Kwa kweli unachokisema ni kweli kabisa and it is very clear, bila ku adress madai ya M23, hii vita haitakwisha. Leta majeshi yote unayotaka, honga ma Raisi wote unaotaka wa SADEC, EAC, AU hata MONUSCO hutaweza maliza hii vita. Nini madai ya M23 na kwanini hii vita haimaliziki? Kuna jamii kubwa ya wa Congo wanao ongea Kinyarwanda ambao ndio wahusika wakuu wa hii issue, wamo Wanyamurenge, Wanya Masisi etc, wote hawa ni wa congo lakini lugha yao ni Kinyarwanda au lugha inayofanana na kinyarwanda, kama walivyo Wahangaza, Waha, Washubi etc(TZ), Wakiga (UG). Hii jamii ya wa Congo wanaoongea Kinyarwanda wamekimbia kwao (Congo) na takribani 350K wako Uganda na 200k wako Rwanda kama wakimbizi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Hawa ndio ambao vijana wao wanajiunga na M23 kila inapobidi wanarudi kudai haki yao ya kurudi nyumbani na kuachana na ukimbizi. Walikuwepo akina Nkunda, Ntaganda na sasa Makenga, mtawapiga lakini watarudi tuu. Sasa sijui Tanzania na SA watabakisha majeshi yao huko milele na milele kwani hawa watu hawataacha kupigania haki yao. In fact TZ na SA wanafanya makosa kuingilia kwenye mzozo wa wenyewe kwa wenyewe. Ni kama vile Chadema anyanyasike kupita kiasi then aanzishe varangati kutaka haki yake ndani ya TZ then baadhi ya nchi zije kuwasaidia kijeshi. Hii ni against AU na UN charters.
Bahati mbaya sana hapa kwenye hili jukwaa kuna watu wanashabikia bila hata kujua nini kinachoendelea, kwa kweli kama Baba wa taifa mwalimu J.K.Nyrere angekuwa bado hai, TZ isingepeleka majeshi kule DRC, Na Kama Nelson Mandela angekuwa hai SA isingethubutu kupeleka majeshi DRC kwenda kuisaidia Congo kupiga raia wake yenyewe kisa viongozi wana pocket few millions in dollars.
So kwa kumalizia Sababu na Madai ya M23 kwenye huu mgogoro, pamoja na kupigania haki ya watu wao zaidi ya 600k walioko ukimbizini Uganda, Rwanda na hata Kenya kwa zaidi ya miaka 25 Mengine wasikilize hawa wazee wa Busara Nyerere, Mandera na Mbeki kwenye hizi video hapa chini then utajua ni nini madai ya M23(See Attachement)