ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 1,400
- 2,623
1. Baada ya kafara ile watu hawafi tena?Mshahara wa dhambi ni mauti,,, na mwanadamu ilitakiwa afe kutokana na dhambi yake ya kula tunda bustanini.......
Sasa sheria haijui msamaha, na hukukuwa na mbadala wa kumwokoa mwanadamu na mauti.......
Hivyo MUNGU kwa upendo wake, akajitoa kufa kwa ajili yetu ili tusife milele.......
Habari ya kafara ilienda kwa nani, MUNGU ndiye mwenye uwezo wa kusamehe...... na kama YESU angekuwa ametenda dhambi asingefufuka baada ya mauti yake.......
Be blessed mkuu!
2. Kafara ile ni kwa dhambi zilizofanyika kuanzia wakati ule kurudi nyuma ama mpaka leo?
3. Kwakuwa aliyetunga sheria hizo ni Mungu, kwanini asingeamua kubadili sheria yeye mwenyewe na kuanza kusamehe hadi amtese mwanaye wa pekee?
4. Imekuwaje kafara kubwa kiasi ikashindwa kuondoa dhambi kabisa ulimwenguni?
5. Kwakuwa Mungu ni muweza wa yote (kadiri ya mafundisho), kwanini asingemuua tu shetani ambaye ndiyo mzizi wa uovu wote ulimwenguni ili kumaliza dhambi iishe kabisa na watu wake wapate kuishi kwa amani badala ya kumuua mwanaye wa pekee ili kufidia uharibifu uliofanywa na shetani?
Mkuu nisaidie majaabu ya hayo maswali niongeze ufahamu wangu juu ya Theology na fumbo hili kubwa la imani