Ila ndoto nyingine zinachosha, ndoto niliyoiota usiku wa kuamkia leo imenitisha.

Ila ndoto nyingine zinachosha, ndoto niliyoiota usiku wa kuamkia leo imenitisha.

Alafu kuna hili tatizo la ukikutana na demu kwenye ndoto ukimuomba namba ya simu ukiwa unaandika namba zinakataa kuingia kwenye simu ukibonyeza 7 inajiandika 9 unafuta futa hadi unashtuka usingizini hivi hii hali wenzangu mlishakutana nayo?
Hii kali 7 inakuwa 9
 
Nilipoota mmama mmoja hapa jirani ananirushia mkuki ule mkuki ukalenga kwenye Biblia kisha mkuki ukamrudia yule mmama, Niliamini ulinzi wa Mungu.
 
Mi nikikutana na mademu ndotoni mara nyingi nawaomba namba ila sina tabia hizo kwenye uhalisia kimbembe ni kuwa sijawahi kufanikiwa kukamilisha kuziandika hizo namba
Huwa unajiskiaje baada ya kushindwa hilo?
 
Nilipoota mmama mmoja hapa jirani ananirushia mkuki ule mkuki ukalenga kwenye Biblia kisha mkuki ukamrudia yule mmama, Niliamini ulinzi wa Mungu.
Mungu yupo na anatulinda, watu wakaribu wengi ndio huyafanya haya na hujamkosea kitu.
 
Tukio lililonishangaza nilipoamka na kukuta pete ipo juu ya t-shirt nyepesi niliyokuwa nimeivaa kabla ya kulala ikiwa imekunjwa vizuri na kuwekwa juu ya meza pembeni ya mlango. Hii pete ni zile rozari pete(kwa Waroma nadhani mnaijua vyema) muda mwingi huwa ipo kidoleni huwa naivua nikifua au kuoga na mpaka nalala ilikuwepo.

Nilivoshtuka na kuamka nashangaa mbona leo baridi kali sana, kujicheki nipo kifua wazi nikashtuka maana kumbukumbu zangu nililala na tshirt. Kuamka kuwasha taa ndio nikashuhudia hayo yote ya pete yangu kuwa juu ya tshirt iliyokunjwa vizuri. Na hata iweje siwezi weka nguo juu ya meza kwa namna ile.

Ni nini kimefanyika wakuu? Au ndio nilifanya kwa vitendo nilivyokuwa nafanya ndotoni maana kuna watu wakiota wanafanya kitu ndotoni na kwenye uhalisia wanafanya kweli kwa mfano kukimbia.

Sina historia ya kufanya matukio ndotoni baada ya miaka mingi sana kuota nacheza mpira nikapiga shuti ukutani mpaka vidole vikateguka.

Hili tukio kama utani ila limeniacha hoi, hii hii pete kuna siku niliikuta chini baada ya kuota kuna mtu anaivua. Inashangaza sana.

Sijui ina maana gani na inaashiria nini lakini naona ni ndoto tu.
Ukiona hivo ujue Mungu anakuepisha na Mengi sana
 
Back
Top Bottom