Ili kuvunja circle ya umasikini tuliyo nayo watu weusi ni muda sasa tuzingatie "FAMILY BUSINESS"

Changamoto sana. Anza na wanao wajengee msingi mpya wa fikra za kimaendeleo wewe ukiwa msimamizi wao ukiwa hai.
 
Umenyoosha maelezo
 
Hoja yako ni nzuri mno , lakini wabongo wengi wanapenda kutukuzwa , yaani wengi wanataka wawe juu ili waabudiwe na ndugu zao
 
Tuna hitaji elimu kubwa katika hili kuanzia chini kabisa. Hakiwezekani Watanzania wenzetu wa races hizo wanafanya vyema katika hili na kuvunja circle of poverty katika jamii yao Ila sisi hatutaki hiki kitu.
Wala SI elimu kubwa Bali Shamba/duka/garage kubwa la familia na kila mwanafamilia kuchangia iwe nguvu kazi au finance.
 
Hoja yako ni nzuri mno , lakini wabongo wengi wanapenda kutukuzwa , yaani wengi wanataka wawe juu ili waabudiwe na ndugu zao
Na hilo ndio tatizo ambalo Baba na Mama yake ni ubinafsi. Ukifanikiwa kutoa elimu wakaacha ubinafsi, kazi inakuwa rahisi sana.

Kuna familia zina vituko sana, yani unakuta kuna mmoja ni tajiri kweli ila mtoto wa shangazi yake ameshindwa kuendelea na shule kwasababu ya hali ngumu nyumbani na anafanya kazi ya ndani huko Dar. Hiki sio kichaa?
 
kwenye familia nyingi zakiafrika kama ni baba au mama ndie breadwinner akishafariki tu mali zote zinaisha na familia iliyobakia nyuma utajiri wao wote unatoweka kwasababu behind utajiri wote wafamilia kuna makafara,masharti na ndagu zakutosha ambozo mzazi amejifunga navyo nasio rahisi kuweka wazi mchongo wakishirikina kwa watoto wake au kizazi chake kijacho hivyo akifariki tu anaondoka na utajiri wote wafamilia
 
Muhimu watoto na familia kwa ujumla kuwajuza shughuli tunazo fanya A-Z.

Lazima tusafirishe ujuzi tukiwa hai, hii haipaswi kuwa hiari bali lazima tunapaswa kuvunja circle of poverty kwenye jamii yetu kwa nguvu kwa kupenda au hata kwa kutokupenda.
Binafsi mimi najenga nyumba idadi ya watoto wangu ...Na labda nipate misukosuko ila naset mambo waishi kama peponi ...Naomba Mungu anipe ujuzi kipata zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…