Imebaki miaka 18 mafuta kuisha United Arab Emirates

Imebaki miaka 18 mafuta kuisha United Arab Emirates

Hao jamaa wana akili kuliko sisi ndiomaana tumewazidi rasilimali na wao wametuzidi utajiri,

Mtu mwenye akili kuliko wewe hawezi kutegemea vitega uchumi vyako wewe husie na akili kuendesha maisha yake, vinginevyo hana akili ila ni mjanja na mlaghai .
 
Indeed tuna majitu majinga sana, tuna gas ya matrillion lakini wananchi wengi bado wanatumia kuni, imagine gas kama ile bado tuna migawo ya umeme na uliopo ni very expensive, tuna ardhi safi, maziwa na mito ya kuzalisha mpaka tukauza nje lakini hata mafuta ya kula na sukari tunaagiza kutoka nje, dhahabu tunachimba tangu 90's lakini hatuna hata dollar ya kuagiza mafuta, hatuna cha kuonyesha kwa huo utajiri zaidi ya mashimo waliyotuachia mabeberu, sasa wanataka kuuza bandari, maziwa na anga, hawa mbwa wata control mpaka maji yetu ya kunywa au ya kilimo tusipoangalia, DP ikataliwe kwa nguvu zote
... lango (entry/exit) likishadhibitiwa na third-party umekwisha! Hawa CCM sijui wana akili za aina gani.
 
Kwa faida ya wengine Mubadala ambayo ndio hela za Uae kwa ajili ya kuwekeza Nje zimewekeza makampuni zaidi ya 200, tena kampuni za maana kama
-Telegram
-reliance jio mtandao wa India
-Global foundries watengenezaji Processor
-Softbank walimiliki Alibaba na Aliexpress
-JD duka kubwa la china
-wana share Wymo kampuni ya Google etc

Kwa Ujumla Mubadala pekee inamiliki Mali zenye thamani zaidi ya Dola Bilioni 300

Hiki ni Ki nchi kidogo chenye watu milioni 1 tu.
Yaani masikini wa mwisho anapomcheka tajiri
Asante kwa kuongezea hili
Mtu akiwa masikini sijui kwa nini na roho inakuwa ya kishetani

Ndio maana kwenye dua tunaomba Mungu atuepushe na umasikini
 
Baada ya sakata kuendelea kupamba moto huku na huku. Imenibidi nianze kuifuatilia United Arab Emirates. Nimefuatilia historia yao na mimefuatilia uchumi wao.

Chanzo kikubwa cha mapato katika nchi yao ni mafuta. Hiki ndicho chanzo kikubwa cha mapato.

Sasa cha kushangaza kabisa ni kutokana na mafuta kuisha. Kulingana na estimate za kitaalam mafuta hayo ndani ya miaka 18 yatakuwa yameisha.

Ka nchi ni kadogo na jangwa kila kona. Wanaona kabisa anguko lao linakuja kwa kasi.

Dalili za Nauru zinawanukia kwa kasi. Sasa wanatafuta kwa nguvu zote na kwa hila zote makoloni au ardhi katika nchi zingine.

Wanajaribu kutengeneza artificial tourism na vitu vingine vingi ili kuweza kujinusuru. Lakini kusema kweli anguko lao li karibu. Ndani ya miaka 18 tutashuhudia mengi mno yakiwapata.

Sisi kama nchi hatutakiwi kabisa kutumia natural resources zetu kwa pupa. Zipo wala haziozi. Tuzitumie kwa umakini sana.

Nitaendelea kueleza na kuleta references.
Hawa wanaweza kutumia hata mabavu inavyoashiria sasa. Hasa ukichanganya na wadini uchwara wasiojitafakari!
 
We ndo mana unaitwa kilaza una google google tu hata huelewi maana zake.

Chukua kilichoandikwa hapo juu kwenye screenshot yako Dubai ilipeak 1991 kwa kuproduce barel 400,000 kwa siku hizo ni data za zamani siku hizi hawana uwezo huo ila kukuelewesha zinatosha.

Zidisha 400,000 x 100 unapata thamani ya barel kwa siku ni Dola 40,000,000 Zidisha kwa siku 365 Unapata Dola Bilioni 14.

Gdp ya Dubai ni Dola Bilioni 500 hebu nielezee Genious kama mafuta hayafiki hata Dola Bilioni 20 hizo zaidi ya Dola Bilioni 400 na zaidi zimetoka wapi?.
 
Mdogo wangu mimi ni kichwa Math. Je, unajua calculus?
 
