Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Mmmmmh! Tulijitenga na dunia lini? Mbona tuliongea na Rwanda na Uganda kuhusu kuonganisha nchi zetu na (SGR). Mbona mkutano wa sadac ulifanyika Tanzania. Mbona balozi zetu hazikufungwa nchi jirani na duniani.Mbona wageni/watalii walifika nchini.Mbona viwanda vya wageni hususani ni waChina vimeongezeka.

Au kuwa karibu na dunia nikujenga bandari ya bagamoyo kwa masharti ya kipumbavu na kubinafsisha Tanesco. Au kusaini bogus treaty

Je umesema kuhusu leagal of nation je kwanini ujerumani aliona ni uboya akawageuka. Nakusuhu UN kwanini Patrice lumumba aliomba jeshi kutoka UN ili kuwaondoa wabelgiji wezi wa shaba congo baadala yake wanajeshi wa UN wakaanza kuwasupport wabelgiji. Huuu ndio uhusiano na dunia? jihusishe na dunia lakini chunga chako kwasababu hakuna wakutupa zaidi ya mungu lazima tuheshimu zawadi hii.

Nasikitika Sana mtoa maada umekuja na kapoint uchwara sijui ka diplomasia sijui naahisi ndo hicho ukijuacho kwenye maendeleo foreign policy hayo ni mambo ya mwisho maendeleo yanaanza ndani tengeneza mazingira ya ndani kwanza. Hizo nchi China na wenzake zimewin sio kwasababu ya blabla unazosema wewe ni kwa kufanya kazi kwa bidii na kutengeneza mazingira ya uwekazaji.
 
View attachment 2014440

Body language, anayeonekana kituko ni yupi?
Diplomacy is a multifaceted phenomenon, it is more than attending international conferences...
Diplomacy is a a tool to project A foreign Policy of a country when she relates with others......

Leo hii hatumuongelei huyu mama, tunamuongelea Raisi wetu mpendwa na jinsi gani sera zake za mambo ya nje zimeathiri usalama, siasa na uchumi wa nchi. Kama alifanikiwa basi naomba nikosolewe kwa kuoneshwa maana niko tayari kujifunza. Lakini kunitukana mimi au kumtukana huyu mama hakusaidii nchi hii,.....
 
Yaani huu unyonyaji dhidi ya Tanzania uanze tu awamu ya tano ???
Mjamaa Nyerere mbona alishirikiana sana na dunia ???
Alikuwa haogopi kunyonywa ???
Labda kichwa changu bado cha moto sana...na labda maelezo ya mleta mada sijakamata sawa sawa. Ngoja kichwa kipoe kwanza naweza kuona tofauti na ninachokiona.

Lakini kwa hali niliyonayo sasa kuna viashiria vingi vinavyofanana na sababu alizoziyotoa Blaise Compaore kuwa alilazimika kushiriki kumuua rafiki yake wa toka utotoni ndugu Thomas Sankara aliyekuwa rais kijana wa Burkina Faso. Moja ya sababu ikiwa ni Sankara alikuwa anaikasirisha Ufaransa kwa matendo yake ya kuwatetea waburkinabe!

Nasema ngoja kichwa kipate baridi naweza kuona tofauti labda.
 
Watu wa Chato waliamini hivyo.
 
Watanzania tuna shida kubwa pahala,...

Mkuu nafikiri ni vyema zaidi uulize ilikuwaje mtu kama jiwe akawa Rais wa Tanzania na maamuzi yake yote kutekelezwa bila kuhojiwa? Kwa sababu yeye ndiye aliyelazimisha msimamo wa kujitenga na “mabeberu na vibaraka wao”.

Mimi hasa ningependa kufahamu mtazamo wako binafsi kuhusu utawala wa Magufuli ulikuwaje na ukoje hivi sasa? Unaweza kurejea michango yako hapa JF kama afanyavyo Pascal Mayalla.

