Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Moja ya vitu sipendi basi ni kukonda aisee.
Ukikonda kwa njaa unaonekana tu.

Nimeishi Mbeya, Iringa, Shinyanga, Tanga na Dsm. Kati ya mikoa yote hiyo Dsm ndo inaongoza kwa vijana kukonda kwa lishe duni.
Unamkuta mwanachuo kapendeza ila sura haina nuru, mwili umekongoroka mno, tumbo limeingia ndani mpaka imekua kama ana kibiyongo.

Mavazi ni muhimu ila wanachuo mzingatie chakula sio kuwaza mavazi tu.
Duh aisee 😂
 
Mimi nilikutana na mtoto mmoja wa kipemba fesibuku. Tuka panga tukutane laivu bila chenga. Ile kukutana nae kumbe mama kijacho mimba ya miezi 6.
 
Unaeza ukawa unasoma huu uzi ukashangaa kujikuta unasimuliwa humu😂
 
Alinambia "kumbe una komwe mchongoko kiasi hicho mahi wangu, mbona kwenye picha halionekani au ulilipeleka likizo".

Nikalia, nikabubujikwa machozii mimi. Chozi moja la jicho la kushoto likashuka likadondoka na kugonga mabuti yangu ya kimgambo. Akanisonkola na kidole kwenye kichwa huku akinifyonyaa....

Nililia, nilimwaga machozi pipa tatu, nikazimiaa nikajikuta nimelazwa wodi ya wagonjwa wenye upungufu wa maji mwilini chini ya usimamizi wa DR Mambo Jambo

Extrovert Poor Brain mshamba_hachekwi
Ila wizo unazingua ujue 😂😂😂😂
Na wewe ungemsonkola vidole vya macho aache ujinga.
 
Back
Top Bottom