Ilala: DC Sophia Mjema athibitisha wagonjwa wa COVID-19 hospitali ya Amana kuleta fujo na kutaka kuondoka wakajitibie nyumbani

Ilala: DC Sophia Mjema athibitisha wagonjwa wa COVID-19 hospitali ya Amana kuleta fujo na kutaka kuondoka wakajitibie nyumbani

Eti mkuu wa wilaya hana uhakika kama ni vurugu.. sasa kwa nini kapokea simu ? Kwa nini anatoa maelezo bila kua na fact ?

Ameshindwa kusema hata anasubiri report ili awe na fact za kuwaambia watu.
Mwandishi nae kilaza sana.
Maswali muhimu kama kulikuwa na wagonjwa wangapi hajauliza.

Malalamiko ya huduma mbovu au kutokuwepo kwa huduma kabisa pia mwandishi hajauliza.
Tumeachwa na maswali mengi
 
Shida hufi peke yako utaambukiza wengine au mbaya zaidi unaweza usife ukaua wengine..., ila nadhani kama watu watajua unaumwa na kukutenga na hao watu wanaokutenga nao kutengwa huenda ikasaidia.., ndugu zenu wengine wawe wanaleta chakula wanakiacha barabarani.... (hapo ni kama mnakaa mbali na majirani)
 
KUNA JAMBO HUKO ITAKUWA WANAKUFA SANA AU HUDUMA NI MBOVU
 
Sophia simba anaficha ukweli
Ukweli ni huu hapa
Jana kuna mwanamke amefariki katika wodi ya corona

Madaktari na wauguzi awataki kuchukua ile maiti
Maiti imeshinda wodini kutwa nzima ya jana
Ikabidi wagonjwa wakaichukua ile maiti mbaka ofisi ya madaktari
Wakasema wagonjwa kama nyie Mnaona kukaa na maiti sio kesi kaeni nayo nyie

Madaktari, manesi na wauguzi pamoja na mapolisi wote kwa pamoja wakatoka nduli kila mtu na njia yake

Ndio sasa vurugu zikaanzia hapo wagonjwa wakavunja mageti wakarusha mawe

Kufika usiku ndio huduma zikarejea na wagonjwa wakaombwa msamaha
Hiyo ndio hali halisi ya Amana

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani mkuu, ina maana hawajatoroka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi.Sophia Mjema athibitisha wagonjwa kulazimisha kuondoka katika Hospitali ya Amana kurejea nyumbani.

===================
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Simba amesema kuwa kulikuwa na wagonjwa ambao walikuwa hawataki kuendelea kukaa hospitali kwa kuwa walikuwa wanajihisi hawaumwi sana.

Hivyo akasema ikumbukwe kuwa mtu akifika hospitali kwa kuhisiwa kuwa na maambukizi ni lazima akae aangaliwe kwanza ndipo aruhusiwe lakini wao walikuwa hawataki bali walikuwa wanataka kurudi nyumbani.

Akasema pia hana hakika kama kweli kuna vurugu zilizotekea isipokuwa wagonjwa walikuwa wanapiga kelele wanataka kurudi nyumbani.

Pia akasema hana hakika kama kweli kuna wagonjwa ambao wametoroka hivyo wanafuatilia swala hilo kwa walinzi wa hospitali ili kujua kama ni kweli wametoroka basi wafatilie ni wagonjwa wangapi na wawafatilie wapo wapi.

''Hili hatuna taarifa hiyo bado hivyo ngoja tulifatilie kwa upande wa wenzetu maaskari wanaolinda hapo na kama wametoroka watakuwa wameendea wapi maana kama mtu alikuwa amehisiwa na anajulikana alitokea wapi hivyo atakwenda kufatiliwa kwenye mtaa aliotekea na atapatikanaili asiweze kwenda kueneza magonjwa kwa watu wengine''

Kwa sasa hospitalini hapo hali ni shwari hakuna tatizo lolote hivyo watulie tu wafatilie taratibu za hospitali na wale ambao wataonekana hawana tatizo wataruhusiwa na kuondoka.

Anasema kuwa watu wana hofu hivyo mtu akijiona hana dalili za ugonjwa kama mafua, kukohoa na kichwa kuuma ni kawaida kwa binadamu kutamani kuondoka, lakini kama alichukuliwa kwa kuwa na viashiria basi ni vyema wakatulia hospitali mpaka taratibu rasmi.

Na wale walio na viashiria hata wakirudi mtaani nako huko watu watawakimbia watawaambia warudi kwanza hospitali wapone ndipo warudi hospitali.

Na pia Amesema wananchi watulie wasikilize serikali inawaambia nini maana kama mgonjwa amepelekwa hospitali kwa kuwa na viashiria vya ugonjwa basi ni bora akatulia asubirie taratibu za hospitali, maana unaweza kaa siku mbili ukijiona kuwa u mzima na na baada ya siku mbili ukawa mgonjwa, hivyo ni bora kusubiri uruhusiwe kwa taratibu zilizowekwa maana hospitali sio jela bali ni kwa aliji ya kuangalia afya.

