Ilikuwa ni suala la muda tu, nilijua lazima Harmonize atusue kwenye hii game

Ilikuwa ni suala la muda tu, nilijua lazima Harmonize atusue kwenye hii game

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Kuna watu tumejaliwa vipaji fulani vya kusoma alama za nyakati na kutabiri mambo yajayo. Zaidi ya miaka miwili nimekuwa nikimfuatilia huyu mwanamziki Harmonise tangu ajitoe kwenye label ya WCB. Na kiukweli kabisa matendo yake na attitude yake ilinifanya nione uwezekano mkubwa wa huyu mtu kufanikiwa kwenye hili game.

Hii hata usipoikubali ila ni kwamba, ndani ya miezi 12 iliyopita Harmonise na label yake wameteka karibu 40% ya game ya bongo fleva ukianzia na miziki mizuri na pia public attention kwenye social media.

Huyu jamaa nimegundua ana attitude na work ethics ambazo ni ngumu sana kuzipata hata kwa watu wa kawaida, mbali na hizi skendo za mapenzi ambazo zilitmtokea mwaka jana ila ameweza ku move on bila kuathiri mziki wake, hiyo kitu mi kwangu imenionesha kwamba huyu mtu ana strong and positive attitude ya hali ya juu sana.

Huyu jamaa anafanya matukio na vitimbi vingi lakini hasau kuhusu mziki. Hiyyo ni advantage kubwa sana. Ni kama vile hajali chochote kuhusu opinion za watu, kitu ambacho ni nadra sana kukipata kwa wasanii.

Mwaka mmoja uliopita niliandika uzi nikimuonya mwanamziki Rayvanny ambaye mimi namuona ni mwanamziki mwenye talanta kubwa sana pengine sawa hata kumzidi Harmonise. Nilimuonya Rayvanny aingie studie afanye kazi ya mziki na asijihusishe kwenye skendo za mapenzi kwa sababu yeye bado ni muajiriwa wa WCB wakati mwenzake Harmonise anamiliki label yake na matokeo tunayaona <<Rayvanny angalia muziki wako usife maskini. Mwenzako Harmonize ana lebo tayari>> nasikitika Rayvanny hakufuata ushauri wangu. Maana miezi 12 iliyopita, sijaona chochote alichofanya Rayvanny kwenye muziki to be honest.

Halafu kitu kingine huyu Harmonise ukimsikiliza akiongea, yaani kuna kitu fulani lazima u notice ana moyo wa huruma sana na jamaa yupo humble kitu ambacho pia kinatakiwa sana ili kufika mbali. Na kingine ni mtu wa kujichanganya na watu, japo mimi binafsi sijawahi kumuona huyu mtu kwa macho ila ukifuatilia tu akiongea kwenye social media, unajua tu.. Yaani hii dunia mtu kama ni mkora akiongea utajua tu.. Na mtu kama ni mwema akiongea utajua tu. Na mtu mwema, Mungu huwa hamtupi aisee.

Angalia tu alivomuinua yule binti mlemavu akamfanya kuwa msanii wa kueleweka, hizo ni thawabu sana. Kubali ukatae, ndo mana mi bado nazidi kuona mafanikio ya huyu mtu bado yatakuwa makubwa sana mwaka mmoja unaokuja.

Ni maoni tu. Matusi ruksa. Kama nimewakera njooni mniuwe.
 
FB_IMG_16557124556012914.jpg
 
Pole mtoa mada. Kama alikutuma mwambie JF hakuna Ndorobo. 😂😂😂😂😂
 
Kwa sasa huwrzi kupita sehemu za starehe au redioni na tv usione au kusikia wimbo wowote wa harmo au usiposikia nyimbo zake basi utamskia yeye..harmo ameshawaoiga gepu pakubwa sana haters wake hasa chawa wa usafini.

Saivi watoto wadogo hawa ukiuliza msanii wanayemkubali kwa haraka haraka watakwambia harmonize.

Kiufupi kizazi cha diamond kinapita taratibu
Wakati huu rayvany ametoa nyimbo majuzi lakini ni kama vile hakuna kitu..

Ngoja harmo atoe sasa goma uone.
 
Back
Top Bottom