View attachment 965593View attachment 965589
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake, Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, wanashiriki utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Rufiji (Stieglers Gorge).
Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na Makamu wa a Rais, Mama Samia; Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai; Mawaziri; Jaji Mkuu na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Ulinzi ha Usalama, pamoja na Viongozi wa Dini.
Kulingana na vyanzo, Mradi huo utagharimu US $ 3.6 Billion (zaidi ya Tsh. Trilioni 8).
Waziri wa Nishati - Medard Kalemani:
Waziri amesema kuwa, urafiti uliofanyika tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere miaka ya 1970s, ulipanga kuutekeleza Mradi wa Stieglers Gorge katika Awamu tatu:
- Awamu ya I - MW 400;
- Awamu ya II - MW 800 na
- Awamu ya II - MW 900
Hata hivyo, kutokana na gharama kubwa za Mradi kwa wakati huo, pamoja na na mahitaji kidogo ya umeme nchini kwa wakati huo yaliyokuwa MW 100 pekee, yalipelekea kuahirishwa utekelezaji wa Mradi huo.
Kwa sasa mahitaji yamekuwa na kubwa nchini, hivyo Mradi urajengwa wote kwa pamoja kuzalisha MW 2,100 na ujenzi wake utakuwa katika stages nne:
- Kujenga ukuta.
- Kujenga tuta lenye uwezo wa kutunza mita za ujazo bilioni 35.2
- Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wenye mashine (turbines) 9.
- Kujenga sub-stations za kufua umeme wa KV 400.
Eneo la Mradi ni km za mraba 914 sawa na 1% ya km za mraba 50,000 za Selous Game areserve. Eneo la Mtambo ni km za mraba 36 sawa na asilimia 0.007 ya Mbuga ya Selous.
Hili ni Bwawa kubwa la 60 duniani na la nne barani Afrika, likizidiwa tu na na mabwawa yaliyoko Ethiopia (2) na moja la Nigeria huku Grand Renaissance (zaidi ya MW 6,000) linaloendelea kujengwa Ethiopia likiwa ndiko kubwa zaidi.
Tayari Misri kupitia Kampuni iliyoshinda tenda ya Arab Contractors inatiliana saini na Tanzania kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Nani Mkuu wa Tanzania,
Profesa Ibrahim Juma amelifananisha Bwawa la Stieglers Gorge na lile la Aswani nchini Misri, lililojengwa miaka ya 1970s na ambalo lilibadilisha kwa kiwango kikubwa uchumi wa a Nchi hiyo.
Spika wa Jamhuri ya Muungano,
Job Ndugai ameunga mkono Mradi huo na kudai kuwa, ana uzoefu mkubwa na eneo hilo kwa kuwa aliwahi kufanya kazi katika Mbuga ya Selous. Alihoji wanaopinga Mradi huo kwa kigezo cha mazingira na kueleza kuwa, kutunza rasilimali kama hiyo kwa ajili ya kutunza mazingira tu na utalii haitakuwa sawa.
Rais Dk. John Pombe Magufuli:
Rais amemkaribisha PM wa Misri na kumwambia kuwa hapa ni kwao. Amesema Nchi hizi zina uhusiano wa muda mrefu tangu zamani kabla ya kuja kwa wakoloni. Alisema hata muziki wa Taarabu unaotamba hapa Tanzania ulianzia huko Misri.
Alisema kupitia Rais Julius Nyerere na Abdul Gamal Nasser wa Misri walishirikiana katika kuziletea Nchi hizi maendeleo.
Alisema anajisikia furaha sana kushiriki uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa umeme wa Stieglers Gorge. Alisema hiyo ni ndoto ya muda mrefu tangu miaka ya 1970s baada ya utafiti kufanywa na Wanorway.
Mradi huo unaotekelezwa na Arab Contractors una thamani ya US $ 2.9 Billion. Trilioni 6.5
Magufuli amesema Yesu alipotaka kuuawa alikimbilia Misri, hivyo na wao wanakimbilia Misri ili isaidie katika kujenga Mradi wa umeme.
Amewapongeza a Watanzania kwa kufikia hatua hii iliyosubiriwa kwa miaka 40.
Amewapongeza pia Arab Contractors kwa kushinda tenda hiyo.
Rais Magufuli amesema, Tanzania ina vyanzo vingi vya umeme lakini sababu ya kuamua kutumia umeme wa HEP, ni:
- Uhakika
- Gharama za utekekezaji
- Gharama za uwekezaji na
- Tija kwenye uchumi
Chanzo cha umeme wa nguvu za maji ni cha uhakika. Mradi huu utazalisha umeme kwa muda wa miaka 60 ijayo.
Gharama za mradi wa maji ni ndogo kulinganisha na vyanzo vingine:
- Umeme wa nguvu za Maji - Tsh. 36 kwa unit
- Upepo - Tsh 103 kwa unit
- Umeme wa ardhi - Tsh. 118 kwa unit
- Umeme wa gesi - Tsh. 147 kwa unit
- Umeme wa mafuta -Tsh. 426 kwa unit.
Umeme uliopo Tanzania Kwa sasa ni, MW 1,560 pekee.
Mradi uradhusha bei na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi.
Mradi huu utasaidia kutunza mazingira. Eneo la mradi ni asilimia 1% ya eneo la Selous.
Rais amesema Watanzania ni wahifadhi wakubwa wa mazingira kwani zaidi ya asilimia 32% ni eneo la hifadhi. Amesema kwa sasa, matumizi ya mkaa nchini ni makubwa yanayopelekea kukatwa miti ukubwa wa hekta zaidi ya 200,000. Kasi ya ukataji miti kwa sasa ni kubwa na kwamba inaweza kukata miti yote ndani ya Selous ndani ya miaka 23.
Rais amesema Serikali inataka kupunguza gharama za umeme kwani bado ni kubwa mno kulinganisha na Nchi nyingine. Alitolea mfano wa gharama za kulipia umeme kwa Nchi nyingine kama ifuatavyo:
- Egypt - Dola senti 4.6
- Korea Kusini - Dola senti 8
- China - senti 8
- South Africa - senti 7.4
- India - senti 6.8
- Uingereza - senti 1.5 na
- Marekani - senti 0.2.
Rais amesema kuwa, Mradi huo ukikamilika utasaidia viwanda kupata umeme wa bei nafuu, hali itakayosaidia unafuu wa bei na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa za viwandani na kuzifanya bidhaa za Tanzania kuwa competitive kimataifa.
Rais amesema Watanzania wana upendo mkubwa kwa Wamisri na ndiyo maana Tanzania haikutaka kujenga umeme kwenye Mto Kagera ili kutopunguza maji yanayotiririka kwenda nchini Misri kupitia Mto Naili.
Rais amesema Mradi huu utajengwa kwa muda wa miaka miwili na nusu.
Rais Magufuli amewaasa Watanzania kujifunza kutoka kwa Wamisri ili na wao waache legacy nchini ya kulibadilisha Taifa hili. Kila mmoja akafanye jitihada katika kubadilisha hali iliyopo kwa sasa.
View attachment 965510
View attachment 965526
View attachment 965541
Bonde mwanana la Mto Rufiji. A romantic River majestically standing and boasting the pride of Tanzanians.
Al-Sisi accepts Magufuli’s invitation to put cornerstone of Tanzania’s largest dam - Daily News Egypt
Kampuni ya Misri kupata tenda ya Mradi wa Umeme wa Stieglers Gorge: Rais wa Misri, Al Sisi kuja Tanzania kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi. - JamiiForums