Watanzania wengi hatuna shida katika ufahamu uelewa, tafakuri na mantiki. We’re somehow intelligent and relatively smart. Kama tuna tatizo basi ni kuwa na ustaarabu uliopitiliza na kuthamini sana uhai wetu. We’re ready to be subservient to nasty people rather than annoy anyone and/or physically endanger ourselves.
 
we jamaa ni mjinga kweli yaani watu wapigane kujenga nchi zao. Hafu wewe uwende na pua yako eti uwaite nchini kwako waje kukupa faida hapo ni unyonyaji mtupu hiyo point ya foreign policy na diplomasia hivyo vitakuja tu Cha kwanza ni mazingira. Yaani wewe umwite na umaskini na ujinga aje hafu utegemee equal trade
 
Kinachosikitisha ni kwamba kuna watu hawastuki kabisa.

Unakaa unajiuliza hivi hizi kuna tatizo gani hapa nchini Tanzania.
Tatizo ni kubwa ni elimu
Mwalimu alifanya kosa kubwa sana kutumia kiswahili kama lugha ya taifa ,
Leo hii hata taarifa ya habari ya bbc world watu wanataka watafsiriwe na lufufu au mkandara
Mijadala mingi ya kimataifa kuhusu haki , utawala bora na uhuru wa kujieleza , watanzania hatuijui kinachoendelea ,
 
Jibu lako ni rahisi: kwakutumia unafiki mfano wewe uliyeandika huu Uzi unetumwa na mabeberu
 

Soma tena kisha rejea kuandika comment na si kama utaamua kui edit
 
Ukisha kuwa tegemez utanyonywa tu... Hutaki kunyonywa mwisho wa siku unataka misaada kwao, unataka mikopo, dawa unawategemea, ARV, silaha Sasa kwann usinyonywe.. Magufuli alijarbu kupiga hizo kelele lakn honestly Hawa jamaa tunawategemea kwene kila kona lazima tu watatuendesha..
 
Ndo maana kuna nchi zinaitwa first world na sisi ni third world, get that fact right kwanza kabla ya yote!
Nchi tajiri zina templates kadhaa katika profile zao, wakiamua wanajitegemea, wakiamua wanaweza kututegemea masikini kwa faida zao , wakiamua wanasaidia masikini..kuna wakati nchi hizo zinafanya mamboyote hayo kwa wakati mmoja
hadi leo dawa za kifua kikuu , hiv, zinakuja kama misaada kutoka kwa beberu, meantime copper ya zambia hadi leo hii masoko yake yapo huko huko kwa beberu.
Mama anazunguka huko kwa sababu anajua beberu haipukiki kwa namna yoyote.
She will loose some and win some games katika rounds hizo
 
Labda nikuulize swali. Marekani enzi za Trump ilijitenga na Africa. Vipi enzi za Joe Biden, imejitenga na Africa? Rais Putin katika vipindi vyake vyote vya Urais hajawahi kuja Africa Je, amejitenga na Africa? Mama yetu amejitenga na Asia, Bara Arabu, India na China kwasababu hajaenda huko? Ukinijibu scholarly nikaelewa, nitakuheshimu.
 
Anhaa, kwahiyo mkuu unataka kusema kwamba sera ya mambo ya nje ya Tanzania ilitekelezwa ipasavyo kwasababu ya SGR, mkutano wa SADC, kuongezeka kwa viwanda vya wachina na watalii SI NDIYO ??? Lakini, vipi kuhusu utekelezaji wa International Commitments at Regional and International Levels ambazo tuliziweka kisiasa na zile ambazo ziko kisheria ???

