Imebaki miaka 18 mafuta kuisha United Arab Emirates

Imebaki miaka 18 mafuta kuisha United Arab Emirates

Baada ya sakata kuendelea kupamba moto huku na huku. Imenibidi nianze kuifuatilia United Arab Emirates. Nimefuatilia historia yao na mimefuatilia uchumi wao.

Chanzo kikubwa cha mapato katika nchi yao ni mafuta. Hiki ndicho chanzo kikubwa cha mapato.

Sasa cha kushangaza kabisa ni kutokana na mafuta kuisha. Kulingana na estimate za kitaalam mafuta hayo ndani ya miaka 18 yatakuwa yameisha.

Ka nchi ni kadogo na jangwa kila kona. Wanaona kabisa anguko lao linakuja kwa kasi.

Dalili za Nauru zinawanukia kwa kasi. Sasa wanatafuta kwa nguvu zote na kwa hila zote makoloni au ardhi katika nchi zingine.

Wanajaribu kutengeneza artificial tourism na vitu vingine vingi ili kuweza kujinusuru. Lakini kusema kweli anguko lao li karibu. Ndani ya miaka 18 tutashuhudia mengi mno yakiwapata.

Sisi kama nchi hatutakiwi kabisa kutumia natural resources zetu kwa pupa. Zipo wala haziozi. Tuzitumie kwa umakini sana.

Nitaendelea kueleza na kuleta references.
Dubai mafuta yaliisha siku nyingi tu, na wala hawategemei mafuta, Real estate tu ya Dubai nusu mwaka tu ameingiza $28B ambazo ni zaidi ya Trilioni 60 za madafu, kwa mwaka wanaingiza Zaidi ya Trilioni 100 kwenye majengo tu.

Ni ujinga kudhani sehemu ambayo chini ya asilimia moja ya mapato yake yanatokana na mafuta eti itakufa sababu mafuta hakuna.
 
Swali zuri ..hivi Dubai Kabla ya mafuta palikuwaje?
Dubai kabla ya Mafuta ilikua ni Hub ya Biashara, miaka na miaka Wahindi, Wa Iran, Watu toka Africa walifanya biashara pale,
Picha Za Dubai kabla ya mafuta
images (20).jpeg

images (19).jpeg

Hata Uingereza alipo kwenda hapa hakutawala, bali waliingia mikataba ya Ushirikiano hasa kukomesha pirates baharini ili biashara ziendelee.
 
Kweli tunawacheka UAE leo
Wao wamewekeza sana kwao na miradi na viwanda vya kila aina
Dunia inahamia kwenye magari ya umeme na hapo kuna batteries za magari ambapo wanaweza kuwa na viwanda pia hata vya magari
Sisi tunapambana kuwa na mlo mmoja tu
Hawategemei mkataba mmoja kwani kama ni njaa wachina wamemaliza misitu na kuiba rasilimali za Africa bila mikataba ya milele bali wanachota kama kwao

Waarabu wamenunua makampuni ya ulaya mengi sana na hata nusu ya majengo ya London ni ya kwao pamoja na makampuni

Sisi wenye dhahabu kila sehemu hatuna hata duka moja Dubai wala Paris

Halafu tuna uwezo wa kuwasema wao eti mafuta yanaisha

Sisi hata maji mwanza ya tabu wakati maji yamejaa
Wao unafikiri maji wanachota ziwa nyasa?

Tujiangalie sisi na tujiulize tunaenda wapi
Kwa faida ya wengine Mubadala ambayo ndio hela za Uae kwa ajili ya kuwekeza Nje zimewekeza makampuni zaidi ya 200, tena kampuni za maana kama
-Telegram
-reliance jio mtandao wa India
-Global foundries watengenezaji Processor
-Softbank walimiliki Alibaba na Aliexpress
-JD duka kubwa la china
-wana share Wymo kampuni ya Google etc

Kwa Ujumla Mubadala pekee inamiliki Mali zenye thamani zaidi ya Dola Bilioni 300

Hiki ni Ki nchi kidogo chenye watu milioni 1 tu.
 
Nimeona nzi wameingia hapa. But mimi nawagonga kwa facts.
 
Zikiisha huko watahamia huku afrika
Kujichotea rasilimali tu,maisha yao yataendelea kama kawaida

Ova
 
Zikiisha huko watahamia huku afrika
Kujichotea rasilimali tu,maisha yao yataendelea kama kawaida

Ova
Hawana akili hiyo mzee. Si unaona mwenyewe mikataba ya kidwanzi. Mtu mwenye akili hawezi kuja na mkataba wa hivyo.
 
