Maulid Mubaraq good people.
Naandika uzi huu tucheke kidogo tupoze machungu ya Ima.
Ni hivi,miezi kadhaa nyuma tuli update kiji mansion chetu interior na exterior.Tuliweka vi udambwi udambwi vingi vya kurembesha nyumba na hakika palivutia.Vijana walikua wakipita lazima wapate selfie.
Hata hivyo furaha ya kufurahia mazingira yetu mapya yalikatishwa ghafla na jirani yetu mmoja.
Huyu jirani ni mtumishi mzito wa uma na ni mstaarabu ila mke wake sijui alimuokotea wapi.Ni mswahili na malezi ya watoto ni -0 .
Wana watoto 6 wasiotulia getini kwao.Kutwa kuzurura mitaani saa ingine hadi giza linaingia wapo mtaani na mama tao anaona sawa tu na hv baba yao kila mara yuko safari ni huzuni.
Sasa hawa madogo wakawa kazi yao kuharibu na hawakanyiki.Wakiharibu anaitwa fundi anarekebisha then wanaharibu tena.
Mume wangu akaongea na huyo mzee wawacontrol watoto wanatufanyia uharibifu.Mzee akasikitika sana akaomba samahani na akataka kulipa Mr. wangu akakataa akasisitiza tu watoto wadhibitiwe.Mzee alipofika kwake akawanyuka sana wanae. K
Kesho yake yule mama alivyoona mzee wake na Hubby wangu wameenda kazini akasimama karibu ya geti yetu akawa ananichamba kimafumbo kuwa nina roho mbaya sipendi watoto,kwamba yeye hajawatuma waharibu na kama nataka nimwambie baba yao awachape kila siku au aweke mlinzi wakuzuia wasitoke kucheza mana yeye hiyo kazi haiwezi.Sikumjibu coz namuogopa kwa mdomo mchafu..
Baada ya wanae kuchapwa na baba yao ndo uharibifu ukazidi hadi Mr wangu akasema haiti tena fundi coz hela zinaharibika bure coz kila vikirudishiwa wanavitoa tena.Roho ikanouma sana.
Sasa siku moja mwanangu akanambia kapata idea ya kufanya yule mama azuie watoto wake wasije tena kuharibu.Akanambia mama tutishie kuwaloga.Nikamwambia how.Akasema subiri utaona.
Kuna chungu kikubwa kilikua jikoni hakitumiki akakichukua akaingia nacho chumbani kwake kikiwa kimejaa mchanga na baada ya muda akatoka nacho akakiweka chini mbele yangu
Nilichoka!!
Juu ya kile chungu kulichomekwa kimdoli cha vijiti vimezungushiwa kitambaa chekundu then kimefungwa yai ndo kichwa .Lile yai lilichorwa macho na mdomo kwa marker pen ya kijani na yule mdoli alizungukwa na vimishumaa vinne.
Akanambia mama,tukiweka hiki chungu pale nje naamini kina fulani hawatakuja tena kuharibu.Nikamwambia ngojea baba akirudi na yeye umueleze idea yako.
Mr. wangu alivyoingia tu sebuleni na kuona kile chungu aliruka kwa mshituko.Mimi na dogo tukamcheka sana.Dogo alivyomuelezea plan yake na yeye akacheka sana akasema hata yeye anaamini itasaidia akiweke.
Dogo akaenda kuweka kile chungu kule nje.Haikuchukua muda tukaanza kusikia wqpita njia wakiongea,mara si jini hili jamani,mara eeh watu hawajifichi siku hizi wanaloga hadharani,mara eeh msione majumba haya mkatamani yana siri nyingi.Mara hawa wanaiba nyota za watu washenzi hawa sipiti tena hapa.Mara unasikia sijui Adhu Billah min shetwain Ra jim.
.Sisi tuko kwa ndani tunakaukia kucheka.
Sasa basi,tokea kile chungu kikae pale wale watoto hawatoki tena getini kwao.Mtoto akigusa tu geti lao ili atoke unasikia' we mbuzi toa miguu kwenye hilo geti kama sijaikata!Sitaki mabalaa mimi.😃.
Na hakuna kitu kimeharibiwa tena.Mwanzoni ilikua hata ua likichanua tu linachumwa au linang'olewa ila sasa hv maua yangu yamechanua hayaguswi.
Ujinga ni mtaji kwa mwerevu.