Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Miaka ya 60 karatasi zilizokuwa zinatumika sio za aina hii na hazikuwa nyepesi kama hii wanayosema ndio halisi .....wamebugi......
 
Siamini kama saini ile ni ya Karume, ile saini ni ya kisomi na ya msomi wa hali ya juu kuliko Abeid Amani Karume.

kama mna wasiwasi si mkachuke vingerprinti?
Nendeni mkafukue walio tangulia mbeleza haki mchukue finger print ,ili uzalilishaji uendeleee na laaana zitafune nchi
 
Tanganyika

sasa ubishi uko wapi, basi rudisheni mataifa yaliyoungana Tanganyika na Zanzibar, tunaipenda tanzania ila hati ya muungano inasema zanzibar imeungana na Tanganyika, tufanye tanganyika imekufa, basi zanzibar ndo liwe taifa maana tanganyika imekufa, wanataka kusema kuna muungano wa zanzibar na tanzania au zanzibar na Tanganyika??
 
kama mna wasiwasi si mkachuke vingerprinti?
Nendeni mkafukue walio tangulia mbeleza haki mchukue finger print ,ili uzalilishaji uendeleee na laaana zitafune nchi

Hiyo ni argument dhaifu mkuu. Ndio maana nchini kughushi ni kwingi mno.
Kumbuka kuwa huo ni Mkataba wa pili kuonyeshwa. Hati ya Muungano ya kwanza ilionyeshwa kwa Wabunge kwenye Kamati, ambayo hata Mwenyekiti- Sitta aliigomea na hatimaye akadai kuwa iko UN, baada ya Tundu Lisu juzi kuwashushua, leo hati imeibukia Ikulu! Watuambie basi, ile iliyokywa UN imerudishwa? Unaamini hizi sarakasi wewe?
 
Wabongo balaa tu! Wanahoji Vitu vimefanyika hata wao hawajazaliwa! Mtu mgonvi utamjua hutafuta sababu yoyote tu hata haina maana! Zungurukeni baharini hamkosi kisiwa au bara la Antactic halina mtu mkaanzoshe taifa lenu peke yenu.
 
Sahihi ya JKN iko kwa wino wa blue wakati ya AAK ni kama copy....sio wino wa kalamu
 
Kwa jinsi watanzania Tunavyoshadadia Hizi ngonjera za Hati ya Muungano inazidi kuonesha ni jinsi gani tuna safari ndefu kufikia "self realization", Kama taifa. Hatujui tunaenda wapi, wala tumetoka wapi. Kuna njemba humu hata historia ya nchi yao inawapiga chenga.mbaya zaidi wanapayuka kwa sauti kuu, bila hata kujaribu kuficha up*mbavu wao. huyu Tundu Lisu angekuwamo humu ndani ningemuuliza yeye ni mbunge wa nchi gani? raia wa nchi gani? mwanasheria anaetumikia mahakama halali ya nchi gani? angejibu haya maswali kwa ufasaha, then tungeendelea kujadili hoja zake bila kumuona ch*zi mtozeni flani.
 
Walete halisi, na iletwe timu independent ikiwezekana kutoka nje ili umri wa karatasi na wino upimwe. Ikivuka hatua hiyo, tutaingia katika hatua ya kupima hypotheses kadhaa kama vile:
*Hati ya Muungano ilidhamiria mfumo wa shirikisho la serikali tatu.
*Mkataba wa muungano haukumpa madaraka Rais wa Muungano wala Bunge la muungano kutunga sheria za kuifuta Tanganyika.
*Mkataba haukumpa rais mamlaka ya kutoa amri za kugeuza chochote cha Tanganyika kuwa cha muungano.
*Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika (1962) ndio iliyoelekezwa na mkataba wa muungano kuendelea kuwa katiba ya kusimamia masuala ya Tanganyika nje ya yale ya muungano.
*Mkataba wa muungano haukuruhusu chama chochote cha siasa kuingilia masuala ya muungano.
*Rais wa muungano hakupewa madaraka ya zaidi ya mwaka mmoja kusimamia masuala ya Tanganyika.
*Jamhuri mpya huru ilitakiwa iwe imeanza mchakato wa katiba mpya kabla ya tarehe 26 Aprili 1965, na sio kuwa chini ya katiba ya muda kwa miaka 12 (1965-1967).
*Mkataba wa muungano haukusema Tanzania ni nchi moja bali jamhuri moja (jamhuri inaruhusu uwepo wa nchi zaidi ya moja).
*Jamhuri ya muungano ilitambulika rasmi kama nchi moja miaka 20 baada ya muungano (1984), sio siku ya muungano.
*Tanganyika iliendelea kutambulika kwa miaka zaidi ya miwili katika nyaraka muhiu kama katiba ya muda (1965) na mkataba wa muungano (1964), na sio siku ya muungano kama Pinda alivyodai.
*Mkataba wa muungano ulipitishwa kwa 2/3 ya bunge upande wa Tanganyika lakini sio kwa upande wa zanzibar, hivyo muungano kutokodhi sharti la 2/3 la mkataba wa muungano (1964).