Dubai mafuta yaliisha siku nyingi tu, na wala hawategemei mafuta, Real estate tu ya Dubai nusu mwaka tu ameingiza $28B ambazo ni zaidi ya Trilioni 60 za madafu, kwa mwaka wanaingiza Zaidi ya Trilioni 100 kwenye majengo tu.

Ni ujinga kudhani sehemu ambayo chini ya asilimia moja ya mapato yake yanatokana na mafuta eti itakufa sababu mafuta hakuna.
Salamaleko
Screenshot_20230821-064555.png
 
Kabanga nickel inatarajiwa kuzalisha zaidi ya tani 40,000 kwa mwaka itakuwa inatema zaidi ya dollar billion mbili kwa mwaka lakini Ngara ndio wilaya maskini kabisa, na wana umeme wa maporomoko ya Rusumo mkubwa kuliko kidatu unasambaza nchi tatu , tumelogwa I guess
 
Waislam wametawala nchi hii miaka 15. Ndio maana umaskini umekuwa mwingi.
 
Waislam wametawala nchi hii miaka 15. Ndio maana umaskini umekuwa mwingi.
Hapa sasa unaharibu Mkuu,Japo sijui kama umemaanisha au umeongea kimasihara.
Ila uzi ni mzuri nilikuwa nasoma tu maoni ila hii sijaipenda.
 
Mijitu mengine mijinga nikuulize wewe umefaidika na nini na rasilimali zilizokuwemo nchini kwako? tz tuna kila aina ya madini na gesi yenye thamani ya mabilioni ya dola lakini hutafaidiki navyo,warabu ata mafuta yakiisha leo hawaweezi kufilisika wale wanajua kutumia rasilimali zao kuwanufaisha.

Wewe kweli Mamluki!

Kwahiyo Kama mleta mada hajawahi kunufaika binafsi na rasilimali za nchi basi azamishe kichwa chini kama mbuni au sio?

Halafu huduma za miundo mbinu, afya na elimu unadhani vinaendeshwa kwa kodi kwa asilimia ngapi na kwa maliasili ya taifa asilimia ngapi?
 
Kweli tunawacheka UAE leo
Wao wamewekeza sana kwao na miradi na viwanda vya kila aina
Dunia inahamia kwenye magari ya umeme na hapo kuna batteries za magari ambapo wanaweza kuwa na viwanda pia hata vya magari
Sisi tunapambana kuwa na mlo mmoja tu
Hawategemei mkataba mmoja kwani kama ni njaa wachina wamemaliza misitu na kuiba rasilimali za Africa bila mikataba ya milele bali wanachota kama kwao

Waarabu wamenunua makampuni ya ulaya mengi sana na hata nusu ya majengo ya London ni ya kwao pamoja na makampuni

Sisi wenye dhahabu kila sehemu hatuna hata duka moja Dubai wala Paris

Halafu tuna uwezo wa kuwasema wao eti mafuta yanaisha

Sisi hata maji mwanza ya tabu wakati maji yamejaa
Wao unafikiri maji wanachota ziwa nyasa?

Tujiangalie sisi na tujiulize tunaenda wapi

Sentensi yako ya mwisho kabisa, uko sahihi sana.

Lakini, ni kwa mujibu wa nani kwamba ukishindwa kutumia rasilimali zako Kama nchi basi suluhisho ni kuingia mikataba ya kudumu na ya kinyonyaji na nchi nyingine waweze kuvuna kutoka katika hizo rasilimali?

Kwamba wewe mwenye nyumba na family yako mmeshindwa kula mahindi ya shamba lenu basi jirani aingie ayale na kusaza kwa muda husiokua na kikomo na wanao wakihoji unakua mkali?!

Sio busara kuingiza nchi na wananchi utumwani kwa sababu zisizo na mashiko.
 
Kuwa maskini ndo uzalendo wa mtanzania......

Utakuwa unajidanganya kwa kuamini unaweza kuendelea bila ushirikiano na watu wengine....kwenye biashara kuna kitu kinaitwa corporate business

Yes, ushirikiano ndio msingi katika kutafuta maendeleo na mafanikio katika jambo lolote maana Utu wa mtu huletwa na watu.

Lakini mipaka ya ushirikiano inatafsiriwa vipi katika huu mkataba wa uwekezaji husio na kikomo katika Bandari?

Ushirikiano unatafsiriwa vipi ikiwa mwenye mali akihoji kuhusu matumizi ya mali zake anaonekana mkorofi?
 
Back
Top Bottom