Dalili za Nauru zinawanukia kwa kasi. Sasa wanatafuta kwa nguvu zote na kwa hila zote makoloni au ardhi katika nchi zingine.
Ndio maana wanakuja kwa kasi Africa na viongozi wetu bila aibu au soni wanagawa raslimali zetu kwa" vipande vya fedha"
 
We ndo mana unaitwa kilaza una google google tu hata huelewi maana zake.

Chukua kilichoandikwa hapo juu kwenye screenshot yako Dubai ilipeak 1991 kwa kuproduce barel 400,000 kwa siku hizo ni data za zamani siku hizi hawana uwezo huo ila kukuelewesha zinatosha.

Zidisha 400,000 x 100 unapata thamani ya barel kwa siku ni Dola 40,000,000 Zidisha kwa siku 365 Unapata Dola Bilioni 14.

Gdp ya Dubai ni Dola Bilioni 500 hebu nielezee Genious kama mafuta hayafiki hata Dola Bilioni 20 hizo zaidi ya Dola Bilioni 400 na zaidi zimetoka wapi?.
Ngoja nikupatie maelezo marefu kidogo kuhusu ndugu zako. Na ujue kuwa hawana future

Baadhi ya hatari kuu ambazo zinaweza kuathiri uchumi wa UAE siku za usoni ni:

1. Mabadiliko ya Bei ya Mafuta: UAE inategemea sana mauzo ya mafuta, na mabadiliko ya bei ya mafuta yanaweza kuathiri sana uchumi wake. Kupungua kwa bei ya mafuta kunaweza kusababisha mapato ya serikali kupungua, nakisi ya bajeti, na hata kusababisha mdororo wa uchumi.

2. Utulivu wa Kisiasa: UAE iko katika eneo lenye mizozo ya kisiasa, na ongezeko la migogoro au mvutano wa kisiasa Mashariki ya Kati kunaweza kuathiri vibaya uchumi wake. Hatari hizi ni pamoja na migogoro ya kikanda, mzozo wa biashara, na vikwazo, ambavyo vinaweza kuvuruga biashara na kuathiri imani ya wawekezaji.

3. Mkwamo wa Uchumi wa Kimataifa: Kama uchumi unaotegemea sana biashara ya kimataifa, UAE inaweza kuathiriwa na kupungua kwa uchumi wa kimataifa. Kupungua kwa uchumi katika nchi kubwa kama Marekani, China, au Ulaya kunaweza kuathiri mahitaji ya bidhaa za UAE, utalii, na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI).

4. Utegemezi kwa Wafanyakazi Kutoka Nchi Za Nje: UAE inategemea nguvu kazi kubwa ya wahamiaji katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ujenzi, ukarimu, na huduma. Mabadiliko katika sera za uhamiaji, sababu za kisiasa, au hali ya kiuchumi katika nchi za asili zinaweza kuathiri upatikanaji na gharama ya ajira, na hivyo kuathiri shughuli za biashara na ukuaji wa uchumi.

5. Hatari katika Soko la Makaazi: UAE imekuwa ikishuhudia ukuaji mkubwa katika sekta ya ujenzi, hasa Dubai na Abu Dhabi. Hata hivyo, ukuaji haraka na tabia ya kubahatisha inaweza kusababisha uwepo wa wingi wa nyumba, marekebisho ya bei, na hatari za uwezo katika sekta ya benki ikiwa thamani ya mali ishuke kwa kiasi kikubwa.

6. Mabadiliko ya Tabianchi na Upungufu wa Maji: UAE inakabiliwa na upungufu wa maji na ni hatari kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa usawa wa bahari na matukio ya hali ya hewa kali. Changamoto hizi zinaweza kuathiri kilimo, miundombinu, na uendelevu wa uchumi kwa ujumla, na hivyo kuhitaji uwekezaji katika usimamizi wa maji na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

7. Kuvurugika kwa Teknolojia: Ingawa UAE imekuwa mstari wa mbele katika kukumbatia teknolojia na uvumbuzi, maendeleo ya haraka na kiotomatiki yanaweza kuvuruga sekta za jadi na soko la ajira. Nchi inahitaji kuendelea kubadilika na kuwekeza katika kuendeleza nguvu kazi yenye ujuzi ili kupunguza mabadiliko yoyote ya kuzorota.

8. Magonjwa na Hatari za Afya: Mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza, kama janga la COVID-19, yanaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi. Kuvurugika kwa usafiri, biashara, na utalii kunaweza kuathiri sekta muhimu za uchumi wa UAE,kama vile anga za ndege, ukarimu, na rejareja.
 
