Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,222
- 2,912
Nikiwa mdogo kama walivyo watu wengi kuna mambo unakuwa huyaelewi elewi na kadiri unavyokuwa ndivyo unavyoendelea kupata ufahamu
Nikiwa mdogo nadhani hadi umri wa kidato cha Pili (hapa sio mdogo tena hii ilikuwa imani) tungegombana endapo ungeniambia "nafaa" kuwa mwanajeshi au uniambie nikiwa mkubwa niwe mwanajeshi au hakimu/Jaji
Kwa makuzi yangu na malezi yangu yaliyohusisha kumpenda Mungu na kujifunza neno la Mungu, niliamini kabisa kuna watu wa aina mbili wao walikwishajitenga na Mungu kwa hiyari yao na kwa vile nimekulia kijijini sikushangaa kuamini kwamba hata kanisani hawaendagi maana ni kweli nilikuwa siwaoni
Tukiwa darasa la tano kijijini kwetu alihamia hakimu wa mahakama ya mwanzo aliyekuwa wa dhehebu ninalosali na wengi tulimfahamu kwasababu alikuwa wa kutoka mjini (wa mjini akihamia kijijini life style inamtangaza), Pia mmoja wa watoto wake tulikuwa darasa moja
Huyu alihamishia makazi yake kijijini kwetu hakuishi makao makuu ya wilaya kama waliomtangulia.
Alizoeleka sana na watoto wake kwa vile tulikuwa tunasoma shule moja tumecheza nao kombolela, mchazo wa baba na mama na zile za kitoto toto za kulala juu ya mwingine, kutekenyana, nk tumezipitia
Kilichonishangaza kwa huyu hakimu na familia yake, kila Jumapili walihudhuria kanisani tena walipangiwa kusoma masomo na kupeleka vipaji
Kabla sijamaliza kushangaa, miaka michache baadae kijijini jirani ikawekwa kambi ya jeshi, kama kawaida yao vurugu zikawa nyingi kijijini na vijiji jirani. Wake za watu wakawa wake zao, kila sehemu ya starehe wanaijaza wao, kukiwa na mechi za vijiji na wao wanataka washinde wao, na vurugu nyingine
Hata hivyo mara moja moja nikawa nao baadhi yao tunakutana nao kanisani, sadaka wanato tena hadi mwili wa kristu wanapokea!
Miaka michache baadae nikiwa sekondari bilashaka kidato cha nne, siku moja tukiwa kanisani nikashangaa karibu robo tatu ya waumini ni wanajeshi! Kumbe lilikuwa kanisa lililokaribu na kambi na baadhi ya wanajeshi walikuwa viongozi kwenye jumuiya na kwenye kikango
Kufupisha story yangu ya utotoni, ni kwamba taratibu nilianza kuelewa kuwa hizo ni kazi na ajira kama zilivyo ajira nyingine
Hata hivyo, kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele na sasa naelekea uzeeni naanza kuamini kuwa sikukosea nilipokuwa mdogo kuwashangaa wanajeshi na mahakimu kwenda kwenye nyumba za ibada na kuamini kuwa hili kundi linajua kabisa mbinguni haliendi
Kwa mfano, sote tunafahamu kwamba Rais anatokana na siasa za vyama ambao hawamiliki siraha wala mamlaka yoyote ya kiulinzi zaidi ya maneno maneno tu
Hakuna asiyefahamu kwamba usalama wa nchi hauko mikononi mwa Rais wala wizara yotote bali uko mikononi mwa taasisi ya usalama wa Taifa ambayo "inamilikiwa" na watu waliotokana na jeshi wala sio siasa
Hakuna asiyefahamu kwamba Jaji mkuu pamoja na mwanasheria mkuu wanaowajibu wa kumuwajibisha yoyote bila kujali cheo chake cha kisiasa au cha kijeshi pale anapovunja sheria
Sasa, oktoba 29 ya mwaka 2025 imeua watu, imechinja watu, imepiga risasi watu;
Jeshi lipo linaangalia, usalama wa Taifa wapo wanaangalia, majaji wapo wanaangali, mbinguni wataenda kweli?
Kuna watu wanaitwa wasiojulikana, wanateka watu, wanaua watu, wanadhalilisha watu;
Jeshi lipo linaangalia, mahakama zipo zinaangalia, usalama wa Taifa wapo wanaangalia;
Wanamjua Mungu kweli hawa? Wanaenda nyumba za ibada wakimaanisha kweli?
Viongozi wa kisiasa wanaropoka wanavyojisikia kauli mbaya mbaya za kudhalilisha na kutweza utu wa watu wengine;
Jeshi lipo linaangalia, usalama wa Taifa wapo wanaangalia, mahakama zipo zinaangalia;
Halafu uniambie fikra zangu za utotoni hazikuwa sahihi? Hapana, mimi naamini nikuwa sahihi kuamini kwamba hawa watu walishajichagulia njia nyingine tofauti na hii inayosemwa kwenye nyumba za ibada