Imani hizi! Je, unajua kanisa linaitwa "Chanzo halisi?

Linaitwa Kanisa halisi la Mungu baba. Lilianzishwa baada ya mpasuko kwenye kanisa la The Pool of Siloam.

Sasa hawa kanisa halisi la Mungu baba ndio wamewazidi nguvu wale Siloam na sasa wanajulikana zaidi wao.
Mchungaji wao anaitwa nani?
 
Walikuwa maeneo ya Mbezi enzi hizo, kuna jamaa yetu alijikuta anatoa uwanja wa familia yake sadaka.
Jua na mwezi kwao ni vyombo vya kutambikia
Arusha wapo Tanga wapo sare ni mavazi meupe pee na viatu veupe
Kwa sasa wanakwambia kuhiji ni kigoma siyo Israel tena
Kwaiyo watu kigoma jiandaeni kupokea watalii.
 
Dini inaweza kuwa na nguvu kubwa kwa watu kwa sababu huleta mwelekeo, tumaini, maadili, na faraja kiroho. Mara nyingi, imani na mafundisho ya dini huwa na athari kubwa katika maisha ya watu na huwapa mwongozo katika maamuzi yao na jinsi wanavyoona ulimwengu.
 
Mbona bado. Ndio kwanza kumekucha jiandae kushangaa zaidi[emoji3]
 
Na ndio kazi ya dini. Usalama ni kujificha kwa Yesu tu hamna namna. Yesu ndiye Nuru ya ulimwengu. Anayemfuata hawezi kwenda gizani kamwe!
Yaani wanaomfuata Yesu hawako masikini, hawako mafukara, hawaugui magonjwa, hawafilisiki?
 
Nimejikuta natazama Star tv nikakutana na kipindi mubashara cha ibada ya hili kanisa, Nimeahangaa sana

1. Mavazi ya waumini ni meupe tu, hauruhusiwi kuvaa nguo rangi tofauti na nyeupe!

2. Marufuku kutaja Neno 'MUNGU' au 'YESU' bali wao hutaja neno 'Chanzo halisi' mfano, Asifiwe chanzo halisi, Tunampa sifa chanzo halisi, Damu safi halisi ya mnyama n.k

3. Marufuku kushika Biblia, kwa kifupi hawaamini katika Biblia

4.Hawaamini katika Yesu kristu, Kwa maana hiyo sio wakristu.

5.Kiongozi mkuu anaitwa Baba halisi

6.Nyimbo zote na sifa zinaelekezwa kwa chanzo halisi

7.Sadaka zinatolewa kwa madaraja na ndani ya bahasha

Na mambo mengine ya kushangaza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…