Imebaki miaka 18 mafuta kuisha United Arab Emirates

Dubai mafuta yaliisha siku nyingi tu, na wala hawategemei mafuta, Real estate tu ya Dubai nusu mwaka tu ameingiza $28B ambazo ni zaidi ya Trilioni 60 za madafu, kwa mwaka wanaingiza Zaidi ya Trilioni 100 kwenye majengo tu.


Ni ujinga kudhani sehemu ambayo chini ya asilimia moja ya mapato yake yanatokana na mafuta eti itakufa sababu mafuta hakuna.
 
Swali zuri ..hivi Dubai Kabla ya mafuta palikuwaje?
Dubai kabla ya Mafuta ilikua ni Hub ya Biashara, miaka na miaka Wahindi, Wa Iran, Watu toka Africa walifanya biashara pale,
Picha Za Dubai kabla ya mafuta


Hata Uingereza alipo kwenda hapa hakutawala, bali waliingia mikataba ya Ushirikiano hasa kukomesha pirates baharini ili biashara ziendelee.
 
Kwa faida ya wengine Mubadala ambayo ndio hela za Uae kwa ajili ya kuwekeza Nje zimewekeza makampuni zaidi ya 200, tena kampuni za maana kama
-Telegram
-reliance jio mtandao wa India
-Global foundries watengenezaji Processor
-Softbank walimiliki Alibaba na Aliexpress
-JD duka kubwa la china
-wana share Wymo kampuni ya Google etc

Kwa Ujumla Mubadala pekee inamiliki Mali zenye thamani zaidi ya Dola Bilioni 300

Hiki ni Ki nchi kidogo chenye watu milioni 1 tu.
 
Nimeona nzi wameingia hapa. But mimi nawagonga kwa facts.
 
Zikiisha huko watahamia huku afrika
Kujichotea rasilimali tu,maisha yao yataendelea kama kawaida

Ova
 
Zikiisha huko watahamia huku afrika
Kujichotea rasilimali tu,maisha yao yataendelea kama kawaida

Ova
Hawana akili hiyo mzee. Si unaona mwenyewe mikataba ya kidwanzi. Mtu mwenye akili hawezi kuja na mkataba wa hivyo.
 
Salamaleko
 
Kabanga nickel inatarajiwa kuzalisha zaidi ya tani 40,000 kwa mwaka itakuwa inatema zaidi ya dollar billion mbili kwa mwaka lakini Ngara ndio wilaya maskini kabisa, na wana umeme wa maporomoko ya Rusumo mkubwa kuliko kidatu unasambaza nchi tatu , tumelogwa I guess
 
Waislam wametawala nchi hii miaka 15. Ndio maana umaskini umekuwa mwingi.
 
Waislam wametawala nchi hii miaka 15. Ndio maana umaskini umekuwa mwingi.
Hapa sasa unaharibu Mkuu,Japo sijui kama umemaanisha au umeongea kimasihara.
Ila uzi ni mzuri nilikuwa nasoma tu maoni ila hii sijaipenda.
 

Wewe kweli Mamluki!


Kwahiyo Kama mleta mada hajawahi kunufaika binafsi na rasilimali za nchi basi azamishe kichwa chini kama mbuni au sio?

Halafu huduma za miundo mbinu, afya na elimu unadhani vinaendeshwa kwa kodi kwa asilimia ngapi na kwa maliasili ya taifa asilimia ngapi?
 

Sentensi yako ya mwisho kabisa, uko sahihi sana.


Lakini, ni kwa mujibu wa nani kwamba ukishindwa kutumia rasilimali zako Kama nchi basi suluhisho ni kuingia mikataba ya kudumu na ya kinyonyaji na nchi nyingine waweze kuvuna kutoka katika hizo rasilimali?

Kwamba wewe mwenye nyumba na family yako mmeshindwa kula mahindi ya shamba lenu basi jirani aingie ayale na kusaza kwa muda husiokua na kikomo na wanao wakihoji unakua mkali?!


Sio busara kuingiza nchi na wananchi utumwani kwa sababu zisizo na mashiko.
 
Kuwa maskini ndo uzalendo wa mtanzania......

Utakuwa unajidanganya kwa kuamini unaweza kuendelea bila ushirikiano na watu wengine....kwenye biashara kuna kitu kinaitwa corporate business

Yes, ushirikiano ndio msingi katika kutafuta maendeleo na mafanikio katika jambo lolote maana Utu wa mtu huletwa na watu.

Lakini mipaka ya ushirikiano inatafsiriwa vipi katika huu mkataba wa uwekezaji husio na kikomo katika Bandari?

Ushirikiano unatafsiriwa vipi ikiwa mwenye mali akihoji kuhusu matumizi ya mali zake anaonekana mkorofi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…