Ila hizi simu zinachangia sana kuvuruga mahusiano

Wangu alijaribu kuikagua simu yangu haina usiku wa manane nimelala, siku ya kwanza nilimuona nikatulia nikijua labda anashangaa shangaa kwenye gallery.

Siku ya pili nikamuona yupo kwenye App ya Message baadae akahamia WhatsApp sikutaka kumkataza nikatulia kimya Kama nimesinzia.

Haikuchukua hata lisaa nikaona ameitupa na kilio juu.
 
Ndiyo maana mwanamke hatakiwi kushika simu ya mume. Ikitokea akahitaji basi afanye kile tu anachotaka sio kuleta ujuaji.

Mnaishi vizuri tu akute sms za washkaji wanakwambia manzi ako sijui amechukua tv utaenda kulipa
Me najisahau nafuta Convo za mademu naacha convo za washkaji mnaongelea demu flani. Dah
 
Me wa kwangu kana Getto kanifuma na manzi maana aliskia sauti akiwa kwa nnje..kaomba nifungue mlango nikagoma alivyoondoka nikamwambia ni mdada wa usafi..
Alafu nikammind kwanini anakuja bila taarifa kama sio ukorofi
 
Kuna Mwenzako huku nikimuomba simu ananiuliza naingia wapi kisha ana pin kama ni tiktok basi utaganda hapohapo
Huwezi kuhama apps

Oya nyie majambazi jifunzeni utulivu
 
Simu huwa zinawasha kuchungulia mkuu

Mimi kama mimi huwa nikipata chance ya kuishika lazima niwashwe niikague ila nitakayoyakuta sitoyauliza kwa wakati ule nakusubirii uje ushike yangu mashetani lazima yapande
 
Kuna sisi simu zetu wanabaki nazo nyumbani tangu saa10 asbh hadi saa1 usiku anayo lakini ILANI amepewa kuwa weee angalia utakachokuta kubaliana nacho.Maswali maswali kuhusu simu yangu hayana nafasi.Password anazijua na sina hofu kabisa
 
Mimi najaribu sana kufanya usafi ila huwa ikitokea wife aombe simu yangu mapigo ya moyo yanakwenda kasi kwani wakati anayo kinaweza kuingia kirusi kikaharibu hali ya hewa hivyo nikifika home namba za watu wangu nazipiga tofali kwa tahadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…