Hizi ni baadhi tu ya hypotheses zinazohitaji kupimwa ili kubaini iwapo:
*Muungano uliopo ni muungano halali kisheria.
*Muungano uliopo ni wa nchi mbili huru kwa mujibu wa katiba zao.

Kama the above ni true kote, kinachotakiwa kufanywa ni kura ya maoni kuuliza pande zote iwapo wanataka muungano wa serikali moja, mbili, au tatu. Pande zote za umma lazima zitoe majibu ya ndio 2/3. Idadi hii isipopatikana, kwa mfano upande mmoja tu wa muungano upate na mwingine usipate 2/3, jahazi livunjwe, tugawane mbao, tukutane EAC, SADC au COMESA. Wazanzibari wapewe muda wa mwaka mmoja kufikiria iwapo wanataka uraia wa zanzibar au Tanganyika. Baada ya hapo pande mbili zitakuwa zinaruhusiwa kutembeleana bila viza kwa miezi mitatu au sita.




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wabongo balaa tu! Wanahoji Vitu vimefanyika hata wao hawajazaliwa! Mtu mgonvi utamjua hutafuta sababu yoyote tu hata haina maana! Zungurukeni baharini hamkosi kisiwa au bara la Antactic halina mtu mkaanzoshe taifa lenu peke yenu.
Ndio nyie wenye hoja kwamba hamuijui Tanganyika kwa sababu asilimia 80 yenu mmezaliwa baada ya muungano. Scotland iliungana na Uingereza miaka 200 iliyopita, na wanajitoa kwenye unitary system ya UK mwakani, je ni asilimia ngapi ya wa-scottish wamezaliwa ndani ya muungano?





Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwani serikali mbili hazigawi vyeo?!
Unaweza kunambia kazi ya Prof. Mwandosya?!
Pili, ni kwa nini unadhani serikali tatu zitakuwa na vyeo vyingi kuliko tatu na vichache kuliko moja?!

Dawa ni serikali moja...kwa sisi wabongo tulivyo hatuheshimu kabisa mambo. Hapa tulipo ujomba ujomba unatugharimu...subiri uone hizo serikali tatu takuwaje...mawaziri 100 in total...bunge lile itabidi liongezwe mara dufu watu wote waenee. Tatizo sio muundo wa serikali...ni nidhamu katika kuendesha mambo yetu kama Taifa kuanzia ngazi ndogo kabisa ambazo zina tuhusu karibu watu wote mpaka juu mana kikulacho ki nguoni mwako na si vinginevyo.
 
Hivi tatizo letu ni muundo wa muungano au kukosa uzalendo na kupiga vita rushwa na matumizi mabaya ya madaraka?

kunalo tatizo la kimsingi ktk muungano uliopo,manake umekaa ktk mfumo wa "changu changu, chako chetu". Cha znz ni chao,lakini cha tanganyika ni cha wote!sijui kwa nn watanganyika hawalioni hili
 
"...swali la pili linalohitaji kuulizwa la msingi kabisa, je hati hii ni halali...??!!" T. Lissu
 
Ndio nyie wenye hoja kwamba hamuijui Tanganyika kwa sababu asilimia 80 yenu mmezaliwa baada ya muungano. Scotland iliungana na Uingereza miaka 200 iliyopita, na wanajitoa kwenye unitary system ya UK mwakani, je ni asilimia ngapi ya wa-scottish wamezaliwa ndani ya muungano?





Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mwanaume anatakiwa awe straight! haina haja ya kupindisha! Lazima kuna kitu mnakitafuta zaidi ya serikali 3! Just go straight hamuutaki muungano kuliko kuhoji hati! Hati ili iwaje?
 
Back
Top Bottom