Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Ngoja ninywe maji kidogo. Nitarudi!
 
Nani anajifanya mwanadiplomasia ambaye amewahi kukupiga ???
Usihangaike na watu ambao hawataki kuelewa rejea kwenye maandiko ya Plato baba wa falsafa kutoka ugiriki "myth of the cave" utaelewa kwanini watu wanakuja na mihemko nikwa sababu Watanzania wengi wanaishi kwenye ndani ya pango lenye giza na hawataki kutoka na ukajaribu kuwatoa wanaweza kukutoa roho please note my words. Uongozi uliopita ilijaza watu ujinga sana
 
Unamaanisha kushirikiana kama 50/50 au maendeleo ya kisayansi au kushirikiana ambapo tanzania inapewa misaada na nchi ya kigeni inashikilia rasilimali zetu 100%
Ninavyosema mahusiano baina ya nchi (International Relations) nazungumzia vitu zaidi ya uwekezaji wa 50/50, zaidi ya sayansi na teknolojia, zaidi ya misaada. Hapa sasa kwenye mahusiano ya kimataifa (International Relations) ndiyo kinakuja kitu muhumu kabisa kiitwacho Diplomasia (Diplomacy): Mahusiano ya kimataifa (International Relations) na Diplomasia (Diplomacy) ni dhana mbili tofauti kabisa, japo huwezi kuzitenga.

Sasa ili ufanikishe mahusiano ya kimataifa (International Relations) ili uweze kupata hizo 50/50, teknolojia, ulinzi au hata misaada ni lazima uwe na chombo kiitwacho Diplomasia (Diplomacy). Lakini ili hichi chombo kiitwacho diplomasia kiweze kufanya kazi vizuri katika kujenga, kufanikisha na kuimarisha mahusiano ya kimataifa (International Relations) ni lazima nchi husika itengeneze kitu kiitwacho Sera ya Mambo ya Nje (Foreign Policy).

Sasa basi ili kuelewa nini kilifanyika hapa Tanzania ni lazima ufahamu mambo niliyoyataja hapo juu:
1. Mahusiano ya kimataifa (A State of International Relations).
2. Dhana ya neno diplomasia (A Concept of Diplomacy).
3. Sera ya mambo ya nje ya Tanzania (Tanzania's Foreign Policy).

Sisi ili kupima mafanikio ya mtu huwa tunaangalia haya mambo matatu ambayo huingiliana. Ulinzi, Rasilimali, Uwekezaji, haki za binadam, soko ya kimataifa, na Misaada ni sehemu ndogo sana ambazo zinaingia kwenye haya mambo makuu matatu. Bahati mbaya sana sasa, vijana wengi wa kitanzania ambao kazi yao ni kusifia na kuunga mkono kila kitu hawana uelewa wowote ule katika hili.

Ndiyo maana huishia kusema tunachuki na marehemu lakini ukweli wenyewe ndiyo huu ambao wengi wao hawataki kuukubali.
 
My Maaan, my maaan!
Thanks for bringing allegory of the cave.......
 
Populism ipo lakini haitakiwi ivuke mipaka na kuathiri sera ya mambo ya nje na diplomasia ya nchi. Ukisoma sana Diplomasia utakutana na kitu kinaitwa COMPARTMENTALIZATION OF FOREIGN POLICY AND NATIONAL DIPLOMACY. Kwamba utakuwa na ujinga wako ndani ya nchi au utakuwa na uadui na taifa fulani, lakini lazima mshirikiane nalo kwenye mambo muhimu.

