Ulifanyika uchaguzi 2020, Chama Cha mapinduzi kilimpa Magufuli na sa100 ilani waliyopitia nayo Nchi nzima kuinadi Kwa wananchi.
Katika ilani hiyo ya 2020, hakuna mahala popote CCM ilimuelekeza Magufuli na Sa100 kuuza au kukodisha bandari yetu ya Dar Kwa Miaka 100 au zaidi, Bali ilielekeza bandari hiyo iboreshwe na idhibiti wizi na ucheleweshaji wa mizigo Kutoka bandarini na kuongeza ufanisi Ili kuhudumia wananchi na majirani zetu.
Bandari ya Dar ni kitovu Cha Uchumi wetu, hivyo suala hili la kuuza bandari ni la kitaifa, linapasa litokane na ilani ya 2025.
Awamu ya nne, Rais Kagame aliwahi kuiomba bandari ya Dar aisimamie Kwa ufanisi, ombi Hilo wananchi tulilichukulia kama dharau Kwa Nchi yetu na tulikataa Kwa pamoja na kukubaliana kuwa tunaweza kuisimamia wenyewe bandari yetu.
Kama CCM haikuruhusu bandari kukodishwa kupitia ilani Ile ya 2020, Serikali ya Sa100 inatumia ilani ipi kutaka kuibinafsisha bandari ya Dar Kwa miaka 100 au zaidi, bila kupata ridhaa ya chama na wananchi kupitia SANDUKU la KURA?
Nawasilisha🙏🙏🙏🙏🙏