Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Mimi nilipokutana nae kama aliniona wa kuja sijui, ila haku react alikuwa humble sana. Binfsi nilivyomdhania haikuwa hivyo.
Alkuwa mzuri na myenyekevu sana, naami hakuwa anaigiza ila ndio uhalisia wake, ilikuwa siku ya furaha kwangu kiasi sijaweza kuisahau.

Abarikiwe tu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ety chini ya usimamizi wa dr mambo jambo..

Mi nikajua ulikua under mzizi mkavu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Bwana bwana , huyu alieleta mambo ya kuedit mapicha na mafilter kwa ujumla hakuwa na nia njema kabisa.

Hizi tamaa acha tu, nishawai ingia dating site moja huko nikaiimbisha Manzi ikaja Wasap Inbox huko ikatuma mapicha weee, bwana wee nikajisemea mtoto si ndiyo huyuu sasa na kwa jinsi alivyo basi nitamtuliza na kumfanya bibie wangu permanent na nitaacha kupapalika na mamanzi wengine[emoji3].

Toto toto kweli, jiuso zurii, ilo lirangi sasa[emoji3], shape fulani hivi isiyoumiza macho wala kukera watizamaji, kiufupi Toto HD Utra.

Basi bwana, nikaliimbisha toto tukakubaliana kutoka date, siku ilipofika muhuni niliipania siku nzima maandalizi ya kutosha sana nikijua nakwenda kumpokea mwali wangu ambaye kila mwanaume fisi hiyo ni ndoto kuwa na mpenzi wa sifa hizo.

Niishie kwa kusikitika tu, niliyoyakuta si yale niliyoyatarajia wala niliyoyaona katika picha na video zake.

Kiufupi walikuwa watu wawili tofauti kabisa isingelikuwa ile tabia ya kuongea nae kwa Voice call basi ningehitimisha kuwa yule mrembo wangu si huyo kigagura niliyeonana nae[emoji3][emoji3].

Serikali ingilieni kati haya mambo wanaume tunadanganywa sana.
 
filter ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…