Mtu mwenye akili kuliko wewe hawezi kutegemea vitega uchumi vyako wewe husie na akili kuendesha maisha yake, vinginevyo hana akili ila ni mjanja na mlaghai .
Duuuh! Ndio umeandika upuuzi gani hapa? Nani anategemea rasilimali zako kuendesha maisha yake? Achana na stori za vijiweni wewe ishi kwenye uhalisia, wewe unategemea utalii ila mwenzio anaingiza pesa nyingi kwenye utalii kuliko wewe
 
Nilifika nchi moja hivi huko nje. Ni tajiri na wanakila kitu. Nikaingia katika duka la sonara nilikuwa na mkufu wangu wa silver nilihitaji usafishwe.
Ndipo nikapata kuongea na yule sonara alikuwa ni mtu mzima hivi mpersia alie hamia miaka mingi Ulaya toka miaka ya 70.

Alinambia unajua hii nchi wana dhahabu nyingi tu. Sikumuelewa. Nikamwambia mbona hawachimbi? Ndo akanambia wazungu wajanja. Dhahabu yao wamehifadhi kwa vizazi vijavyo. Ndo maana hawataki ichimba sasa.
Hapo hapo nikamkumbuka Mwl. Nyerere alie sema ni heri tusichimbe madini yetu. Siku vizazi vyetu wakipata ujuzi watachimba wao.

Mkapa akamuona Nyerere mjinga akaamua kuleta wawekezaji. Walichimba hadi meneo mengine tayari madini kadhaa yameisha, tumebakiwa na mashimo makubwa hata kufukia huwezi.

Ndo maana Nyerere kwenye migodi aliweka kambi za jeshi na kuanzisha hifadhi za wanyama kuliko kuwa na madini.

Nilishituka na kauli ya mama Samia mapema sana, alipotwaa madaraka akasema madini hata kama yako mbugani lazima tuyachimbe. Wataweka wawekezaji. Roho iliniuma sana. Toka hapo niliona huyu mama kaja kutapanya na kuharibu mali ya wa Tanzania. Nilijua hatuna kiongozi.

Nilijaribu kuandika humu lakini ilifutiliwa mbali. Ushabiki ni mbaya ebu watanzania tuwe na uchungu na maliasili ya nchi yetu. Kuna kundi la uongozi wapo kujinehemesha kwa namna yoyote wao na familia zao. Wakati nchi inauzwa. Alisema Ndungai ila kwakua tunaushabiki tulimtukana na kumuona hafai.

Huyu mama au Rais Samia hana mema na Tanzania, kuna ndoto nilimuota, narudia huyu mama si mtu mzuri. Anaongea maneno matamu lkn moyo wake huko mbali. Na nirahisi kutumiwa ili kugawa maliasili zetu.
"Madini hata kama yako mbugani lazima tuyachimbe. Wataweka wawekezaji. Roho iliniuma sana. Toka hapo niliona huyu mama kaja kutapanya na kuharibu mali ya wa Tanzania. Nilijua hatuna kiongozi."
Daaaah Duniani wawili wawili hiii kauli namimi ilifanya niwaze kama wewe.
 
Baada ya sakata kuendelea kupamba moto huku na huku. Imenibidi nianze kuifuatilia United Arab Emirates. Nimefuatilia historia yao na mimefuatilia uchumi wao.

Chanzo kikubwa cha mapato katika nchi yao ni mafuta. Hiki ndicho chanzo kikubwa cha mapato.

Sasa cha kushangaza kabisa ni kutokana na mafuta kuisha. Kulingana na estimate za kitaalam mafuta hayo ndani ya miaka 18 yatakuwa yameisha.

Ka nchi ni kadogo na jangwa kila kona. Wanaona kabisa anguko lao linakuja kwa kasi.

Dalili za Nauru zinawanukia kwa kasi. Sasa wanatafuta kwa nguvu zote na kwa hila zote makoloni au ardhi katika nchi zingine.

Wanajaribu kutengeneza artificial tourism na vitu vingine vingi ili kuweza kujinusuru. Lakini kusema kweli anguko lao li karibu. Ndani ya miaka 18 tutashuhudia mengi mno yakiwapata.

Sisi kama nchi hatutakiwi kabisa kutumia natural resources zetu kwa pupa. Zipo wala haziozi. Tuzitumie kwa umakini sana.

Nitaendelea kueleza na kuleta references.
Hivi wewe kweli unaijua UAE?
You must be joking.
 
Back
Top Bottom