Ili uchumi ukue, tukubali Rais aongezewe muda hata miaka 20 Ili amalizie miradi yake yote

ili amalizie miradi aliyoianzisha akae miaka 20 madarakani.
Naunga mkono
Ila kazi ina pressure sana
Tuombe tufike uchumi wa kati ili mishahara iwe inapanda kwa wafanyakazi kabla ya kupanda kwa bidhaa
Tatizo letu akiondoka mmoja na miradi inakufa kwa hiyo awe wa maisha tu
 
Kabla yake Nchi ilikuwepo, kuna siku mimi, wewe na yeye hatutakuwepo.

Tunatakiwa tuwe na mkakati wa kitaifa,ambao utabeba vipaumbele vyetu kama Nchi. Yeyote atakayekuwa Rais, awe na jukumu la kuviendeleza na kutimiza kabla hayaleta vipaumbele vyake.

Hata tukiamua aongoze milele, kunasiku tu hatakuwepo au atazeeka, je ndio utakuwa mwisho wa maendeleo ya Nchi yetu?
 
Tufanye kama China, au Russia, aendelee ajenge uchumi wa viwanda tuwe nchi ya uchumi wa kati na pia ajenge Taasisi imara za kuendesha na kuisimamia nchi. Viva JPM viva Tanzania.
 
Hapa leo tuelewane , Maana hata kwenye kupinga hua tunakua pamoja.
Tunahitaji Rais Akae Miaka 20 ili tuweze kupiga hatua ya kweli.
Miradi yenyewe ni kumalizia miundomsingi na miundombinu yote kama reli ya kisasa SGR, Miradi mikubwa ya Bara Bara inayoendelea nchi nzima, Bwawa hilo kubwa la kuzalisha umeme.
Akikaa na Akatulia Akamaliza kila kitu Alichoanzisha Basi nchi itakua imefika mbali na tutaziacha nchi nyingi za Afrika kimaendeleo.
Wasi Wasi wangu akiingia Rais mwingine ataharibu trend ya Miradi na tutajikuta kila alichoanzisha Rais Magufuli kinasimama na tutaishia hapo hivo tumuunge mkono akae Miaka hiyo 20 ili amalize kila kitu ndio astafu hapo itakua safi tu.
Ni kweli mkuu, wasiwasi huo ulio huainisha "labda akiingia raisi mwingne anaweza akahalibu trend...."
Ni wa msingi sana, hivyo tunatakiwa kutafuta namna ya kuzui Hilo
Wewe umetoa hoja kuwa raisi wa Sasa aongezewe muda ikiwezekana hata 20+ years.... Je ikitokea Mwenyenzi Mungu akamuita mapema zaidi/yaaani mapema zaidi, maaana na yeyeni binadamu tu Kama sisi kikombe hicho hakikwepeki. .....

Mi nadhani tulikuwa Kuna haja ya kuwa na vipaumbele na dira ya maendeleo ya taifa iliyo katika mipango madhubuti ya muda mfupi, wakati na muda mrefu... Na dira hiri itambulike kikatiba na KATIBA ilindwe na taasisi huru ya muhimili wa mahakama... Hii itasaidia hata raisi akiishia miaka 5 au jini ya hapo/akifa bado Kama taifa muelekeo na dira yetu isikwame.....
 
Hata wenzake walianzisha miradi hawakumaliza amekuja kuimalizia yeye hata yeye watamalizia wengine hiyo buku 7 isiwatoe akili
 
Hapa leo tuelewane , Maana hata kwenye kupinga hua tunakua pamoja.
Tunahitaji Rais Akae Miaka 20 ili tuweze kupiga hatua ya kweli.
Miradi yenyewe ni kumalizia miundomsingi na miundombinu yote kama reli ya kisasa SGR, Miradi mikubwa ya Bara Bara inayoendelea nchi nzima, Bwawa hilo kubwa la kuzalisha umeme.
Akikaa na Akatulia Akamaliza kila kitu Alichoanzisha Basi nchi itakua imefika mbali na tutaziacha nchi nyingi za Afrika kimaendeleo.
Wasi Wasi wangu akiingia Rais mwingine ataharibu trend ya Miradi na tutajikuta kila alichoanzisha Rais Magufuli kinasimama na tutaishia hapo hivo tumuunge mkono akae Miaka hiyo 20 ili amalize kila kitu ndio astafu hapo itakua safi tu.
Naunga mkono hoja 100%
 
Naona magufuri unajianzishia thread na kujijibu mwenyewe.

Tulia tu tutajadili vizuri kwenye kura za maoni hapo mwakani.
 
Hapa leo tuelewane , Maana hata kwenye kupinga hua tunakua pamoja.
Tunahitaji Rais Akae Miaka 20 ili tuweze kupiga hatua ya kweli.
Miradi yenyewe ni kumalizia miundomsingi na miundombinu yote kama reli ya kisasa SGR, Miradi mikubwa ya Bara Bara inayoendelea nchi nzima, Bwawa hilo kubwa la kuzalisha umeme.
Akikaa na Akatulia Akamaliza kila kitu Alichoanzisha Basi nchi itakua imefika mbali na tutaziacha nchi nyingi za Afrika kimaendeleo.
Wasi Wasi wangu akiingia Rais mwingine ataharibu trend ya Miradi na tutajikuta kila alichoanzisha Rais Magufuli kinasimama na tutaishia hapo hivo tumuunge mkono akae Miaka hiyo 20 ili amalize kila kitu ndio astafu hapo itakua safi tu.
Mkuu jambo la msingi si kukaa miaka mingi madarakani bali ni kutengeneza msingi ambao yeyote atakayekuja ataanzia alipoishia
 
Back
Top Bottom