Walete halisi, na iletwe timu independent ikiwezekana kutoka nje ili umri wa karatasi na wino upimwe. Ikivuka hatua hiyo, tutaingia katika hatua ya kupima hypotheses kadhaa kama vile:
*Hati ya Muungano ilidhamiria mfumo wa shirikisho la serikali tatu.
*Mkataba wa muungano haukumpa madaraka Rais wa Muungano wala Bunge la muungano kutunga sheria za kuifuta Tanganyika.
*Mkataba haukumpa rais mamlaka ya kutoa amri za kugeuza chochote cha Tanganyika kuwa cha muungano.
*Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika (1962) ndio iliyoelekezwa na mkataba wa muungano kuendelea kuwa katiba ya kusimamia masuala ya Tanganyika nje ya yale ya muungano.
*Mkataba wa muungano haukuruhusu chama chochote cha siasa kuingilia masuala ya muungano.
*Rais wa muungano hakupewa madaraka ya zaidi ya mwaka mmoja kusimamia masuala ya Tanganyika.
*Jamhuri mpya huru ilitakiwa iwe imeanza mchakato wa katiba mpya kabla ya tarehe 26 Aprili 1965, na sio kuwa chini ya katiba ya muda kwa miaka 12 (1965-1967).
*Mkataba wa muungano haukusema Tanzania ni nchi moja bali jamhuri moja (jamhuri inaruhusu uwepo wa nchi zaidi ya moja).
*Jamhuri ya muungano ilitambulika rasmi kama nchi moja miaka 20 baada ya muungano (1984), sio siku ya muungano.
*Tanganyika iliendelea kutambulika kwa miaka zaidi ya miwili katika nyaraka muhiu kama katiba ya muda (1965) na mkataba wa muungano (1964), na sio siku ya muungano kama Pinda alivyodai.
*Mkataba wa muungano ulipitishwa kwa 2/3 ya bunge upande wa Tanganyika lakini sio kwa upande wa zanzibar, hivyo muungano kutokodhi sharti la 2/3 la mkataba wa muungano (1964).
Hizi ni baadhi tu ya hypotheses zinazohitaji kupimwa ili kubaini iwapo:
*Muungano uliopo ni muungano halali kisheria.
*Muungano uliopo ni wa nchi mbili huru kwa mujibu wa katiba zao.
Kama the above ni true kote, kinachotakiwa kufanywa ni kura ya maoni kuuliza pande zote iwapo wanataka muungano wa serikali moja, mbili, au tatu. Pande zote za umma lazima zitoe majibu ya ndio 2/3. Idadi hii isipopatikana, kwa mfano upande mmoja tu wa muungano upate na mwingine usipate 2/3, jahazi livunjwe, tugawane mbao, tukutane EAC, SADC au COMESA. Wazanzibari wapewe muda wa mwaka mmoja kufikiria iwapo wanataka uraia wa zanzibar au Tanganyika. Baada ya hapo pande mbili zitakuwa zinaruhusiwa kutembeleana bila viza kwa miezi mitatu au sita.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums