Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kila ngoz nyeupe ni muhindi mkuu...mama ni mrusi.Sasa mkuu hyo ndo wa kukupa ww street we huoni jinsi alivyo hapo itakuwa kawekwa na wahindi wenzake.
Dah,maisha haya bana.anyway ila ili tuendelee kuheshimiana lazima haya magap yawepo ingawa kibinadamu inaumiza unapoona mtu mliyekua nae level moja kakupiga gap kubwa la maisha.lazima mtu ujitafakari umekosea wapi.Huyo dogo alikuwa chief accountant DHL Tanzania kabla hajaenda vodacom.
Kwa kozi za udbs. Ukibahatika kuingia Big 4 auditing firms na kukaa miaka kazaa tu. Kupata nafasi kubwa kwenye corporates ni rahisi sana.
Unajua CEO wa NMB amemaliza b com yake pale udsm miaka ya 2000s tu na hana mzunguko mrefu wa kufikia U CEO huku hapo hapo NMB kawakuta watu wana miaka kibao kazini. Ila kawaruka yeye kaingia kama CFO baada ya mwaka akapewa U CEO
Wengi waliosoma nae wapo halmashauri wanasema maneno kama yako
Yeah,huyu jamaa mama yake ni mrusi na baba yake mchaga wa marangu huko kama sikosei ingawa nadhani mzee wake anaishi iringa ambako ndiko amewekeza miradi yake ikiwemo moja ya shule maarufu huko iringa.Usikate tamaa.Mimi nimemaliza B.comm 2003 mbona silalamiki?Pambana kuna siku unaweza kuwa Rais wa nchi ukampiga Robin gap! BTW nilisoma na Jamaa anaitwa Max Kimambo way back in 1995.Nadhani atakuwa kaka yake na huyu.Mama yao ni Mrusi.Bila shaka Max na Robin watakuwa ndugu.
Gap alilonipiga ni kubwa mno(simuonei wivu)ila najishangaa mimi mbona kaniacha mbali kiasi hiki?yani mimi bado nawaza TGS D mwenzangu hapo anawaza labda kuwa CEO wa kampuni kubwa ulimwenguni in next few yearsMkuu hapo kimekuumiza cheo au mshahara?
Usiache kupambana lakini ...money won't follow you ukiwa kwa graveHuyo jamaa hapo chini anaitwa Robin Ernest kimambo.ni class mate wangu pale udbs miaka kadhaa iliyopita.
Leo wakati mimi bado nawaza ni lini utumishi watatoa majina ya written interview nikagombanie salary ya TGS D ambayo ni sawa na shillings 710,000/=, huyu class mate wangu kateuliwa na vodacom Tanzania kuwa acting CFO na naamini soon anakua promoted kuwa CFO kamili.kwa haraka haraka mshahara wa CFO wa vodacom ni around 25M.
Yani hapa niko natafakari haya maisha naona kama sisi wengine hayatutendei haki pamoja na kwamba tunapambana sana tu pasipo kuchoka.
Ukiwa na moyo mdogo unaweza kujikuta unajinyonga kwa msongo wa mawazo.
Sio kwa haya magape aisee
View attachment 2295845