Matunzo 02
JF-Expert Member
- Jul 7, 2026
- 1,620
- 3,165
- Thread starter
-
- #81
mwili unapewa ruhusa na roho kwann ukiona uchi wa mtoto hupati hisia za mapenz angali ukiona wa mtu mzima unapata hisia? Ukombozi wa roho ni ukombozi wa mwili na dhambi ya mwili ni ya rohoUkombozi wa kiroho kwa makosa ya kimwili. Naomba maelezo kdgo hapa
Naam
Warumi 6:23....
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele.
Mshahara wa dhambi ni mauti,,, na mwanadamu ilitakiwa afe kutokana na dhambi yake ya kula tunda bustanini.......
Sasa sheria haijui msamaha, na hukukuwa na mbadala wa kumwokoa mwanadamu na mauti.......
Hivyo MUNGU kwa upendo wake, akajitoa kufa kwa ajili yetu ili tusife milele.......
Habari ya kafara ilienda kwa nani, MUNGU ndiye mwenye uwezo wa kusamehe...... na kama YESU angekuwa ametenda dhambi asingefufuka baada ya mauti yake.......
Be blessed mkuu!
Asante mkuu...
Watu wa zamani walikuwa wanahesabiwa haki kwa kumwamini MUNGU hapakuwa na ubatizo.....kama akina Ibrahim
Sasa MUNGU alipowatoa israel utumwani alitaka awafanye wawe kielelezo kwa mataifa mengine....
Akawapa maelezekezo kama taifa takatifu, na maelekezo ya ibada...
Ambapo aliwaambia kama mtu atatenda dhambi itapaswa atoe kafara ya kondoo au njiwa kwa ambae hana uwezo....
Sasa huyo mnyama itabidi umuchinje na unaungama dhambi zako, kwa hiyo yeye anakufa kwa ajili yako!
Woote hao wanyama walimwakilisha YESU aliyekufa msalabani....
kwanza ile damu ipo hai iliifanye kazi inatakiwa kuwe na toba, utii na kushika amri zake.Lakini Biblia pia inasema Mungu anataka toba na utii, si damu tu. “Nataka rehema, wala si dhabihu” (Hosea 6:6).
Na kuhusu wanyama, Mungu alisema: “Mtu atakufa kwa sababu ya dhambi yake mwenyewe” (Ezekieli 18:20). Pia Yesu mwenyewe alisema: “Ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri” (Mathayo 19:17).
Kwa hiyo swali ni: kama kafara ya wanyama ilikuwa picha ya Yesu, kwa nini Yesu alisisitiza toba, utii na kushika amri?