Nigeria huku Grand Renaissance (zaidi ya MW 6,000) linaloendelea kujengwa Ethiopia likiwa ndiko kubwa zaidi.
Tayari Misri kupitia Kampuni iliyoshinda tenda ya Arab Contractors inatiliana saini na Tanzania kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Nani Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amelifananisha Bwawa la Stieglers Gorge na lile la Aswani nchini Misri, lililojengwa miaka ya 1970s na ambalo lilibadilisha kwa kiwango kikubwa uchumi wa a Nchi hiyo.
Spika wa Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai ameunga mkono Mradi huo na kudai kuwa, ana uzoefu mkubwa na eneo hilo kwa kuwa aliwahi kufanya kazi katika Mbuga ya Selous. Alihoji wanaopinga Mradi huo kwa kigezo cha mazingira na kueleza kuwa, kutunza rasilimali kama hiyo kwa ajili ya kutunza mazingira tu na utalii haitakuwa sawa.
Rais Dk. John Pombe Magufuli:
Rais amemkaribisha PM wa Misri na kumwambia kuwa hapa ni kwao. Amesema Nchi hizi zina uhusiano wa muda mrefu tangu zamani kabla ya kuja kwa wakoloni. Alisema hata muziki wa Taarabu unaotamba hapa Tanzania ulianzia huko Misri.
Alisema kupitia Rais Julius Nyerere na Abdul Gamal Nasser wa Misri walishirikiana katika kuziletea Nchi hizi maendeleo.
Alisema anajisikia furaha sana kushiriki uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa umeme wa Stieglers Gorge. Alisema hiyo ni ndoto ya muda mrefu tangu miaka ya 1970s baada ya utafiti kufanywa na Wanorway.
Mradi huo unaotekelezwa na Arab Contractors una thamani ya US $ 2.9 Billion. Trilioni 6.5
Magufuli amesema Yesu alipotaka kuuawa alikimbilia Misri, hivyo na wao wanakimbilia Misri ili isaidie katika kujenga Mradi wa umeme.
Amewapongeza a Watanzania kwa kufikia hatua hii iliyosubiriwa kwa miaka 40.
Amewapongeza pia Arab Contractors kwa kushinda tenda hiyo.
Rais Magufuli amesema, Tanzania ina vyanzo vingi vya umeme lakini sababu ya kuamua kutumia umeme wa HEP, ni:
- Uhakika
- Gharama za utekekezaji
- Gharama za uwekezaji na
- Tija kwenye uchumi
Chanzo cha umeme wa nguvu za maji ni cha uhakika. Mradi huu utazalisha umeme kwa muda wa miaka 60 ijayo.
Gharama za mradi wa maji ni ndogo kulinganisha na vyanzo vingine:
- Umeme wa nguvu za Maji - Tsh. 36 kwa unit
- Upepo - Tsh 103 kwa unit
- Umeme wa ardhi - Tsh. 118 kwa unit
- Umeme wa gesi - Tsh. 147 kwa unit
- Umeme wa mafuta -Tsh. 426 kwa unit.
Umeme uliopo Tanzania Kwa sasa ni, MW 1,560 pekee.
Mradi uradhusha bei na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi.
Mradi huu utasaidia kutunza mazingira. Eneo la mradi ni asilimia 1% ya eneo la Selous.
Rais amesema Watanzania ni wahifadhi wakubwa wa mazingira kwani zaidi ya asilimia 32% ni eneo la hifadhi. Amesema kwa sasa, matumizi ya mkaa nchini ni makubwa yanayopelekea kukatwa miti ukubwa wa hekta zaidi ya 200,000. Kasi ya ukataji miti kwa sasa ni kubwa na kwamba inaweza kukata miti yote ndani ya Selous ndani ya miaka 23.
Rais amesema Serikali inataka kupunguza gharama za umeme kwani bado ni kubwa mno kulinganisha na Nchi nyingine. Alitolea mfano wa gharama za kulipia umeme kwa Nchi nyingine kama ifuatavyo:
Rais amesema kuwa, Mradi huo ukikamilika utasaidia viwanda kupata umeme wa bei nafuu, hali itakayosaidia unafuu wa bei na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa za viwandani na kuzifanya bidhaa za Tanzania kuwa competitive kimataifa.
- Egypt - Dola senti 4.6
- Korea Kusini - Dola senti 8
- China - senti 8
- South Africa - senti 7.4
- India - senti 6.8
- Uingereza - senti 1.5 na
- Marekani - senti 0.2.
Rais amesema Watanzania wana upendo mkubwa kwa Wamisri na ndiyo maana Tanzania haikutaka kujenga umeme kwenye Mto Kagera ili kutopunguza maji yanayotiririka kwenda nchini Misri kupitia Mto Naili.
Rais amesema Mradi huu utajengwa kwa muda wa miaka miwili na nusu.
Rais Magufuli amewaasa Watanzania kujifunza kutoka kwa Wamisri ili na wao waache legacy nchini ya kulibadilisha Taifa hili. Kila mmoja akafanye jitihada katika kubadilisha hali iliyopo kwa sasa.
View attachment 965510
View attachment 965526
View attachment 965541
Bonde mwanana la Mto Rufiji. A romantic River majestically standing and boasting the pride of Tanzanians.
Al-Sisi accepts Magufuli’s invitation to put cornerstone of Tanzania’s largest dam - Daily News Egypt
Kampuni ya Misri kupata tenda ya Mradi wa Umeme wa Stieglers Gorge: Rais wa Misri, Al Sisi kuja Tanzania kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi. - JamiiForums
Yaelekea nawe ni mzee wa 'vibapa'Lusekelo!! Hapana nashangaa kwa kuwa nampenda sana yule mzee.
Namheshimu.
Hapana, Lusekelo namheshimu sana.Yaelekea nawe ni mzee wa 'vibapa'
Tatizo atakaa na kiu maana kinywaji chake hakiwezi kuwepo pale.Vipi tena kuna ubaya ? mbona unamshanga Lusekelo?
mh Membe tena?Kama ni umaarufu kidini wa kuitiwa Ikulu basi angewaita hata na Shehe Ponda na Kakobe. Ameanza kuwabembeleza wanao mpinga? Au ni kwa vile ndani ya nyumba #Membe kapiga chafya yeye makamasi yana churuzika?
Membe angalia utaua watu kwa kihoro!