Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Wewe mwenye akili timamu unaweza ukathibitisha kuwa tulikuwa hatushirikiani na dunia na tulikuwa tumejitenga? Mabalozi wetu walirudi? Tulikuwa hatupokei misaada na mikopo toka nje ya nchi? Au watu WAJINGA kama wewe mnaamini kuwa na mahusiano ni mpaka Rais awe anasafiri Ulaya? Ushamba utawaisha lini?
 
Je tanzania ni nchi maskini au raia wake ndio maskini ?
 
Unaniita mpumbavu halafu unataka niendelee kuzungumza na wewe ???
Mkuu hii thread kuanzia kichwa tu umeandika upuuz. Hakuna sehemu Magufuli hakutaka kushirikiana na dunia. Swala ni maslai ya Tz mbele.Kuanza kufumua mikataba ya ovyo tayari ni kukataa kushirikiana na dunia?Kukataa Lockdown au Chanjo tayari hataki kushirikiana na dunia?
 
Kwa sababu waliona miaka 10ya kupishana angani iliwapelekea kwenye migao ya umeme na maji ndio wakaamuam kujaribu strategy mbadala.
Japo kila mtu na maoni yake lakini aliyepo madarakani muda wote huo ni ccm
 
Ushirikiano ni muhimu sana. Lakini ushirikiano kwa namna ulivyo sasa hatutakuja kuendelea kamwe, tutabaki maskini siku zote. WTO wanahimiza soko huria, vikampuni toka nchi maskini vikashindane kwa usawa sokoni na makampuni makubwa ya matajiri. Hao IMF na WB wanalazimisha nchi zifuate sera za kichumi ambazo zinadumaza maendeleo ya nchi maskini. Sera ambazo nchi tajiri hazikuzitumia kujipatia maendeleo.

Hata nchi tajiri zenyewe mambo yakiziendea kombo zinaachana na makubaliano ya kimataifa. US kuipiga pin Huawei ni mfano mmoja wapo. Ushirikiano ni muhimu lakini kwa namna uliopo hautufai.
 
Nakumbuka mwaka 2018 nilivyoandika kuhusu vijana wa Magufuli aina ya Makonda na Sabaya kwamba watamponza Magufuli, bwana MISULI uliniambia mimi naunga mkono mashoga na mpuuzi. Hivi bado tu umepungukiwa na busara wala hutaki kujifunza kwamba kuna kitu umepungukiwa katika mtazamo na mwono wako kimaisha na kisiasa ???
 
Hivi ni nani aliyekwambia kwamba Diplomasia ya nchi inafanywa na mabalozi peke yake ???

Balozi ni kitaalamu ni Diplomatic Agent/Legate/Envoy yeye hufanya kazi kama wakala au muwakilishi wa nchi na sera zake. Wao hawafanyi kazi nje ya TOR ambazo hupewa baada ya teuzi na kutumwa nje ya nchi. Sasa kama unafikiri mabalozi ndiyo wanaendesha diplomasia ya nchi au lazima mtua aende nje ya nchi ili awe mwana diplomasia, UMECHELEWA BASI (You've missed a bus) mkuu.

Nadhani sasa kuna haja turudishe ule utaratubu wa zamani vijana wote wa UVCCM, Viongozi wa umma, TISS na JWTZ na makada wengine wa UVCCM lazima tuwapeleke Kurasini kinguvu au wasome vyuo vya itikadi kwa lazima: Hiki kiwango chenu cha ujinga is beyond ordinary comprehension. Yaani wewe SWEETTABLET nilikuwa nakuona walau ziko kichwani kumbe na wewe ni mweupe hivi ??? SMH
 
We ni mshamba tuu wa wazungu.. kwako kuona rais anasafiri nje ya nchi ndio sera ya mambo ya nje
Diplomasia haifanywi na safari za nje, huanzia kwenye Back-Door Channels/Informal Talks hadi kufikia Bilateral au Multilateral Agreement. Lengo kubwa la diplomasia ni utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ya nchi fulani katika kufanikisha mahusiano ya kimataifa. Nadhani hili limekupita kimo ndiyo maana umeshindwa kunielewa vizuri.....
 
