Ila ndoto nyingine zinachosha, ndoto niliyoiota usiku wa kuamkia leo imenitisha.

Naijua mkuu
Ok the issue is easy.
Nunua Chumvi ya 1000 tu kwanza,

Chota chumvi kwa mkono wako ijae kwenye kigonja, loweka kwenye maji size ya nusu ndoo.

wakati unaiweka inenee maneno ya kukemea khs kusahau ndoto, kuota ndoto mbaya, n.k kisha subiri dk kadhaa mpk itakapoyeyuka yote..

asubuhi ile unaamka oga kwanzq na maji ya kawaida (kwa sabuni)

ukishamaliza kuoga sasa chukua maji yale ya chumvi ukiyoloweka njoo yaoge mwili mzima

zoezi litafanyika Asubuhi na USIKU Ukikaribia kulala

Addition: wataalam wa mambo wanasema ukideki nyumba yako ni vizuri ukadekia hio kitu pia
 
Kama nakiona hiko kitambi kinavyocheza mkuu
 
Aisee
 
Ahsante kwa maelezo mkuu, wataalam wa mambo ndio waganga? Sitaki kujihusisha kabisa na mambo ya shirki.
 
Mkuu Kwanza hapo unakumbushwa kuwa makini na watu wako unaenda nao kwenye Kula Bata hata sehemu ya kutuliza akili. (marafiki) siku moja mtakuja kugombana Kwa sababu ya Kijinga ambayo wewe ndio sababu mwenyewe.

Pili kama unaweza kunywa mkojo wako wa asubuhi kunywa au Tafuta mzizi wa MTI wa mjohoro Choma kisha mkaa wake sugua alafu lile vumbi changanya na maji kunywa.

Tatu usipende kulala Chali yaani sura iangalie juu na pia jitahidi kitanda chako kiwe katika upande wa jua linapotoka au linapozama.

Nne Hakikisha una omba Kwa Mungu wako usiku unapolala.
 
Kuhusu umakini nipo makini ila huwezi jua mbaya nani kwa namna binadamu tulivyo na wema machoni lakini wabaya rohoni.

Kunywa mkojo wangu hapo kipengele mkuu.

Kulala chali sipendi na nikilala hivyo hata kwa bahati mbaya nikishtuka nabadili style haraka sana.

Kuomba Mungu nitaendelea kila iitwapo leo maana ndipo imani yangu ilipo.

Shukrani kwa ushauri mkuu.
 
Tafuta huo MTI wa mjohoro.
Hilo tumbo litakuja kukusumbua Sana Mzee wangu na mwisho wa siku utaambiwa una vidonda vya tumbo.
 
Kumbe bora mimi ninae ota mimi ndie muhusika mkuu kwenye movie za kizombie hasa Train to busan😅😅tafuta tafsiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…