Sasa mtu usipofahamu jinsi mfumo wa dunia unafanya kazi unaweza kuyapeleka yale ya ndani ya nchi nje ya mipaka yako na yakakuletea madhara. Hili ndilo liliiukuta Tanzania yetu, tumepata madhara makubwa. Hebu angalia hapa:

1. Uchina na Marekani ni maadui wakubwa - Lakini ndiyo mataifa yenye mahusiano makubwa kibiashara.
2. Uchina na Japan ni maadui wakubwa - Lakini wanahusiana sana kwenye ulinzi na usalama wa Pasifiki.
3. Uchina na Australia wameanza kuwa maadui- Lakini biashara ya Real Estate Uchina ina mkono wa Australia.
4. Urusi na Marekani ni maadui - Lakini wanashirikiana sana kwenye teknolojia na usalama wa Mashariki ya Kati.
5. Urusi na Ukraine ni maadui - Lakini juzi Ukraine wameomba kuuziwa gesi na Urusi baada ya uhaba kutokea Ulaya.

Hujiulizi kwanini haya mataifa makubwa hayasusi au kuzira kama mataifa ya kiafrika, huku mkijivuna kwamba sisi ni matajiri na tunajenga kwa pesa za ndani. Mara hatuwahitaji hawa wanyonyaji, tunaweza kufanya wenyewe. Hizi kauli hata mtu binafsi huwezi kuzisema kwa jirani zako. Lakini watanzania wakaingia mkenge, ona leo sasa.......
 
Ushirikiano wa kutuletea Symbion na Aggreko na kutukamua na capacity charge halafu wao wanakuletea vyandarua vya msaada gharama zake ni sawa na pesa ya siku moja wanayotukamua kwenye capacity charge.
Tumia akiri Sasa kukwepana nao siyo kuwakimbia. Kuwakimbia bila strategy u akuwa kama digidigi tu na unaua wananchi wako. Hivi unajua kuwa Kuna watanzania wanaona Bora kutawaliwa na mzungu kiliko mwafrika?
 
Umefunga mjadala.
 
Watu wenye akili timamu Tanzania?

Labda wenzetu walikuwa wagonjwa hatujui?

Wapo wengine hadi leo hawataki Mama asafiri na akisafiri ni matusi tu mwanzo mwisho
Hapa Tanzania wananchi na viongozi wenye akili timamu wapo wachacheee mnoooooo yaani mnoooo, inawezekana kwenye hili taifa zima la watu wapatao milion 55+ watu wenye akili timamu hawafiki 200.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hapa Tanzania wananchi na viongozi wenye akili timamu wapo wachacheee mnoooooo yaani mnoooo, inawezekana kwenye hili taifa zima la watu wapatao milion 55+ watu wenye akili timamu hawafiki 200.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Aiseee umetutukana mno..Hebu tutake radhi watanzania!!
🤣 🤣 🤣 🤣
 
MALCOM LUMUMBA
 
Usianze kuleta habari za homework hapa! Hizo wape wanao hapo nyumbani kwako.

Mimi nataka uniambie ni wapi alisema hashirikiani na dunia na kwa vipi?
 
Ukiwajazaje watu ujinga?
 
Kichwa cha mada yake tu ni upotoshaji. Umemjibu vizuri sana.Yaani wao wanaamini kushirikiana na dunia ni kuwapa madini na kupokea neti na Condoms. Ukisema hapana nataka niuze madini mwenyewe na niende dukani kununua neti mwenyewe tayari unakua hutaki kushiriki na dunia.Hili jukwaa Kuna muda watu wanaoonekana wana akili TIMAMU huwa wanapost vitu vya ovyo sana.
 
Hivi ni wapi jpm alikataa kushirikiana na dunia?

Alikatakaa kushirikiana kwenye nini hasa.?

Tupe mfano wa wapi alisema mimi sitaki ushirika na mtu kwenye hili na lile! Hebu taja.
Hahahahhah mkuu huyu jamaa kaandika vitu vya ovyo kabisa. Yaani Magufuli kukataa Lockdown basi hataki kushirikiana na dunia.
 
Anakera sana hapo ukimuuliza akitajie wanadiplomasia hasa anaona wanafaa hapa Tanznlania utasikia January, Nape, Membe wapiga porojo tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ni mshamba tuu wa wazungu.. kwako kuona rais anasafiri nje ya nchi ndio sera ya mambo ya nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…