Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Ila wizo unazingua ujue πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Na wewe ungemsonkola vidole vya macho aache ujinga.
Wizo umefunguliwa kutoka gerezani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Umenikumbusha mshikaji wangu Lumi. Tumevuka maji toka Kigamboni kumpokea demu katoka Bagamoyo hakuwani kumuona. Si akamkimbia baada ya kumuona kwa mbali. Eti sura haikuwa kama kwenye picha, kademu kembambaaa halafu kamepiga mkorogo hatari
πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wizo umefunguliwa kutoka gerezani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Nimefunguliwa wizo
 
Hapana siwezi fikia huko naiogopa dhambi sitaki kuzidi kumtesa Yesu msalabani kwa dhambi zangu.
Wee ngadu umeanza lini kuhubiri neno?? Mbona hatari hii jirani?!! Nimerudi na watu wameokoka?? Kwema?
 
Mwaka 2011 nikiwa nafanya kazi Njombe nikaongea na rafiki yangu anisaidie ku- process cheti cha kuzaliwa Cha mtoto niliyezaa na binti 1. Huyo rafiki yangu akaamua kumpa dada mmoja hiyo kazi akampa na namba yangu ya simu ili niwe nampa details na mambo mengine in case. Basi bana binti ndiye alianza kunipigia, mara ya kwanza sauti nzuri kweli, laini na nyororo. Siku zikaenda nikamtongoza akakubali, baadae akanambia ameolewa lakini mume wake amemtelekeza ameoa mke mwingine, anaishi kwenye nyumba ya huyo mme wake. Tulikuwa tunaongea kila siku usiku hadi mida ya saa saba, tunaagana ili nipimzike niamkie kibaruani. Nikaenda likizo kijijini kwetu, yeye alikuwa Bunda mjini, siku moja nikamwambia nakuja Bunda ninashida Musoma hivyo naomba tukutane Bunda stand. Nilikuwa wa kwanza kufika nikampigia simu akanambia ngoja achukue boda aje, nikawa alert kuona nani atanipigia simu, dakika 5 mbele boda inaingia ikiwa na mdada,akamlipa ajanipigia, hahaha! Sauti na muonekano tofauti kabisaa, tulikaa kama dakika 5 nikamwambia ngoja nifike Musoma nitakucheki wakati narudi. Jioni akaniuliza vp, nikamwambia nimekwama. (Musoma nilikuwa naenda kwa mchumba wangu ambaye ndiye mke wangu kwa sasa). Sikumtafuta tena, baadae rafiki yangu ajanipigia akinambia mme wa yule dada alituona wakati niko nae hapo stand ya mabus! Sikuwahi tena kujihangaisha na huyo dada
 
Pole sana kijana. Wewe ni mtu mwenye nyota ya punda. Nenda ukasafishe nyota. Ulikataliwa kikatili sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…