Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

11953226_800129036771756_8497164063140780257_n.png
 
Teh teh teh ukawatajia katiba mpya MACCM ni kama unawalazimisha kuja.mba hadharani.

Wao wanampango wa kutununulia sisi waalimu laptop mpyaaaaa kotoka china,
alafu watugawie vijiji vyote nchini mil50 "TZS" kwa kila kijiji (vijiji 12,000 * 50,000,000 = 600,000,000,000 i.e bil 600),
alafu wakimaliza watujengee kiwanda cha samaki teh teh teh (huku Kanda ya ziwa tunakula mapanki),
alafu wakimaliza wawagawie wachina gesi na mafuta ya nchi hii,
alafu wakimaliza wazindue vyoo tutakavyojengewa na wachina kwa thamani ya mabilioni,
alafu wakimaliza tuwapigie makofi na kuimba iyena iyena,
na wao wahitimishe kwa kutuita sisi WAPU.MBAVU na MAL.OFA.
11058630_799445870173406_283617673143350987_n.png
 
Huyu magufuli hana jipya wizara yake ya ujenzi imefeli, wakandarasi wanaidai serikali mpaka wengine wamekufa kwa presha kwa madeni kwenye mabenki halafu eti ndio jembe? Huyu ndio mchapakazi wa ccm wizara imemshinda nchi ataiwezaje? Magufuli angejitazama kwanza ndio aanze kampeni hafai hafiti ni janga lingine nchi hii.
11891209_799097420208251_3954131202743216338_n.png
 
CCM ingezaliwa demu mwaka 2015 isingepata hata men wa Sound!!
 
Unajua cc hatupendi mijada ya namna hii inafanya wananchi kuwa na hasira na serikali yao acheni mara moja tujadili mambo mengine sio haya
 
Vipaumbele:
1. Elimu
2. Afya
3. Kilimo
4. Miundombinu
5. Utawala bora
6. Mawasiliano

Swali: Je, kwa takribani miaka 54 ya kuwa madarakani wametekeleza hayo kwa kiwango gani cha kuridhisha wananchi?!

Je, kwa sasa kuna miujiza gani watakayotumia kutekeleza ilani hiyo?


Ilani kuu ya uchaguzi 2005 na 2010: Kasi mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya iliishia wapi? Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Nadhani ccm wanawaona watanzania kama mazuzu hivi, maana wanabadilisha biti tu lakini wimbo ni uleule!





Ndugu wewe.hujaona serikari iliyokufanyia mpaka na wewe leo unajitambua? Leo umepata elimu kupitia shule.zilizojengwa na serikari ya ccm na una afya njema sasa hivi kupitia serikari ya ccm inakuaje unaanza kudharau waliokupa hiyo elimu yako ukajitambua. Hata siasa haiko.hivo ukawa mmezidi na tumewashtukia
 
Ndugu wewe.hujaona serikari iliyokufanyia mpaka na wewe leo unajitambua? Leo umepata elimu kupitia shule.zilizojengwa na serikari ya ccm na una afya njema sasa hivi kupitia serikari ya ccm inakuaje unaanza kudharau waliokupa hiyo elimu yako ukajitambua. Hata siasa haiko.hivo ukawa mmezidi na tumewashtukia

acha kututangazia ujinga wako ndugu kaa nao tu siyo mpaka na sisi tukujue kuwa u mjinga
 
Ndugu wana JF
sikubahatika kuangalia uzinduzi wa kampeni za CCM,kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu
KWA WALIOBAHATIKA KUANGALIA NAOMBA KUJUZWA KAMA HAWA WALIONGELEA ISSUE YEYOTE KUHUSIANA NA SWALA LA KATIBA MPYA MAANA BADO IKO PENDING
NAOMBA KUWASILISHA
 
Labda kama alisahau kutusomea siku ya uzinduzi,maana magufuli siku ile alikuwa kwenye pressure kubwa inawezekana alisahau,vinginevyo hatukusikia
 
Wao hii iliyopo ndo inawanufaisha kwahyo hawakuwa na sababu ya kuweka tunayoitaka sisi malofa
 
Hatukusikia wakiongelea Katiba labda kwenye kampeni zake.
 
Katiba mpya ilikuwa gia ya kikwete ya kupiga hela za walalahoi na malofa tu.hawakuwa na dhamira ya dhati ndio maana wapo kimya
 
yeye kama kiongozi mkuu wa awamu ya tano, inatakiwa umhukumu kwa aliyoysema pia muangalie usoni na anachokisema je kinaendana , dr maghufuli atatuvusha ni kiongozi mwenye muono wa miaka 100 ijayo,

TM 2015( Twende na Maghufuli 2015)

Hapa kazi tu
Atawavusha nyie na liccm lenu, ila sio Tanzania!! mwenye uwezo wa kuivusha tanzania ni Lowassa tu!!!
naamini Tanzania tutakuwa na kupaa kiuchumi kuliko utawala wowote
Unachesha kweli!! Kama ccm mmeshindwa kwa miaka zaidi ya hamsini je miaka 5 mtaweza ?? embu usijitoe ufahamu wewe mtoto.

Kwa kuongezea tu, embu jaribu kufikiria haya:
1. Pembe za ndovu zilizoshikwa huko uswis
2. Uonevu wa vyombo vya dola
3. Kuporomoka kwa shilingi (1USD=2000+ Tsh) naimani wewe ni msomi na utanielewa hapo namaanisha nini!!
4. Kusafirisha twiga kwenye ndege (sijui kama walizikatia tiketi au la)
5 etc etc...

Kwa hayo yoooote bado unatujipa moyo ccm wataibadili hii nchi???????? hnajua hata wewe uko ccm kwa sababu ya pesa, na kama sio hivyo trust me leo usingekaa na kupigia debe chama cha majambazi!!! think.
 
Katiba mpya ilikuwa gia ya kikwete ya kupiga hela za walalahoi na malofa tu.hawakuwa na dhamira ya dhati ndio maana wapo kimya

Bora umefunguka aisee kama una ushahidi zaidi wa jinsi alivyopiga hela njoo nao uweke hapa ili tuheshimiane!
 
Ipo kimya kimya kwa style ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia kumbe kuna fisi, soma vifungu 144. (e), 145. (g) 188. (a) vya ilani hiyo. Kwenye utangulizi wa ilani hiyo haitajwi wala kwenye kampeni haizungumziwi, ila in short ukiipigia kura CCM umepitisha kukamilisha utekelezaji wa Katiba Pendekezwa ya Bunge la Sitta. Akili za kuambiwa....


Ndugu wana JF
sikubahatika kuangalia uzinduzi wa kampeni za CCM,kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu
KWA WALIOBAHATIKA KUANGALIA NAOMBA KUJUZWA KAMA HAWA WALIONGELEA ISSUE YEYOTE KUHUSIANA NA SWALA LA KATIBA MPYA MAANA BADO IKO PENDING
NAOMBA KUWASILISHA
 
Katika uongozi wake Mh JOHN POMBE MAGUFULI ameahidi kutekeleza yafuatayo;
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda vya ndani
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za mwana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa.

CCM NI MBELE KWA MBELE
 
Back
Top Bottom