Ilani ipi ya Uchaguzi inatumika kutekeleza issue hii nyeti?

Mimi sitakubali, nawashtakia Kwa Muumba aingilie kati,

CCM hatukumtuma haya.

Wananchi hatukuagiza haya, maamuzi haya wanatoa wapi?
 
USALAMA wa Taifa KAZI yake nini?

Hili halikubaliki!!!!!!!
 
Mimi si mwanasheria, lakini Rais hawezi jiamulia vitu tu kuna context katika hilo na katiba imeweka wazi nje ya hapo ni kuvunja katiba na sheria inaruhusu kushitakiwa iwapo atavunja Katiba...Kwamba haijawahi kutokea yeyote akashitakiwa hili ni tatizo la nchi na wananchi zaidi kuliko Katiba...Labda mnipe mwongozo.
 
Nenda kasome muswada.

Kuwaza tu kuibinafsisha bandari Kwa wageni ni DHAMBI isiyosameheka!!!
 
Alichofanya awamu ya pili Loliondo kinasumbua mpaka leo, na hakuna impact yoyote positive aliyofanya mwarabu kwa wananchi, hili la bandari litakuwa kitanzi.
Mikataba hii ni mibaya,

Magu aliishia tu kuchungulia Loliondo na kuacha,

Mikataba ya namna hii inaumiza Nchi na vizazi vijavyo,

Enyi mnaoshika zamu , Enyi walinzi wa Nchi hii msikae kimya.

Nchi hii ni yetu sote, itoshe kusema yatosha.

Ni huzuni kiasi Gani kuwa watumwa katika Nchi yetu wenyewe?

Kwanini tunasikia habari mbaya Kila uchao katika Nchi yetu?
 
Nenda kasome muswada.

Kuwaza tu kuibinafsisha bandari Kwa wageni ni DHAMBI isiyosameheka!!!
Siwezi kuusoma acha niendelee kuamini ni uzushi....

Basi hatuna walinzi na nchi imetekwa kama ndivyo, nisemeje sasa kwamfano?
 
Afufuke basi MTIKILA kufungua kesi ya kikatiba kupinga hili ikiwa KIBATALA na LISSU wameshindwa!!!!
Kibatala na Lissu hawawezi kum-interrupt adui yao, kama anafanya makosa. Naona jinsi wanavyoshangilia kimya kimya huku wakiongeza hoja kwenye kitimtimu cha siasa jukwaani. haha
 
Watu hawajifunzi kwa yale yanayotokea SA na Zimbabwe.
 
Yaani tupoteze Ajira ya wtz, tupoteze biashara na Burundi, Zambia, DRC, Rwanda, Uganda sababu ya tamaa na kushindwa kuwajibika Kwa viongozi Wachache?

Yaani naskikia huzuni na HATIA moyoni kana kwamba maamuzi haya nimefanya Mimi!!!!

Ee Mwenyezi Mungu ingilia kati utuokoe🙏🙏🙏🙏
 
USALAMA wa Taifa KAZI yake nini?

Hili halikubaliki!!!!!!!

Usalama iko chini ya Rais. Hakuna chombo Tanzania chenye uwezo kiuhalisia kuhoji au kumuita Rais atoe ufafanuzi amefikiaje maamuzi fulani.

Trump ana kesi kadhaa na amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Boris Johnson ameitwa kujitetea na kufafanua maamuzi yake wakati wa COVID na tume maalum ya uchunguzil

Ikumbukwe tayari alishinikizwa kuwajibika na kujiuzulu Uwaziri mkuu.

Wachunguzi wamechukua mawasiliano yake ya simu, chats, notebook, SMS, WhatsApps, diaries, zake, yeye pia atahojiwa na tume.

Ukijua maamuzi yako kama siyo sahihi yatachunguzwa na kuna uwezekano wa kuwajibika na kuwajibishwa utajitahidi kuchukua maamuzi sahihi tofauti na ukijua hakuna uwajibikaji wala kuwajibishwa wala uwazi.
 
CCM ni janga
 
Hapa alipogusa ni nyeti sana, kelele zitapigiwa Hadi na majirani wanaonufaika na Bandari ya Dar.
 
Hapa alipogusa ni nyeti sana, kelele zitapigiwa Hadi na majirani wanaonufaika na Bandari ya Dar.

Issue zote muhimu kiongozi mkuu wa TZ huwa kimya. Issue kama umeme, maji, Loliondo, Hii ya Bandari, mfumuko wa bei, nk.

Report ya CAG sina uhakika kama kuna hatua yoyote imechukuliwa kwa mtu yoyote.
 
CCM ni janga
Katika hili CCM wasisingiziwe,

Ilani ipi inatumika kutekeleza haya?

Aulizwe mamlaka haya kayatoa wapi, ndani ya Chama kupitia ilani ipi?

Asubiri 2025 ikitokea kakabidhiwwa ilani inayoruhusu hayo ndipo aje kuomba ridhaa ya wananchi aone kama atatoboa!!!!!

Hiki ni kipindi Cha mpito, hapaswi kugusa sehemu nyeti namna hii!!!
 
Kama mbuga,,,migodi,,gesi,, zinabinafsishwa na raia kuondolewa,,watashindwa bandari kwa hulka ya viongozi wetu na ubinafsi wa hovyo waliokuwa nao na kutojali maslahi yenye tija kwa taifa hili,,,Hili la bandari ni kweli kwa % 99.99!!Watu hawewezi kurupuka na kuropoka tuu ni lipo kama halipo Lipo njiani linakuja!!
 
Wanaotekelwza hayo ni ukawa au mazimwi,?
Ukimya wa CCM ni jibu kwamba imebariki hayo.

Janga letu ni CCM
 
Tusikubali SULTAN kuichukua Bandari salama Kwa mgongo wa uwekezaji!!!

Tutumie uhuru wetu kukataa na kulaani hili.
 
Wanaotekelwza hayo ni ukawa au mazimwi,?
Ukimya wa CCM ni jibu kwamba imebariki hayo.

Janga letu ni CCM
Katika hili la Bandari, Janga ni Sa100!!
 

Kiuhalisia Rais wa Tanzania Yuko juu ya katiba, Bunge, mahakama, Watanzania wote milioni sitini.

Nani au chombo gani kiuhalisia kina meno na kinajiamini cha kumuhoji, kumshtaki au kumtoa madarakani?

Nani amempa idhini, mamlaka SSH kusaini MOU, aliwauliza Watanzania, aliliuliza Bunge kama katiba inavyotaka?

Alifuata katiba au alifanya kinyemela kwa usiri mkubwa? Sababu SSH anajua anachofanya sio sahihi na ni kinyume na katiba na maslahi ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…