Tatizo Rais ana madaraka makubwa Tanzania kuliko mfalme. Ni kama mungu mtu.
Kwamba anaweza kujiamulia mambo nyeti kama haya yeye kama mtu mmoja. Anaweza asifuate maoni ya Watanzania milioni 60 na hakuna mtu, chombo cha kumuhoji, kumuwajibisha, kumuuliza kitu.
Maoni ya wananchi kwenye issue muhimu kama hii, loliondo, LNG ilitakiwa yazingatiwe, na issue kama tozo, matumizi ya mikopo/ kodi muhimu maoninya raia kuzingatiwa.
Kinga ya kutoshitakiwa iondolewe Kwa viongozi wote hadi Rais.
Bunge, mahakama, vyombo vya habari viwe na meno na Uhuru wa kuhoji, kupiga Kula ya kutokuwa na Imani na Rais kama anafanya vitu kinyume na maslahi ya Taifa.
Rais aweze kushtakiwa na mahakama kuwa huru kutoa hukumu bila kuingiliwa na yoyote.
Issue kama hii, umeme, loliondo na nyingine muhimu ingebidi Rais aulizwe maswali na vyombo vya habari / wananchi na atoe ufafanuzi.
Bila uwazi, uwajibikaji ni vigumu hii nchi kupiga hatua, kuepuka maamuzi yasiyo na tija kwa maslahi ya Taifa.