Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Ulikutana na matapeli, hapo hakuna sista wala mdogo wake.
 
Pole sana aisee.
Cha msingi jipe muda utakaa sawa tu na ujifunze.

Mimi kuna limoja tena nalifahamu kabisaaa lilinitapeli likafanya niishi maisha magumu sana na familia LAKINI sasa ni zamu yake dunia inamnyoosha linaishi maisha ya ovyo sana.

Matapeli wote mlaaniwe.
 
Mkuu kwanini hukumshitaki ulivyomfaham?
 
Kati ya banki ambazo ukienda unatakiwa uwe makini basi ni NMB. Matapeli wengi wanajichanganya ndani ya bank na wengine wanakuwa nje. Kuna dada mmoja mwaka Jana alitapeliwa mil 15 ndan ya bank. Wakat yupo ndan ya bank alifuatwa na mtu ambae hamjui ila wakajikuta wanaongea kama vile wanafahamiana.
Akili ilipokuja kuka sawa yule dada anajikuta hana hela amebaki na fomu ya kudeposit, ndo anakumbuka kumbe wakati wanaongea alimkabidhi yule jamaa hela yote.
 
Pole sana na kuibiwa. Mwenyezi Mungu atawalipa hao wezi na wewe atakufariji kwa namna usiyoijua.

Ya laiti ungesema kuwa aliyokutapeli ni mtu aliyevaa kanzu na mwanamke kavaa babui na gari lao limeandikwa maneno ya kiarabu ... basi humu watu wala wasingejadili kuhusu utapeli au kuibiwa bali wangejadili uislamu na kusema waislamu ni wachawi au washirikina.

Lakini kwa sababu wahusika wametoka kanisani na gari lao la St Joseph na mavazi ya mwanamke ni ya sista basi watu wanajadili kuhusu kutapeliwa kwako na wala hawajadili kabisa kuhusu ukristo wao au kanisa.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mimi niliwahi kuwa Wakala wa pesa yaani mpaka nilichoka kila siku wanakuja na mbinu mpya nikistuka hii kesho wanakuja na hii mpaka walifanikiwa kunipiga 1million
Kwenye wakala nilikuwa smart lkn siku nakuta short ya 274,000 niliumwa kichwa vibaya mno.,,.....


Yaani wakala kwa ufupi wanalizwa.... Jamaa mmoja akatuma laki tisa + simu ya wakala na siku hiyo hiyo akaacha kazi..... Ni tandale huko.....

Mitaa iliyonilea
 
Mitaa yangu kabisa hiyo.

Kuna classmate wangu walimtapeli kwa style hiyo kule Peramiho. Kuna madawa wanatumia kukupumbaza.

Usiruhusu kuongea sana na sura ngeni mabarabarani humu. Mambo ni mengi.
 
Mkuu kwanini hukumshitaki ulivyomfaham?
Ni mtu ambaye tulikuwa tunafanya nae biashara afu tukawa na ukaribu hadi katika familia, polisi niliona nitapoteza muda na pesa.

Nilishauriwa nikamsuribishe kwa mtaalamu, na kwa hasira nilizokuwa nazo ilikuwa ni rahisi sana kwenda sema huwa siamini katika revenge, MUDA ni mwalimu kuliko yote aisee nilimuacha kama alivyo, nikajifunza kupitia upumbavu wangu maisha yakaendelea.
 
Nilizani mjanja kumbe bhana πŸ˜…πŸ˜…
 
Shangazi yangu akiwa njiani hasa maeneo ya Kariakoo akiitwa na mtu asiyemjua huwa anamwambia BWANA YESU ASIFIWE KAKA MUNGU ANAKUPENDA SANA 🀣🀣🀣
 
Jaribu kufanya hivi inaweza kukusaidia kiasi chake.

Hapo ulipoibiwa ni Songea mjini, sasa hapo mbele ya hiyo bank ya Nmb kuna jengo la watawa wa mission ya Abasia Hanga monastery kabla hujafika mbele Nbc bank na jengo lao linatazamana na soko kuu, nafikiri wewe ndo umetapeliwa maeneo hayo. Kuna sister mmoja wa mission ya chipole ana sifa hizo za kitapeli alishawahi kumtapeli dogo mmoja wa Mpesa laki 4, issue nzima ilikuwa hivi:

Hawa watawa wana kawaida ya kutembeleana maana wapo wa mashirika mengi, mfano wa benedictine Ndanda wakawatembelea wachipole, wa peramiho wakaenda Bukoba... Kama hivyo.

Sasa huyo sister alitoka akaenda Hanga monastery, alivyofika akawa ana survey mitaa ya kijijini.... Akafika Mpesa flani kwa huyo dogo akamwambia amuwekee hela kwenye cm ndo hiyo 400k. Dogo kamaliza kuweka anamuomba hela....sister anajifanya kutafuta kwenye mkoba mara anamwambia nimesahau utawani ngoja nikachukue, sasa sijui mavazi yalimchanganya akamuamini ndo ikawa imeenda kihivyo. Dogo kwenda utawani anaambiwa mbona hapa wanakuja na kuondoka masister wengi! Huyo tutamjuaje? Basi ikabidi aondoke tu.

NIMETOA HIKO KISA ILI WATU WAJUE KUNA BAADHI YA WATUMISHI WA MUNGU SIO WA KWELI.


Nirudi sasa kumshauri mtoa mada, ila ikiwa bado hujasamehe laki 6 yako.

1. Ukiweza nenda kwenye hilo jengo la watawa ukifika ingia lile duka la vitabu halafu jitambulishe halafu useme hiyo siku ulipita ulikuwa unawahi bank ila kuna gari uliliona limepack hapo kulikuwa na Sr ndani yake limeandikwa sijui st Joseph nini vile... Sasa ulivyotoka bank hukulikuta, kwahiyo lengo la kuja hapo ni kuulizia pengine wanalijua labda la shule kati ya primary au secondary kwa sababu mpaka sasa bado unatafuta shule kwaajili ya kijana wako, hivyo ulivyoliona hilo gari (kama unakumbuka rangi na model yake litaje) ukahamasika kutaka kupata taarifa zake ni la shule gani.

Kama akikuuliza sasa imekuwaje umekuja kuulizia hapa? Simple mjibu nimekuja hapa sababu ni kwa wa mission halafu nilivyomuona yule sister nikajua haya mashirika huwa yanafahamiana kwahiyo naweza nikapata pa kuanzia ili nipate shule bora kwa kijana wangu. HEBU JARIBU HII UNAWEZA KUPATA PA KUANZIA KUMPATA MWIZI WAKO, (kibongo bongo jiwe 6 si mchezo!)



2. Nenda kwenye ma bank yote na Mpesa hizi kubwa kubwa, wale huwa wanabandika sehemu maalumu majina ya shule nyingi tu na taasisi mbali mbali kama za dini kwaajili ya michango mbali mbali. Hapo we chukua majina ya st. Joseph yote! Yawe ya shule au taasisi then ingia Google ingia jina moja baada ya lingine, zaidi we deal na images tu... Huwezi jua pengine unaweza kuliona gari linalofanana na hao matapeli ukaenda sehemu husika ukajikuta unakaribishwa na wezi wako πŸ˜‚πŸ˜. (japo hii njia hai make sense kivile ila siku ukiyatimba! Kila njia utaona inafaa kujaribu).


Nb: hiyo hela ni nyingi jamani! Kwahiyo mpango mkakati ni muhimu. Ila kama mtoa mada umeamua kusamehe basi achana nazo, maana process zote hizo zina consume time!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…