"Ni sehemu ya nafsi ya Mungu" na "Ni Mungu aliyekuja duniani katika umbo la kibinadamu" hizi ni kauli mbili zenye zenye muktadha tofauti kabisa.
Na hakuna mahali penye biblia ambapo Yesu aliwahi kukiri/kusema kuwa yeye ni Mungu.
Bali alikuwa akijiita kuwa yeye ni mwana Mungu, au mwana adamu.
Na hata yeye alionekana akimwomba Mungu, sasa huwezi kunambia Mungu anajiomba yeye, how come ?
"Eee Baba, ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, au isipowezekana basi mapenzi yako yatimizwe"
"Eloi eloi lama sabakthani', yaani Mungu wangu Mungu mbona umeniacha" ?
Hivi Mungu anaweza kujiomba mwenyewe.
Siku tuki bahatika kwenda mbinguni lazima tukute Yesu na Mungu ni vitu viwili tofauti.
Hauwezi kumkuta Mungu tu umkose yesu eti akuambie Yesu ndiyo mimi huyo huyo niliyekuja duniani kimwili, hicho kitu hakipo