Mara hana hakika kama kuna vurugu! Mara wanajisikia wananafuu na wanaomba kurudi majumbani. Ila kichwa cha habari amethibisha kutokea vurugu! Nia yako nini sasa?
 
Jambo pekee la kujiuliza ni kwamba " Je serikali iko serious na janga hili?"
Majibu ni mengi kwa mitazamo tofauti, binafsi namshukuru sana Paul Makonda kwa kutulazimisha kuvaa barakoa jambo ambalo limeitikiwa na nchi nzima

Swali langu kuhusu wagonjwa waliotoroka.
1. Je mgonjwa akisha sajiliwa hapewi sare? Kama alipewa imekuwaje akatoka na nguo za kiraia?
2. Kama hawakupewa sare za hospitali nini utaratibu wa hospital za umma katika kudhibiti wagonjwa.
3. Katika mawasiliano ya simu na mkuu wa wilaya ya Ila Ni Sophia Mjema inaonyesha hatuko serious maana hata yeye hana taarifa rasmi kaenda kisiasa zaidi kwamba walitaka kutoroka lakini hathibitishi kama je wamedhibitiwa?

NB: KUNA HAJA YA WAHUSIKA WA WIZARA KUJIHUZULU ILI KUPISHA WENGINE.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi.Sophia Mjema athibitisha wagonjwa kulazimisha kuondoka katika Hospitali ya Amana kurejea nyumbani.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Simba amesema kuwa

Baada ya ugonjwa kupungua au kwisha utamsikia Polepole na Dk. Bashiru wakijitokeza na kuleta dhiaka tumepambana na Corona kama tunavyopambana na mabeberu.
 
Duh! Habari mbaya sana hii,

Hii chain itakayotengenezwa hapo duh nchi haipo salama tena hii nawaonea huruma sana wazee na wenye magonjwa mengine mwilini ni kupukutika tu.

Wacha tufe tu watakao baki watatoa historia na ushuhuda miaka ijayo.
Ndio kusema bado unaomba huu ugonjwa uenee ili utumalize?
 
Kama wamepona waachiwe warudi makwao,rais amesisitiza takwimu za waluopona zionekane
 
Hii ni trela tu...movi lenyewe bado halijaanza....!!
 
Sophia simba anaficha ukweli
Ukweli ni huu hapa
Jana kuna mwanamke amefariki katika wodi ya corona

Madaktari na wauguzi awataki kuchukua ile maiti
Maiti imeshinda wodini kutwa nzima ya jana
Ikabidi wagonjwa wakaichukua ile maiti mbaka ofisi ya madaktari
Wakasema wagonjwa kama nyie Mnaona kukaa na maiti sio kesi kaeni nayo nyie

Madaktari, manesi na wauguzi pamoja na mapolisi wote kwa pamoja wakatoka nduli kila mtu na njia yake

Ndio sasa vurugu zikaanzia hapo wagonjwa wakavunja mageti wakarusha mawe

Kufika usiku ndio huduma zikarejea na wagonjwa wakaombwa msamaha
Hiyo ndio hali halisi ya Amana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mgonjwa wa Covid-19 ambae anashindwa hata kupumua ataweza kubeba maiti? Maana huu ugonjwa unaathiri sana mfumo wa hewa kwa muda mfupi sana.
 
Hapo ndio tatizo la wagonjwa kusambaa mikoni lilipo
Aseme na sababu zinazofanya walazimishe kuondoka na kutoroka
Labda ni tatizo la kutengwa na ndugu zao bila aliyewatenga kuwahudumia.
Fikiria kama mtu alikuwa ana kawaida ya milo mitatu kwa siku ila sasa hata huo mmoja ni shida. Ni lazma atamani hali yake ya awali .
Cha kushauri ni serikali isiwahesabu hawa wagonjwa kuwa mateka au wafungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sophia simba anaficha ukweli
Ukweli ni huu hapa
Jana kuna mwanamke amefariki katika wodi ya corona

Madaktari na wauguzi awataki kuchukua ile maiti
Maiti imeshinda wodini kutwa nzima ya jana
Ikabidi wagonjwa wakaichukua ile maiti mbaka ofisi ya madaktari
Wakasema wagonjwa kama nyie Mnaona kukaa na maiti sio kesi kaeni nayo nyie

Madaktari, manesi na wauguzi pamoja na mapolisi wote kwa pamoja wakatoka nduli kila mtu na njia yake

Ndio sasa vurugu zikaanzia hapo wagonjwa wakavunja mageti wakarusha mawe

Kufika usiku ndio huduma zikarejea na wagonjwa wakaombwa msamaha
Hiyo ndio hali halisi ya Amana

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasema kweli?...
 
Back
Top Bottom