Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Hapana hata sio mtu wa dini, sema tu by nature nipo hivyo pia maisha yanatufundisha. Ila upande wa pili pia niko brutal sana pia, huwa sitabirikagi.
Anha sawa,.
Hongera lakin
 
Usikupate tu mkuu, maana kwa jinsi wanaongea na wewe huwezi kujua hata kama wanakutapeli akili sijui ilikuwa wapi maskini
Yaani mimi akili ingenijia tu 😅😅😅. Sista wa kanisa katoliki hawezi kukosa msaada kwenye kituo chake hadi aombe msaada kwa wapita njia.
Labda ingekuwa nje ya mji huko mahali ambapo hakuna mawasiliano.
Mimi nikisemeshwa tu na mtu nisiye mjua akili inaniambia hapo hapo tapeli huyu.
 
Siamini katika kuibiwa kwa njia ya uchawi
 
Wakala unaweza ukawa na mtaji na ukafilisika chapu
 
Anha sawa,.
Hongera lakin
Ushauri wangu; hao waliokutapeli uwezekano wa kuwapata ni mdogo sana ila amini kabisa hawana mwisho mzuri, wame win kuchukua pesa zako angalia wasi win focus yako. Maana tayari naona umeshaanza jikatia tamaa kuwa mwaka huu wote ni mbaya kwako.

Tumia hasira ulizonazo kupambana na kuzizalisha pesa nyingi zaidi ya hizo, chukulia kama funzo.

“MATAPELI WOTE WALAANIWE”
 
Wakala unaweza ukawa na mtaji na ukafilisika chapu
Nakumbuka alikuja dada mmoja alikuwa mteja tuu....

Kumbe bhn..... wale wazee wa umepokea laki tatu Salio lako ni laki tatu na nusu!!

Ikaingia mesejii hiyo kwa bidada yule,, ghafla wakampandia hewani....

Wazee: Kuna hela imeingia hapo nenda kwa wakala uitoe afu umwambie atutumie....

Dada: haya

Kaja mpaka kwenye kibanda changu.... Kaka niekee laki mbili na tisini....

Nikamwambia okay maake namjua Haina ttzo, nimeeka ghafla kapigiwa mpe wakala tuongee nao

Mimi Tena; Kuna nn

Wazee;:: huna nyongeza, utuongezee maake mgonjwa anahitaji kupatiwa matibabu..... wanakaza nikashtuka nikamuuliza yule dada kina nani Hawa?

Dada;;;;; hata siwajui

Aaaah kubbke nilivurugwa namuuliza haya nipe cash ananiambia ipo kwenye simu shika utoe.......

Kutoa mia tatu hamna Salio,

Maadam alinipa password nikachek Salio ana mia tatu sijui.....

Mimi!!! Mbn huna Salio ?

Dada:::: hamna Salio mbona naambiwa wametuma laki naa

Nikamwambia ushapigwa.... ko tunafanya nn ?

Nikampandia sister hewani kaja fasta.... Yule dada kaomba waende serikali za mitaa wakaandikishane na mumewe akirudi badae walipe kidogo kidogo......

Basii ikawa hivyo!!

Lkn wakala acheni unaweza rudi nyumbn huna mtaji tena
 
pole sana. Ni kweli matapeli wanatumia nguvu za giza maana hata kazi yao ni ya kishetan so lazima wapate sapoti ya ibilis. Imeandikwa mwenye haki huanguka mara 7 akainuka tena. Jipe moyo uwe hodari tukio hilo likawe sababu ya wewe kusimama na kufanikiwa kiuchumi katika mwaka huu 2025. Wamechukua pesa hawajachukua uhai utafanikiwa tu.
 
Ameen🙏
 
Wakala unaweza ukawa na mtaji na ukafilisika c

Ndugu yangu amefunga ofisi yake ya uwakala sababu ya ujinga km huu. Waliaza kumpiga mfanyakaz kama laki 6, akaona isiwe tabu akaka mwenyewe ofisini. Siku amekaa ofisini jion anafunga hesabu anakuta mil 1 haipo.
 
 
Nilitapeliwa pesa alf 60 na simu mwaka 2012 na mwamba aliyesema anataka niwe namtafutia coins za zamani baadae sikuelewa kinachoendelea nikajikuta nafanya kila anachonielekeza mwishoni akili inakuja kuzinduka simu sina na pesa vumbi nadhani alinitafunia kadawa ka ushawishi na ningekua na hela zingine zingeenda
 
Hujapumbazwa amini kwamba kuna jinsi ambavyo walikuingiza tamaa tu kwamba utanufaika kwa kiasi fulani ila huwezi kusema maana hapo ndo mwanzo wa kujionesha kwamba tamaa ilikuponza.

Sheria ya kwanza ya kuepuka kutapeliwa ni kuzuia tamaa isiponze kichwa.

“When the deal is too good, think twice”
 
Hapana mkuu, Ni sister kabisa ana kilemba na msalaba jamani
Sikatai kabisa mkuu, ila kuna namna hapo.

1. Kwa nini walilijua jina lako ( kwamba hao ma-sister) huwa ni wateja wako kwenye biashara yako ??
2. Ilikuwaje ukakubali kutoa hela yako bila wewe kujua nini unafanya.. ( hicho ni Kiini macho... ✍️ )

Hapo tunakubali kabisa kila kitu ulicho kiona pale kwenye tukio kilikuwa kitu siyo halisi..

Na ukienda mbali zaidi huu mchezo walikuwa wanakufuatilia pindi unaenda bank..( au walinusa tu kulingana na mbinu zao)
 
Pole mkuu.. na haya maumivu yatapita tu, songa mbele utapata pesa nyingi zaidi.

Ila kiukweli matapeli/ wezi wanaudhi sana ndo mana wakidakwa wanachomwagwa moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…