Kwahiyo makonda kamponza Magufuli?
 
Unaukumbuka vizuri ule uzi au umeusahau nikukumbushe kwa kuanza kukufafanulia upya ???
Mkuu sema unataka kujipa umuhimu ambao huna.Unachuki na Magufuli hili liko wazi,nimeona hata uzi mmoja huko umetoka kumsiliba.Unachoweza we ni kuonesha chuki dhidi yake lakini sio kuja na hoja zenye kumkosoa.Hii thread iko chini ya kiwango yaani sana na we mwenyewe umeona wachangiaji wengi wanavyokupopoa. Punguza chuki na Magufuli, kwanza hayupo unapambana naye ili ugundue nini?Kibarua mlichonacho cha kumponda Magufuli ni kizito mno. Bora uwe busy na mada zingine tu.
 
Sawa, mkuu. Lakini wewe unaonaje ???
Bashite anaenda jela ua haendi ???
 
Inasikitisha kuwa watu kama mtoa uzi huu wapo wengi tu!! Akili yao haifanyi kazi!! Wanaamini kuwa bila msaada wa wengine hatuwezi chochote! watu waliofilisika kichwani hadi leo wanaabudu ubeberu!!! Pole yao!
 
Hivi unategemea nani akuendeleze dunia ya leo? We ujajua kwamba bila afrika mzungu ni masikini mwafrika akijitambua na kuacha kulialia anaweza kujitegemea hii ndiyo mtizamo wa walioleta uhuru. Misaada haijawahi saidia popote ukienda ulaya tunaitwa omba2 tumalizane hewa ya dunia bure hatuna faida na kuna watawala wanatamani kutufuta kabisa kwenye uso wa dunia. Usiwe unaandika tangazo la kuchosha kwa mtizamo hasi ulionao, jambo hili linataka mjadala wa kitaifa usifikiri kuondoa umasiki ni lelemama!
 
Inasikitisha kuwa watu kama mtoa uzi huu wapo wengi tu!! Akili yao haifanyi kazi!! Wanaamini kuwa bila msaada wa wengine hatuwezi chochote! watu waliofilisika kichwani hadi leo wanaabudu ubeberu!!! Pole yao!
Hakuna taifa lililowahi kuendelea hapa duniani bila kushirikiana na wengine: Kama lipo litaje basi.......
 
Nakubaliana kabisa na wewe, misaada "Foreign Aid" haijawahi kulitoa taifa lolote kwenye umasikini. Kama alivyosema Dambisa Moyo "Aid is Dead". Lakini pia hata mikopo "Foreign Debt" haijawahi kulitoa taifa lolote kwenye umasikini. Kitu ambacho nashangaa ni kwamba Raisi Magufuli hali akilifahamu hili ukopaji wake wa miaka mitano uliwazidi hata watangulizi wake. Hili liko nje ya mada na sitalizungumzia kabisa,....

Hebu tujikite kwenye hoja kuu mezani ambazo ni hizi:
Hivi unadhani Tanzania inaweza kufanikiwa kama taifa bila kushirikiana na mataifa mengine ???
Kwanini tulijiaminisha kwamba kila anayekuja Tanzania ni mtu mwenye nia mbaya na sisi na anataka kutuibia ???

Je, Sera ya mambo ya nje ya Tanzania ilitekelezwa vizuri, kwa kiwango gani ndani ya utawala wa Raisi Magufuli ???
Je, Mambo aliyoyafanya katika utawala wake yamekuwa na madhara gani kiusalama, kisiasa na kiuchumi kwa nchi ??
 
Ulikuwa ujinga wa bwana mmoja akiitwa JPM siku hizo na unafiq wa baadhi ya watu ambao bado wanaongoza nchi leo hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…