Hapo kuna tatizo la kumuangalia mtu badala ya kuangalia hoja.
The logical fallacy is called ad hominem.
Kwa msimamo huo, wewe unaweza kupotoshwa kirahisi sana siku DP World wakijua kwamba Watanzania wanamuamini sana Issa Shivji kutokana na misimamo yake ya awali, wakamuhonga, akaja aka support DP World, na wewe kwa sababu unapenda kuangalia mtoa hoja, badala ya hoja, ukasema "Hata Issa Shivji kaikubali DP World, mimi ni nani niikatae?".
Unajiweka katika hali ya kukataa neno la kichaa, kwa sababu limesemwa na kichaa.
Siku kichaa atapata nafuu, labda kapewa dawa, atakwambia usipite njia hiyo kuna joka kubwa mbele hapo.
Wewe utasema huyu kichaa tu, maneno yake hayana msingi, hutataka hata kuhakiki maneno yale kama yanaweza kuwa ya kweli.
Utapita kwa mbwembwe zote njia ile na kugongwa na joka kali.
Tujadili hoja, tuache kujadili mtu.
Kama hoja ni mbovu, ipangue tu hoja huna haja ya kumsakama mtu.Hoja mbovu ni mbovu tu hata ikitolewa na nani, sasa kwa nini unaangalia mtu badala ya hoja?
Ukianza kumsakama mtu wakati hujajibu hoja, unaonekana kama umeshindwa kuijibu hoja, na sasa unakimbilia kumsakama mtoa hoja.
Sent from my SM-S908U1 using
JamiiForums mobile app