Ili kuvunja circle ya umasikini tuliyo nayo watu weusi ni muda sasa tuzingatie "FAMILY BUSINESS"

Ili kuvunja circle ya umasikini tuliyo nayo watu weusi ni muda sasa tuzingatie "FAMILY BUSINESS"

Kuna akina sisi ambao ni wazazi wa wazazi wetu! Yani umezaliwa kwenye Lindi la umaskini umejikongoja kuweka mazingira sawa ya kuingiza kipato ila Kila ukijaribu kutuna kihela wanunue tofali zinapigwa juu kwa juu tena na baba mzazi wako.mpaka unajiuliza hivi huyu ni mzazi kweli au Mimi ndio mzazi! Kweli Africa tuna laana.
Changamoto sana. Anza na wanao wajengee msingi mpya wa fikra za kimaendeleo wewe ukiwa msimamizi wao ukiwa hai.
 
Mkuu, hoja zako ni nzuri sana lakini mimi ninaamini katika kubadili mitazamo ya watu.

Watoto wako wanapaswa kufanana na wewe, sidhani kama unaweza kuwa na watoto wanne na kati yao wote wakawa wajinga/vilaza na wakajaa ukurutu vichwani. Na tunaposema biashara ya familia nzima hatumaanishi familia nzima inakuwa katika uongozi, wengine wanakuwa waajiriwa tu katika huo mradi.

Ni kwasababu sisi waafrika hasa watanzania maana hawa ndio ninawajua zaidi ni wabinafsi sana ndio maana hata ukitaka kuanzisha wazo la mradi wa familia utapingwa sana na wale ambao ndio wenye uwezo mkubwa kwenye familia. Ni kwasababu tunaona sisi tumemaliza na hao ndugu maskini tutaendelea kuwatupia vihela pale watakapohitaji. Ila swali la msingi ni tutawasaidia hadi lini?

Nina rafiki ambaye kwenye familia yake(kwao) yeye pekee ndio mwenye pesa nyingi, ndugu zake wote ni njaa kali na mara kwa mara yeye ndio kimbilio. Sasa huwa namuuliza utawapa misaada midogo midogo ndugu zako hadi lini? Kwanini usianzishe biashara ambayo utaisimamia na ukawaajiri ndugu zako wasio na kazi humo na watoto wao, ukianguka leo watamkimbilia nani?

Kwahiyo ni kubadili mtazamo tu, hata hao wahindi kama akina MO sio wote kwenye familia wenye akili ya biashara, ndio maana MO ndio yupo mbele wengine huwasikii sana lakini huwezi kuwakuta na bahasha za kaki wakipeleka CV zako zikaguliwe.
Umenyoosha maelezo
 
Ili kuvunja poverty circle tuliyo nayo ni muda sasa kuanzisha na kuzingatia miradi au biashara za kifamilia.

Tujifunze kwa hawa ndugu zetu watu weupe.

Tusione ufahari mradi, kilimo au biashara kufahamiwa na mtu mmoja tu kwenye familia akifa yeye na yenyewe inakufa naye unabaki mgogoro wa mali kila mtu akitaka chake.

Dunia sasa inabadilika ni vyema nasi kubadilika wanafamilia na wazazi wasione sifa kuwa fichia white watoto wao na kuwafukuza ili wakabangaize hovyo kwenye umasikini kwa kuanza kwenye zero.

Ni muda sasa ujuzi kuanza kuamishiana tukiwa hai iwe ujuzi wa biashara, kilimo, kazi nyingine yoyote kutoka kwa baba/mama kwenda kwa mtoto naye anafanya hivyo kwa watoto wake nao wanafanya hivyo kwa watoto wao inakuwa muendelezo.

Kupambana sasa na umasikini inabidi tulinde hata kile kidogo tulicho nacho na kukikuza ili kiongezeke ukubwa.

Tusione mila na tamaduni za wahindi na waarabu kuhusu mali ni za hovyo bali tione ni bora kabisa kuigwa katika kuvunja umasikini unao tuzunguka.

Tuamke sasa.
Hoja yako ni nzuri mno , lakini wabongo wengi wanapenda kutukuzwa , yaani wengi wanataka wawe juu ili waabudiwe na ndugu zao
 
Tuna hitaji elimu kubwa katika hili kuanzia chini kabisa. Hakiwezekani Watanzania wenzetu wa races hizo wanafanya vyema katika hili na kuvunja circle of poverty katika jamii yao Ila sisi hatutaki hiki kitu.
Wala SI elimu kubwa Bali Shamba/duka/garage kubwa la familia na kila mwanafamilia kuchangia iwe nguvu kazi au finance.
 
Hoja yako ni nzuri mno , lakini wabongo wengi wanapenda kutukuzwa , yaani wengi wanataka wawe juu ili waabudiwe na ndugu zao
Na hilo ndio tatizo ambalo Baba na Mama yake ni ubinafsi. Ukifanikiwa kutoa elimu wakaacha ubinafsi, kazi inakuwa rahisi sana.

Kuna familia zina vituko sana, yani unakuta kuna mmoja ni tajiri kweli ila mtoto wa shangazi yake ameshindwa kuendelea na shule kwasababu ya hali ngumu nyumbani na anafanya kazi ya ndani huko Dar. Hiki sio kichaa?
 
kwenye familia nyingi zakiafrika kama ni baba au mama ndie breadwinner akishafariki tu mali zote zinaisha na familia iliyobakia nyuma utajiri wao wote unatoweka kwasababu behind utajiri wote wafamilia kuna makafara,masharti na ndagu zakutosha ambozo mzazi amejifunga navyo nasio rahisi kuweka wazi mchongo wakishirikina kwa watoto wake au kizazi chake kijacho hivyo akifariki tu anaondoka na utajiri wote wafamilia
 
Muhimu watoto na familia kwa ujumla kuwajuza shughuli tunazo fanya A-Z.

Lazima tusafirishe ujuzi tukiwa hai, hii haipaswi kuwa hiari bali lazima tunapaswa kuvunja circle of poverty kwenye jamii yetu kwa nguvu kwa kupenda au hata kwa kutokupenda.
Binafsi mimi najenga nyumba idadi ya watoto wangu ...Na labda nipate misukosuko ila naset mambo waishi kama peponi ...Naomba Mungu anipe ujuzi kipata zaidi.
 
Back
Top Bottom