Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, bila Magufuli pale Dodoma kusingekuwa makao makuu ya nchi, Magufuli amepambana Sana Sana kuhakikisha kuwa Leo hii Dodoma imesimama imara kama makao makuu ya nchi.
Magufuli ndiye amelifufua wazo hili ambalo limedumu tangu enzi za mwalimu Nyerere mpaka Jana Ikulu imesimama, sasa je n'nani huyo aliyethubutu kulifanya hili?
Mwalimu Nyerere yeye alileta hili wazo, hakufanya chochote Ila Dodoma jina tu.
Mwinyi ndio kabisa hakufanya lolote. Na wakati huohuo hata Mkapa na Kikwete nao vilevile.
Magufuli yeye amethubutu pakubwa kuhakikisha kuwa Leo hii Dodoma imekuwa kama hivyo, jamani n'nani hakuliona hili? Magufuli amejenga mfano wa Ikulu ya muda huku hii ikijengwa inamaana yeye ndiye alilifufua wazo la mwalimu Nyerere na akalifanyia kazi, Magufuli yeye amefariki huku Ikulu ikijengwa na Rais Samina akashika hatamu.
Kwahiyo Magufuli ana mchango mkubwa Sana Katika ujenzi wa Ikulu hiyo, watu hawaoni wanajifanya macho kuziba.