Ila haya maisha wakati mwingine yanaweza kukufanya utamani kujiua

Dah,maisha haya bana.anyway ila ili tuendelee kuheshimiana lazima haya magap yawepo ingawa kibinadamu inaumiza unapoona mtu mliyekua nae level moja kakupiga gap kubwa la maisha.lazima mtu ujitafakari umekosea wapi.
 
Yeah,huyu jamaa mama yake ni mrusi na baba yake mchaga wa marangu huko kama sikosei ingawa nadhani mzee wake anaishi iringa ambako ndiko amewekeza miradi yake ikiwemo moja ya shule maarufu huko iringa.
 
Hiyo ni kawaida mbona?
Mwenyewe ninae room mate wangu pale mabibo hostel kala shavu akati me bado navua samaki huku kilombero.binafsi naamini kila mtu ana bahati yake katika maisha
 

Attachments

  • Screenshot_20220719-045158_Opera Mini.jpg
    38.3 KB · Views: 33
ndo ivo mzeiya naye jamaa apo pamoja na mshahara wake bado anawaonea wivu waliio juu yake wapo wanaomkae iyo 25ml kwa wiki tena form four failed
 
Bora hata wewe unamshahara wengine tumejiajiri kwa mtaji mdogo, ya mwisho wa mwezi hatuyajui kama kuna chochote kitapatikana.

Kutofautiana kwa vipato katika maisha ndio huleta maana na umuhimu wa kupambana ili kufikia malengo yako. Kifupi kama una afya na nguvu mshukuru Muumba wako na pambana huku ukiamini utafika unapotaka. Get rich or die trying !
 
Kikubwa nilichoona jamaa huna shukrani na ni mtu mwenye roho ya husda yaani unaumia mtu akipata...
Kiufupi humu wengi tunatamani tupate hata hiyo laki mbili kwa mwezi lkn hatupati kabisa .. sasa wewe unaipata hiyo fursa unamkufuru mungu kweli??
 
Mshukuru Mungu Kwa Kila jambo,inaumiza sana ila hatuna budi kushukuru Kwa Kila jambo
 
Pole mkuu Ila ni kawaida saana, mimi kuna watu wengi saana nilisoma nao, na wengi tu wamenipiga gap Ila nashukuru mungu kwa kipato kidogo nilichojaaliwa na Hao watu sijawachukia Ila nimewaweka kama back up na connection, mfano nimesoma na Humprey Polepole na Nusrat Hanje ambae sasa ni mbungee wa Tanzania pia mdogo wangu tumbo moja sasa anapokea mshahara Mara tatu ya ninaopokea mimi wakati nimempita umri zaidi ya miaka 4. Kwa Hiyo ni kumshukuru mungu kisha kuendelea kupa mbona na kutokata Tamaa na kuwa tumia Hao watu kama daraja au connection na loop ya kutokea unapokwama mahali
 
Kwenye maisha kwa sasa tunapambana na vingi sana. Kwanza hali zetu wenyewe, pili ni afya ya akili juu ya vitu kama kuchanganywa na mafanikio ya wengine(hili lipo kabisa). Lakini mi naamini kama mtu ukiweza kuiweka akili yako sawa ikawa haitingishwi na mafanikio ya wengine, utaishi vizuri sana mana hali zetu pekeake sio kitu kigumu sana
 
Usiache kupambana lakini ...money won't follow you ukiwa kwa grave
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…