KERO ILEMELA, MWANZA: Je, Serikali ya CCM Inashindwa Kumdhibiti Mwana CCM Anayevunja Sheria?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
ILEMELA, MWANZA: Je, Serikali ya CCM Inashindwa Kumdhibiti Mwana CCM Anayevunja Sheria?

Buswelu A – Majengo Mapya, Ilemela. Mwaka 2019, wananchi wa eneo hili waligundua kuwa kuna mpango wa kujenga baa katikati ya makazi yao. Kwa kuwa sheria za nchi zinadhibiti wazi wapi baa zinaweza kujengwa kupitia mipango ya matumizi ya ardhi na utoaji wa leseni, wananchi walichukua hatua ya kisheria.

Waliandika barua rasmi za kupinga, na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilichukua hatua na Mkurugenzi kusitisha ujenzi. Wamiliki wa eneo hilo, SHIRIKA LA MAENDELEO ENDELEVU MWANZA (SHIMEMWA), waliitwa kutoa maelezo.

Baada ya ukaguzi, Manispaa ilibaini na kuthibitisha:
  • Matumizi ya eneo hilo ni makazi maalum na biashara ya maduka pekee.
  • Ujenzi ulioidhinishwa ni wa uzio na stoo pekee, siyo biashara ya baa.

Wananchi walipumzika wakidhani haki imetendeka. Lakini mshangao ulitokea. Baa ilifunguliwa kwa jina la ‘THE FOGO GRILL’. Leo hii inaendeshwa kwa jina ‘THE ROCK SPORTS BAR & GRILL’, na kero iliyoanza miaka hiyo bado inaendelea hadi leo.

Wananchi wanalalamika kuhusu:
1. Kelele za muziki zenye sauti kubwa kupita kiasi, kinyume na viwango vinavyoruhusiwa kisheria.
2. Ukiukaji wa amani na utulivu wa makazi, hadi kuwalazimu majirani kukabiliana na walevi usiku wa manane.
3. Ueneaji wa tabia chafu kama vile matusi na umalaya mbele ya watoto wadogo.

Madhara haya yameshathibitishwa kwa nyakati tofauti kutegemeana na vyombo husika vifuatavyo:
  • Ofisi ya Officer Commanding District (OCD),
  • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,
  • Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Buswelu Kaskazini Kitalu ‘A’,
  • Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Swali Kubwa Mbele ya Umma:

Kama eneo hili halina uhalali wa matumizi ya biashara ya baa, na kama imethibitishwa kuwa biashara hii inavunja Sheria ya Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004, Kifungu cha 106(5) kwa kutoa kelele zinazozidi kiwango kinachoruhusiwa, kwa nini Serikali haijachukua hatua yoyote hadi leo? Hata wananchi kujibiwa barua kuhusu hizi kero imekuwa shida?! Au je, ni kwa sababu anayedaiwa kuwa mwenye baa hiyo ni kiongozi wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa Mkoani Mwanza, aliyepata umaarufu hivi karibuni baada ya kuhama kutoka CHADEMA kwenda CCM?

Ikiwa sheria inatumika kwa wote bila upendeleo, basi hatua stahiki zichukuliwe mara moja. Ukiukaji wa sheria haupaswi kufunikwa kwa kivuli cha siasa. Wananchi wa Buswelu A wanastahili kuishi katika mazingira salama na yenye utulivu, kama inavyoelekezwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kuandika barua tu haitoshi ikiwa changamoto bado inaendelea, ni vizuri kupeleka malalamiko yako na jamii ya eneo husika kwenye mamlaka husika gentleman, ikiwa ni pamoja na mahakamani na itapendeza zaidi.

ila ikiwa unatafuta kiki na public sympathy humu jukwaani, utapata but haitakusaidia chochote 🐒
 
Acha mmletewe bar hapo mjaziwe wauza nyap watu wanyanduane ndicho kilichobaki

Ova
 
hizo mambo haziruhusiwi kabisa gentleman, unyanduzi? hapana,

na hata mtoa hoja na jamii inayoathirika na wanachoona ni usumbufu kwao, wakijipanga vizuri, eneo hilo linaweza kuendelea kua na hizo bar but with soundproof na huo ndio ustaarabu duniani kote 🐒
 
Back
Top Bottom