Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Kuna aliyeniambia hatuendani kutokana na kazi yangu wakati huo, nikaona isiwe tabu nikapiga kimya. Baadaye ananitafuta baada ya kugundua nimepiga hatua. Nikaweka big no!

Kuna mwingine kwa style hiyo hiyo, hadi kuniambia ana mimba yangu, ila katika kuchanganua nikandua ni uongo. Nikamwambia aendelee na maisha yake. Alikuja kuniomba msamaha ila ikawa tabu kurudi reverse.

Mambo yalikuwa mengi sana mtandaoni.

Kuachana na mapenzi, mali zangu zote nilizonazo ikiwemo kazi yangu nimezipatia mtandaoni.

Hata utafiti huwa ninafanyia mtandaoni.
 
"Samahani sana ninavyokuona sio kama nilivyotegemea, HATUENDANI"... baada ya kusema hivyo jamaa aliyekuwa naye kwenye Toyota Hiace nyeupe akaniangalia na kutabasamu kisha akaondoa gari. Mimi nikaachwa nimesimama. Kubaya zaidi hata kwenye gari hakushuka. Sikuweza kujua yule kijana alikuwa nani yake hadi leo. Ilitokea Arusha maeneo ya Njiro nje tu ya Njiro Complex (Bugaluu).

Mwaka 2007 kupitia mtandao wa marafiki.com niliweza kupata mchuchu mwenye asili ya kiasia na kuanza kuchat naye. Chats zilikuwa nzuri sana za kuvutia utadhani tumejuana kitambo sana. Siku tunakutana kwa mara ya kwanza nje ya Njiro Complex ndo akakata tamaa na kunijibu kama nilivyoandika kwenye aya ya kwanza. Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwenye haya maisha yangu. Bahati nzuri hakukuwa na mtu niliyeenda naye eneo la tukio kwahiyo aibu ilikuwa ni yangu binafsi.

Ila sikumchukia wala kumlaumu yule binti wa kishua kwa sababu kwa wakati ule kweli nilikuwa nimepigika haswa. Yaani nilikuwa mwembamba ila ule wembamba wa lishe duni. Kiufupi nilikuwa nimekonda. Kama unavyojua mtu mwenye njaa ndo mwenye sura mbaya kwahiyo hata mimi nilikuwa mtu mwenye sura mbaya sana kwa hisani ya NJAA. Zilikuwa nyakati ambazo kutembea kwa mguu kutoka Mianzini hadi Mbauda ni kitu cha kawaida sana. Au wakati mwingine Clock Tower - Njiro ilikuwa jambo dogo. Akitembea tajiri huwa ni matembezi ya hisani ila mimi sijui ilikuwa matembezi ya kuchochea umaskini?

Nakumbuka mwaka 2010 ndo nilipata matumaini makubwa sana baada ya manzi mmoja wa Chalinze kuniambia mimi ni handsome. Huyo manzi nilikutana naye nilipokuwa natoka Iringa kuchukua cheti cha form six.

Kimsingi baada ya tukio la 2007 nikaanza kuogopa sana kutongoza demu mtandaoni. Hadi leo nikiona manzi mtandaoni huwa hadi nifuatilie sana kumjua kiasi na sio kukurupuka.
Daaah,

Kila nikikumbuka nacheka sana
 
Kuna aliyeniambia hatuendani kutokana na kazi yangu wakati huo, nikaona isiwe tabu nikapiga kimya. Baadaye ananitafuta baada ya kugundua nimepiga hatua. Nikaweka big no!

Kuna mwingine kwa style hiyo hiyo, hadi kuniambia ana mimba yangu, ila katika kuchanganua nikandua ni uongo. Nikamwambia aendelee na maisha yake. Alikuja kuniomba msamaha ila ikawa tabu kurudi reverse.

Mambo yalikuwa mengi sana mtandaoni.

Kuachana na mapenzi, mali zangu zote nilizonazo ikiwemo kazi yangu nimezipatia mtandaoni.

Hata utafiti huwa ninafanyia mtandaoni.
Mtandao ndo mpango mzima ukijua kucheza nao.
 
hoja yake hapa ni jinsi ya kukutana kwa mara ya kwanza na kutodhania jinsi alivyomtegemea.

picha za mtandao zinadanganya; filter,editting na photoshop kibao.. ni lazima wakikutana wakimbiane tu.

ndo nikahoji kwanini wasiwafuate huku mtaani ambapo ndo kuna uhalisia zaidi?
Yeah sure hapo nimekuelewa mkuu
 
Mkuu unataka kuniambia demu anayekaa masaki ndio huyohuyo unayekaa naye hapo chalinze ndanindani? Unatania aisee!
demu anayekaa Masaki ni mrembo kulingana na nguo na vipodozi anavyotumia.

demu anayekaa Chalinze ndani ndani ni Mzuri wa asili.

kwani huyo demu anayekaa Masaki anazaliwa na Malaika au Eliens?
 
Mbona unakuta mtu ana acha mademu wa mtaan kwake kisha anaenda tongoza mademu wa mitàa mingine
uko napo ni mtaani pia.

nilimaanisha kuwa ili kuepukana na hiyo changamoto aliyokutana nao ni bora akafuata wanawake anaokutana nao kwenye mazingira anamoishi. eg. kazini, shuleni, nyumba za ibada, sehemu za starehe, gym etc..

uko atakutana na wanawake ambao hawajiedit kwa kupitia picha za camera.
 
Back
Top Bottom