Kuna matatizo mangapi ambayo nchi iliingizwa kwasababu za kutokuwa makini katika kuheshimu hizi international Commitments ??? Kuhusu mambo ya Bilateral Investment Treaties (BIT's) ni mara ngapi tulijiingiza kwenye shida zisizokuwa na ulazima kisa tu kiburi cha mtu mmoja ??? Haya ni baadhi ya mambo ambayo inabidi tuyazungumzie, lakini sioni mtu hata mmoja akiyaleta hapa.

u kuwa karibu na dunia nikujenga bandari ya bagamoyo kwa masharti ya kipumbavu na kubinafsisha Tanesco. Au kusaini bogus treaty
Hakuna nchi inayolazimishwa kusaini mikataba endapo inahisi mikataba hiyo haina manufaa kwa taifa lake. Kila taifa ni Sovereign na Signin of Treaties falls within a scope of sovereign prerogatives. Pia hata kujitoa kwenye mikataba nayo ni Sovereign Prerogative, nchi inaweza kuamua kujitoa. Sisi tunachokataa ni kujitoa bila kuwa na mkakati, kudanganya umma au kutaka umaarufu.

Katika kusoma kwangu kote hata nchi kama Serikali za nchi kama Uingereza huwa hazishindi kesi dhidi ya wawekezaji endapo pale serikali imeamua kujitoa bila kufuata mkakati maalumu. Kama tunaikataa hii mikataba basi lazima tuje na mkakati na siyo kukurupuka hapa, mwishowe tunakuja kupata madhara kama yale yaliyotukuja kisa tulivunja baadha ya BIT kwa kukurupuka.

Daaah, hili swali huwa nilikuwa nakutana nalo kila nilipokuwa nafundisha International Law kwa wanafunzi wa mwaka wa pili. Ntakujibu kwa kufupi kabisa: International Relations cross-cuts many issues other than peace and security, it touches investment issues, health issues, international monetary systems, markets, culture etc.

Kilichotokea kwa Lumumba siyo kitu kuzuri hata kidogo, na kilidhihirisha udhaifu wa mfumo wetu wa dunia ambao uko mpaka leo hii. Lakini busara ni ipi, tuendelee kujitenga na kujificha au sisi kama bara la nchi masikini tuungane ili kusaidiana kubadilisha mifumo ya dunia ambayo inatukandamiza ??? Tanzania ilipoteza pesa nyingi sana katika kusaidia nchi za Afrika kupata Uhuru, lakini unafahamu faida za kiusalama ambazo nchi ilizipata kutokana na ule uwekezaji ???

Swali la msingi kijiuliza: Kikwete na Mkapa walifanikiwa sana kuendeleza hii tunu tulioachiwa na Baba wa Taifa. Je Raisi Magufuli alifanikiwa kufanya hivyo au alishindwa ???

Kaa chini fikiri.....

Dunia hii ya leo huwezi kutengeneza ya ndani bila kutengeneza ya nje pia, maana kila kitu ambacho kinakuja ndani ya nchi hutoka nje. Kiasilia, taifa ambalo huwa tajiri ni lile ambalo linafanikiwa sana kuuza bidhaa zake nje ya nchi kwa kiwango kikubwa, na lile ambalo linafanikiwa kuvutia mitaji ya nje kwa kupitia uwekezaji. Sasa ili ufanikiwe katika hili ni lazima uwe unafahamu fika mfumo mzima wa masoko ya dunia na michezo michafu ambayo mabeparu hucheza.

Nikikuuliza Sera ya uwekezaji na viwanda ya Tanzania kwa miaka mitano iliyopita ilikuwa ni ipi hutanijibu kabisa. Mkakati ambao ulitekelezwa vizuri ni ujenzi wa miundo mbinu, katika hili lazima tukubali kwamba Raisi Magufuli alijitahidi sana , lakini huko kwingineko hebu mnifundishe zaidi
 
Nakwanini unyonywe? Kunyonywa ni ujinga wa mnyonywaji ...Dunia ya leo watu wanasaka fursa kama kwako ipo watakuja issue unajua kutetea maslahi yako? Sasa nyie mmemezeshwa Ujinga kwamba dawa kurudisha mpira kwa kipa ujinga
 
Tanzania ilipoteza dira baada ya Nyerere kufariki.

Awamu ya tatu na ya nne Tanzania lost its soul ikabakiza historia ya marehemu.

2015 hivi aliyeruhusu Magufuli awe rais alikuwa anawaza nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…