Ile kafara ya YESU KRISTO ilienda kwa nani? MUNGU AU SHETANI?

Ile kafara ya YESU KRISTO ilienda kwa nani? MUNGU AU SHETANI?

Ukombozi wa kiroho kwa makosa ya kimwili. Naomba maelezo kdgo hapa
mwili unapewa ruhusa na roho kwann ukiona uchi wa mtoto hupati hisia za mapenz angali ukiona wa mtu mzima unapata hisia? Ukombozi wa roho ni ukombozi wa mwili na dhambi ya mwili ni ya roho
 
Naam
Warumi 6:23....
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele.


Biblia yenyewe inasema kila mtu atawajibika kwa dhambi zake mwenyewe (Ezekieli 18:20). Yesu pia alisema mtu akitaka kuingia katika uzima, azishike amri za Mungu (Mathayo 19:16–19).


Kwa hiyo, unaweza kujiuliza: ikiwa mtu husamehewa kwa damu ya mtu mwingine, kwa nini Biblia inasema kila mmoja atawajibika kwa dhambi zake?
 
Mshahara wa dhambi ni mauti,,, na mwanadamu ilitakiwa afe kutokana na dhambi yake ya kula tunda bustanini.......

Sasa sheria haijui msamaha, na hukukuwa na mbadala wa kumwokoa mwanadamu na mauti.......

Hivyo MUNGU kwa upendo wake, akajitoa kufa kwa ajili yetu ili tusife milele.......

Habari ya kafara ilienda kwa nani, MUNGU ndiye mwenye uwezo wa kusamehe...... na kama YESU angekuwa ametenda dhambi asingefufuka baada ya mauti yake.......

Be blessed mkuu!

Lakini Biblia pia inasema: “Mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe” (Ezekieli 18:20), na Mungu alisema kwa mwenye dhambi: “Akiiacha dhambi zake... hakika ataishi” (Ezekieli 18:21-22).

Kwa hiyo, kama Mungu anaweza kusamehe mwenye kutubu, swali linabaki: kwa nini asiwasamehe moja kwa moja badala ya kumfanya asiye na dhambi alipe deni la mwenye dhambi?
 
Asante mkuu...

Watu wa zamani walikuwa wanahesabiwa haki kwa kumwamini MUNGU hapakuwa na ubatizo.....kama akina Ibrahim

Sasa MUNGU alipowatoa israel utumwani alitaka awafanye wawe kielelezo kwa mataifa mengine....

Akawapa maelezekezo kama taifa takatifu, na maelekezo ya ibada...

Ambapo aliwaambia kama mtu atatenda dhambi itapaswa atoe kafara ya kondoo au njiwa kwa ambae hana uwezo....

Sasa huyo mnyama itabidi umuchinje na unaungama dhambi zako, kwa hiyo yeye anakufa kwa ajili yako!

Woote hao wanyama walimwakilisha YESU aliyekufa msalabani....

Lakini Biblia pia inasema Mungu anataka toba na utii, si damu tu. “Nataka rehema, wala si dhabihu” (Hosea 6:6).

Na kuhusu wanyama, Mungu alisema: “Mtu atakufa kwa sababu ya dhambi yake mwenyewe” (Ezekieli 18:20). Pia Yesu mwenyewe alisema: “Ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri” (Mathayo 19:17).

Kwa hiyo swali ni: kama kafara ya wanyama ilikuwa picha ya Yesu, kwa nini Yesu alisisitiza toba, utii na kushika amri?
 
Lakini Biblia pia inasema Mungu anataka toba na utii, si damu tu. “Nataka rehema, wala si dhabihu” (Hosea 6:6).

Na kuhusu wanyama, Mungu alisema: “Mtu atakufa kwa sababu ya dhambi yake mwenyewe” (Ezekieli 18:20). Pia Yesu mwenyewe alisema: “Ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri” (Mathayo 19:17).

Kwa hiyo swali ni: kama kafara ya wanyama ilikuwa picha ya Yesu, kwa nini Yesu alisisitiza toba, utii na kushika amri?
kwanza ile damu ipo hai iliifanye kazi inatakiwa kuwe na toba, utii na kushika amri zake.
Ndo maana alisisitiza bila hivyo damu haimtakasi mtu.
 
Namna mchakato wa Mungu dhid ya shetan ulivyo mrefu ndo inafanya watu wamkubali shetan au watilie shaka uwezo wa Mungu kwamba kwann hii vita inadum namna hii! ilianza kabla ata ya binadam kuumbwa na ipo tu had leo na haijulikan itaisha lin; kama n vita bas n Israel na Palestina😂.

Apo ndo linaibuka na ilo swali kwamba vita gan hii had Mungu anatoa kafara!? na kamtolea nan iyo kafara!, kafara ya ukombozi unaokosa uhalisia maana dhambi zinaendelea kama sio kuzid na yeye kasema zikizid n ishara ya hukum ya mwisho ukitoa ile ya gharika.

Jibu n watu wanajiuliza hayo maswali sababu hawajui shetan nnn baada ya kuambiwa n malaika aliyeasi_ingekuwa shetan malaika aliyeasi hii vita ingekuwa rahis sana ila n ngumu sababu shetan n uasi uliomuingia malaika, point ya kwanza kujiuliza n je? huu uasi umetoka wap na umetokana na nn.

Uasi n nguvu kinzan, kwenye kanun za ulimwengu hii n polarity/kinyume_kila kitu kina kinyume chake
Kinyume cha Mungu n shetan,
Kinyume cha chanya n hasi,
Kinyume cha nuru n giza.
Sasa kuiondoa iyo kanun n kama kuifanya shiling iwe na pande moja.
Sio mchakato rahis japo unawezekan na sis kwa vile tupo kwenye huu ulimwengu unaofinyangwa uwe na hali moja tu ya Nuru lazima tupate shida uku tukiwa tumepewa njia yakufuata ili tuwe huru baadae na ndo apo linaibuka neno Iman au matarajio mema.
 
Back
Top Bottom